Mabinti wa siku hizi ni hatari kwa afya, wengi watapinga

Mabinti wa siku hizi ni hatari kwa afya, wengi watapinga

MABINTI WA SIKU HIZI

Katika enzi za sasa, mwenendo wa mabinti wa siku hizi unaibua maswali mengi, hasa kuhusu matarajio yao katika mahusiano na maisha kwa ujumla. Imeonekana wazi kuwa baadhi yao wameweka viwango vya juu sana, ambavyo kwa kiasi kikubwa vinaathiri jinsi mahusiano yanavyoendeshwa. Lakini je, matarajio haya ni halali, au yamezidi kiwango cha busara?

Kwanza, mabinti wengi wa kizazi hiki hawaamini kabisa kwenye mchakato wa maendeleo ya hatua kwa hatua. Wao hujikita zaidi katika kufanikisha ndoto zao kwa haraka, mara nyingi kwa njia za mkato. Kwa mfano, mwanaume anapomwendea binti kwa nia ya kumtongoza, matarajio huanza mara moja. Leo hii wametambulishwa kwa jina, lakini kesho tayari matarajio ni ndoa. Wanapuuza hatua muhimu kama kujenga urafiki wa kweli, kuelewana vyema, na kupanga maisha kwa pamoja.

Kwa baadhi yao, ndoa si mwisho wa matarajio, bali mwanzo wa orodha isiyokwisha ya mahitaji. Mara baada ya ndoa, matarajio yanazidi kuwa mazito: nyumba ya kifahari inahitajika, biashara ya familia inapaswa kuanzishwa mara moja, na hata suala la watoto halicheleweshwi. Mwanaume anapojitahidi kutimiza yote haya, bado haitoshi. Mabinti hawa pia wanahitaji wazazi wao wajengewe nyumba za kisasa, kabla hata ya wazazi wa mwanaume kupata nafasi hiyo.

Kilio hakikomi hapa. Mabinti wa siku hizi pia wanataka "uhakika wa maisha," kwa maana ya kujengewa apartments za kupangisha kila wilaya. Wanaona kuwa huo ni uthibitisho wa mapenzi ya dhati. Wakati mwanaume anajitahidi kuimarisha maisha, bado analazimika kufanikisha ndoto za binti huyo kwa muda mfupi sana, bila kujali ugumu wa maisha au rasilimali alizonazo.

Hali inapofika hapa, mwanaume hujikuta amefika mwisho wa uwezo wake, huku akiendelea kukabiliana na shinikizo za familia, jamii, na mke mwenyewe. Cha kushangaza, baada ya juhudi zote hizi, baadhi ya mabinti huanza kudai talaka. Wanaona kuwa wamepata walichotaka, na sasa wanaweza kuendelea na maisha bila mzigo wa ndoa.

Ni wazi kuwa matarajio haya yanajenga mazingira magumu katika mahusiano. Hakuna ubaya kwa binti kuwa na ndoto kubwa, lakini inahitajika busara na subira katika kuzitimiza. Wanaume wanahitaji msaada na ushirikiano badala ya shinikizo lisilo na kikomo. Kwa pamoja, wenza wanaweza kujenga maisha bora yanayoheshimu ndoto na michango ya kila mmoja.

Mabinti wa siku hizi wanapaswa kuangalia upya matarajio yao. Mahusiano yanapaswa kuwa nguzo ya kusaidiana, sio mashindano ya nani anapata nini. Mwisho wa siku, maisha bora yanajengwa kwa upendo wa kweli, subira, na kuheshimiana.

View attachment 3167727View attachment 3167729View attachment 3167730
Tamthilia na mitandao imewapumbaza maigizo na kiki za watu maarufu wanataka kuapply kwenye maisha halisi ya mtaanj
 
Ukiwa na akili Timamu hauwezi ukawa na mawazo ya kutaka kufanya kitu ili umridhishe mtu (mwanamke/mwanaume) hususani kimapenzi.
Huwa nashangaa sana vijana wenzangu wanavyojitutumua ili kuwaridhsha wanawake ama kutafuta uthibitisho(seek validation) kutoka kwao, kwangu huo huwa nauona kama ni udhaifu na upungufu wa akili mwilini.
The more you chase a woman, the more you lose your respect as a man.
 
Binafsi naona kawa Wazazi kuna sehemu tumekosea kwenye malezi yao.

Sote tunafahamu, Kila uozo kwenye jamii asili yake ni kulega lega Kwa familia. Kama watoto watalelewa kwenye misingi mizuri, hayo mambo sio rahisi kuyaona yakitokea.

Mbona Wanawake na mabinti wa zamani ambao ndiyo mama zenu/Bibi zenu hawakuwa hivyo?

Turudi nyuma na kusimamia malezi ya watoto wetu ipasavyo

Vinginevyo tunaandaa Wake na Waume wa hovyo wa baadaye.

Kamwe usitegemee mtoto alelewa na Mama peke yake Kwa kudanga utegemee naye asije kuwa gold digger (mdangaji) akikuwa

Huwezi kupanda Mahindi shambani kwako uje utegemee kuvuna Maharage.

Tunavuna tulichopanda
Kuna asasi za kiraia pia ni changamoto kubwa sana, especially hizi zinazojinasibu kwamba zinalinda haki ya mwanamke, wanamjaza ujinga mtoto wa kike na wanamlinda nanhuo ujinga wake. Mzazi au mkubwa ukiwa mkali utashambuliwa balaa.

Wakati nipo olevel ilikua binti anaesoma akitiwa mimba anafukuzwa myumbani aende kwa aliempa iyo mimba hii ilisaidia kuwa warning sign mabinti wengine, sasa hivi mzazi ukifanya ivyo utaandamwa balaa matokeo yake watoto wa kike wamekua na uhuru wa kufanya chocjote bila kuwa accountable kwenye familia wala jamii.

HIzi taasisi zinazodai zinamtetea haki za wanawake inabidi zifanyiwe review kuangalia kama zinamsaidia mwanamke au zinazidi kudhoofisha nafasi na utu wa mwanamke
 
Umesema sahihi Mkuu, ila pamoja na uwepo wa hizo Taasisi, tujitahidi kama Wazazi kuwalea watoto wetu kwenye misingi imara ya tabia na mwenendo.

Tujiulize mbona miaka ya zamani msichana alikuwa achelewa kuingia Kwenye mahusiano ya kingono tofauti na sasa.

Wengi walikuwa wanaolewa wakiwa hawawajui Wanaume(Hawajawahi kuingiliwa) tofauti na sasa.

Hata watoto wakiume ilikuwa hivyo, unakuwa na rafiki wa kike lakini huwezi kumwingilia hadi uwe na commitment ya kumwoa.
 
Kugeza umagharibi kunatuponza.
 
Kugeza umagharibi kunatuponza.
Ndiyo maana maadili yanashuka Kila Leo

Mwanamke aliyewahi Kulala na Wanaume 15 hata akiolewa hawezi kutulia, kwani Kuna matendo atakuwa alifanyiwa ambapo Mume atakaye kuwa amemwoa anaweza asiwe anafanyia
 
Bila aibu wanaambiana tafuta mume mwenye pesa!
Impliedly maana yake wanataka mwanaume mtu mzima tena mwenye familia.

Kijana under 30 bado anajitafuta hatokuwa na hizo pesa!
 
Prioritize yourself kaka ....fanya yako jijenge timiza malengo yako Kisha ndio uanze deal na ya watu ....

Tuendelee kusubiri mpaka tupate mwanamke alie tayari kujenga pamoja sio kubeba mbao akajenge kwake... yule anaetambua maana ya teamwork sio hizi ng'ombe zilizo Jaa ubinafsi utapeli tamaa na Kamasi kichwani
Sahihi sana mkuu
 
Back
Top Bottom