Vijana mnapaswa mtambue kwamba wanawake wa miaka hii hasa Hawa kisasa waliopo mijini ni watu wenye tamaa sana na wengi wao wanajifanya wako too ambitious, yaani Wana malengo makubwa sana na katika malengo hayo suala la ndoa kwao sio kipaumbele kabisa.
Ukiona mwanamke yeyote wa mjini hususani jijini Dar anaolewa, basi ujue kwenye hiyo ndoa anaingia kimikakati, yaani hiyo ndoa kashachungulia na kuona kwamba ni daraja rahisi la yeye kufikia matamanio yake.
Hapa dar karibu Kila mwanamke unayemuona huko barabarani ana ndoto siku Moja awe anamiliki Nyumba Mbezi beach, awe anamiliki angalau hata magari mawili au matatu ya kutembelea, awe anamiliki Boutique kubwa ya nguo za kike na za kiume huko Sinza, awe anamiliki apartments kadhaa huko kigamboni Tena awe anapangisha wazungu, awe anamililiki mashamba na plots Kadhaa huko morogoro..... Na vyote hivi anataka viwe katika jina lake.
Sasa kutimiza haya natamanio yate kwa Juhudi zao wenyewe binafsi huwa hawawezi, kwa hiyo unakuta wanaingia kwenye multiple relationships na wanaume Kibao lengo ikiwa asaidiwe na wanaume hao kutimiza malengo hayo.... Na pale inapotokea amepata kibopa mwenye hela za kutosha basi ana anafanya haraka iwezekanavyo aolewe na kibopa huyo hili atimiziwe matamanio yake kwa haraka halafu baada ya hapo anaomba taraka.
Vijana mnatakiwa kuwa makini sana na hiki kizazi Cha wanawake wenye tamaa ya Mali na maisha ya anasa, wewe mwanaume wanakuchukulia kama daraja tu la kumfikisha kwenye nchi ya ahadi na usifikiri sijui eti wanakupenda acha ujinga