Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Wakuu
Nchi ina heka heka sana hii vijana kama hawa sidhani hata wanachokiongea kama wanakijua au ni ilmradi tu, yani ni kama wale wale wazee wa lile jiji
===
Katibu Msaidizi wa idara ya Mabinti na Uwezeshaji wa Taasisi ya Mama Asemewe Bi. Beatrice Mwahegili amewataka Vijana hususani Mabinti wa Kitanzania kuheshimu, kulinda na kuitunza amani ya Tanzania, akisisitiza kuwa hakuna Tanzania nyingine zaidi ya hii ya sasa na ni gharama kubwa kurejesha amani pale itakapopotea.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dodoma leo Alhamisi Disemba 04, 2025, amewataka Vijana kuamka na kutokubali kutumika kwa maslahi ya watu wachache, akiwataka pia kuwakataa wale wote wanaohamasisha vitendo vya uvunjifu wa amani nchini.
"Tunapinga vikali maandamano yanayoendelea kuhamasishwa tarehe 09. Tarehe tisa ni siku ambayo Taifa letu lilipata uhuru, si siku ya vurugu au kuhamasisha machafuko katika Tanzania yetu. Tanzania tumezaliwa tukiikuta yenye amani na sisi kama Vijana ni wajibu wetu wa kwanza kuitunza amani yetu. Hatuna Tanzania nyingine na tukiiharibu, hatuna sehemu ya kukimbilia." Amesema Beatrice
Mbele ya waandishi wa habari, Beatrice pia amesisitiza kuwa amani iliyopo nchini ndiyo inayosababisha maendeleo na ustawi wa Mabinti, Vijana na Jamii nzima ya Tanzania pamoja na upatikanaji wa fursa mbalimbali za kiuchumi kwa Vijana na Watanzania kwa ujumla.
"Kipindi cha Rais Samia ametugusa mabinti kwa asilimia kubwa sana kuanzia kwenye Mikopo ya elimu ya Juu ikiwa ni msaada mkubwa kwa Mabinti tuliotokea familia duni, imetuepusha na vishawishi mbalimbali. Rais Samia pia amepanua wigo wa elimu kwa wale wanaopata ujauzito wakiwa shuleni na zaidi tumepewa Wizara ya Vijana itakayobeba maslahi ya sisi Vijana." Ameongeza kusema.
Source Mwendokasi TV