Mabinti wahitimu wa vyuo Amkeni

Umeongea ukweli mzito. Mtoto wa kike akimaliza chuo kinachomtesa home ni kukosa ule uhuru kama wa chuo wa kutoka out kwenda viwanja na groupies za marafiki zake wa kike, kudate na wanaume tofauti, kuletewa offer mara kwa mara, kulala kwa wanaume weekend na kuwa huru kurudi muda anaotaka hostel au sehemu alipopanga.

Ndio maana mabinti wengi wakitoka chuo anachotamani ni apate madanga wampangie chumba au nyumba halafu awe huru hata miaka 5 awe anafanya hata biashara isiyo na faida town ili tu aonekane anaenda town kazini akijiskia asitoke alale tu ndani mradi kupoteza muda kuwa huru. Halafu umri ukienda atokee fala m'moja ampigie goti amuoe aendelee na maisha kawaida.

Balaa kwa mtoto wa kiume, akiwa hajapata ajira na ameshamaliza chuo kitaa watamvumilia mwaka m'moja then baada ya hapo ni mwendo wa kunyanyaswa na kunyanyapaliwa kama vile mtu mweusi kwenye jamii ya wazungu karne ya 18.

Hakuna mtu anakutetea, ukiomba hata buku ya vocha lisala utakayopewa hadi utajiuliza huyu mtu nilishawahi kuwa na hela nikamnyima msaada nini? [emoji23]

Ndugu wanakutenga kauli zao zinakuwa tata wakiongea na wewe mradi tu wakuonyeshe kuwa wewe ni outcast na misfit kwa sasa. Yaani unakuwa unaishi kwa huzuni na msongo mkubwa wa mawazo aisee.

Sasa subiri utoboe ghafla hapo hautaamini wale wale ndugu wanavyogeuka na kuwa upande wako wanajua sasa kuna kitu watapata kutoka kwako. Kimsingi jamii ya sasa inamkandamiza sana mtoto wa kiume kwa makusudi bila huruma na haijali afya yake ya akili wala ustawi wake ila wanataka mgao wa mafanikio yake ikitokea kafanikiwa.

Boychild, jikaze popote ulipo, ukitoboa kula na wale waliokushika mkono tu, hata kama sio ndugu zako wa damu. Kama ndugu zako wa damu walikuletea umafia na wewe waletee umafia somo liwafikie. Hakikisha wanajua kuwa walikukosea. Familia yako ulipozaliwa inatakiwa ikutetee nyakati za shida na unapojitafuta wakupe bega la kuegemea hata uanguke mara ngapi, sapoti ya shida ndogo ndogo kama vocha, pesa ya kula mavazi haitakiwi kuleta maneno kama familia yako wanajimudu wao wanatakiwa kukulinda huku wakikuhamasisha na kukuencourage kujipanga upya na maisha.
 
Ngekewa siku hizi hapatikani kirahisi, hata sisi waganga tunapata shida sana kutengeneza dawa
 
Wanatakiwa watengenezewe mazingira ya kukutana na watu. Ndiyo maana watu wanafanya sherehe zinazokutanisha vijana.
 
Ila unajua hii mental programing hivyo tusiwalaumu. Mtu ambaye amejiandaa kwa miaka zaidi ya kumi kuja kufanya kazi za kiofisi ambazo yeye anaziona ni heshima akizikosa ndicho chanzo kikubwa cha vijana kususa maisha maana wakichoandaliwa kukifanya hakipo kimewakataa.

Inataka ujasiri na kujizima data kuanzia chini tena na manual works au kazi za kuchafuka. Sio kazi rahisi ku dismantle fikra za status ambazo ulishajiaminisha na jamii ilikuaminisha kwa miaka yote ndani ya muda mfupi.

Ndio maana wengi huwachukua several years and several mental breakdowns kukubaliana na uhalisia wa maisha kuwa kile walichoambiwa kilikuwa uongo tu na wazazi na jamii iliwapotosha na kuwapoteza dira kuhusu uhalisia wa maisha.
 
You are talking, ila hili linaua zaidi sisi wa kiume wale pisi kali nyingi zinapumulia katika kupangiwa nyumba na kupewa matumizi na wazee wetu wastaaf
 
KUMBUKA wamama hawajuagi wanachotaka
hao mabinti wakianza mitoko lawama zitaanza tena ,kwamba wanazurura tu, mwisho watawaletea wajukuu
 
Wanataka kuolewa na watu wenye elimu kama wao, hapo waoaji wenye elimu na wenyewe hawana ajira wanaogopa majukumu ya familia. Wengine wanataka wafanyabiashara wakubwa ambao ni catch ya wanawake wengi pengine wazuri zaidi yake.

Note: Sisemi kwamba wanawake hawana haki ya kuchagua, kila mtu ana haki ya kuchagua akipendacho.
 
Wow! Unaishi kwenye jamii gani ambayo wanaume wote wameshajipata na wako tayari kuoa na kubeba majukumu ya kifamilia kikamilifu?? Sio hii jamii ambayo wanaume pia wanastruggle kujitafuta kwa zaidi ya 15 years?

Unaamini kila anayepigania kuolewa basi atafanikiwa kuolewa? Bahati isipokuwa yake akawa hajaolewa je??

Ukiolewa ni guarantee ya kutimiziwa mahitaji yako yote? Have you ever heard women who are single mothers although they are married???

Come on, una binti? Wadogo wa kike je? You can do better with them, ndoa inaweza isiwe destiny, lakini as long as huyu binti yuko hai atatakiwa kumove around, kula, kuwa na makazi etc....... na hayo yanapatikanaje? Lazima kila mtu awe na kipato cha kulipwa au kujilipa!
 

Sasa kama unajua maisha ni ya kustruggle why unasumbua kichwa chako kuamini mwanaume unayetakiwa kuolewa nae anatakiwa kuwa na mafanikio ambayo baba yako miaka yote amekulea hadi sasa ana miaka 60 hajawahi kuyafikia? [emoji848]

Wanaume wapo tayari kubeba majuku ila sio majukumu yankushtukizwa, kupangiwa, kupelekeshwa, kuforce, na kadhalika. Majority wanaume wanashindwa kuishi na wanawake sababu wanawake wanaokutana nao wana mambo mengi sana na wapo speed na tamaa za maisha. Hawana utulivu wa akili na upole wa nafsi ili mwanaume aweze tulia kufanya yake.

Unakuta mwanaume anataka kufocus afanye biashara fulani halafu ikue ili afungue nyingine kwa faida ile ya kwanza wewe mwanamke kazi yako ni kuharibu huo mpango na kuharibu focus yake. Ukiona tu mnabadilisha chakula ushabeba ujauzito bila hata kumshirikisha, ukiuliza unasema kwan yeye hajui kuwa tunafanya mapenzi tupate watoto, wewe hujui siku zako uzicontrol ili mkubaliane lini mtapata watoto?

Mara ulete shida zako binafsi kwenye biashara mara umpe shida za familia yako wakati yeye binafsi unakuta amewalia buyu hata familia yake.


Kwann upiganie kuolewa? [emoji848] Ndoa au kuolewa sio kitu cha kupigania, ukiona unapigania then jua haupo tayari kama mwanamke. Ndoa huwa inakuja yenyewe na mwanaume atakufuata na kukushika mkono akitaka umfuate. Wanaume huwa na ufahari sana akimpata mwanamke aliyemvutia na akamkubali kwa wakati sio kuleta usumbufu na mapozi as if kuna mwanaume anapenda kuchezewa akili na mwanamke m'moja na wakati kuna wanawake zaidi ya milioni.

Nikuulize na wewe usipoolewa ni guarantee ya kupata kila unachokosa ukiwa umeolewa? [emoji848] Ukiishi maisha kwa formula ya kutaka kila unachotaka then utajikuta unafocus kufuta 20% ya hasara huku ukiacha kukinga mikono kupokea 80% ya faida. Take a second think about that.

Unaolewaje halafu uwe single mother, hivi umeelewa hata ulichosema. Ni sawa na useme mtu ambaye hakuwahi kusoma darasani akalia chuo kumtengenezea cheti feki useme ni msomi, alisomea nini na hakukaa darasani? Sasa mtu single mother aliolewaje, au haujui matumizi ya neno Single kwenye mahusiano?

Tufanye kuolewa ni Bahati. Bahati ni matokeo ya maandalizi yanapokutana na fursa. Wewe kama mtoto wa kike na hizi mentality za kuona ndoa ni bora liende umejiandaa fursa ikikutokea mwenzi huu au ndio hadi uanze kublock watu huko WhatsApp, ufunge status kwa baadhi ya watu wasione post zako na mtu mpya, mara uweke yale ma WhatsApp ya hovyo sijui WhatsApp FM , GB.

So wanawake miaka ya nyuma hawakuwa na ajira kama wasasa, waliishi na kula kwa namna gani? [emoji848] Nadhani hapa unamiss the point kuwa maisha ya sasa yanawatoa wanawake kwenye uhalisia wao taratibu bila wao kujijua. Wanawake wachache sana wanaplay role yakuwa mwanamke kwenye jamii ila wengi sana wanaplay roles za kiume of which inawagharimu sana.
 
Kuna muda huwa nadhani majibu yako unayatoa ChatGTP. Una tatizo la msingi la kuchanganya mtazamo wako binafsi na experience za watu wengine. Na je mbona haujibu maswali niliyokuuliza.

Your long a** paragraph sioni inahusiana vipi na ulichoniqoute. Na hapo nilipobold pananihusu mimi? Na je panaihusu comment yangu ya mwanzo?

Sio wewe ndiye uliyesema mwanamke kitu cha kwanza kupigania kiwe mahusiano imara na ndoa? Nikakujibu usipopata ndoa basi angalau uwe na kipato cha kujipa chakula, malazi, na movement, ni wapi nimesema usipoolewa unakuwa umekata ticket ya kupata kila kitu ambaye wa ndoani atakikosa....I'm afraid unatumia experience za wengine kunijibu mimi.

Again, uliskip topic ya comprehension/kusoma kwa ufahamu? Nilipozungumzia single mothers ndani ya ndoa nilimaanisha mwanamke aliyeolewa na ikatokea kwa bahati mbaya au kwa makusudi mumewe akashindwa kuhudumia familia kiasi kwamba ikamlazimu mwanamke kusimamia majukumu yote kifamilia, Sasa huyu mwanamke atawezaje kusimamia majukumu ya kifamilia ikiwa hana kipato (kazi/biashara). Haya maelezo ndiyo foundation ya mimi kusema wale wamama badala ya kuwahamasisha mabinti zao wafanye hata biashara ndogo ndogo wao wanawahamasisha waolewe...... I hope unakumbuka ulivyoniqoute uliandika nini.... nini kilikuwa tatizo kwa ile conment.

Bottom line, mtu akisoma hiyo comment yako ndefu hataweza kufahamu unashauri mabinti wafanye nini....
 
Mtoto wa kiume unamaliza chuo unarudi vipi hom....
How
 
Ungewaambia hao wamama kuwa kuolewa sio ajira, wawasisitize mabinti zao kufanya hata biashara ndogondogo.
Kumaliza chuo na ukaenda kukaa nyumbani bila harakati yoyote inachosha wazazi. Kwa haraka haraka hapo hao wamama wameshapima hawawezi kupata hata huo mtaji wa kuwapa wafanye biashara, moja kwa moja solution ya kuwaondoa nyumbani ni kuwaozesha. Lakin hata kuolewa haiwezekani kwa kuwa hawajichanganyi na watu wengine.
Wito wangu kwa wasomi wangu hao, wajaribu kutengeneza channel za where next wawapo vyuoni mapema sana. Hali ya ajira nchini kwa wanaomaliza vyuo ni ngumu sana. Waache kudharau kazi na kutaka kazi kwa kutaka kazi zenye hadhi ya elimu yao. Wajichanganye na watu wengine kujua mitaa inaishije kwani huko watapata fursa zinazoweza kuwaboost kimaisha.
 
Toka magetoni [emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…