Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 8,323
- 18,051
Umeongea ukweli mzito. Mtoto wa kike akimaliza chuo kinachomtesa home ni kukosa ule uhuru kama wa chuo wa kutoka out kwenda viwanja na groupies za marafiki zake wa kike, kudate na wanaume tofauti, kuletewa offer mara kwa mara, kulala kwa wanaume weekend na kuwa huru kurudi muda anaotaka hostel au sehemu alipopanga.Kuna siku tulikuwa na mjadala kati ya Ke na Me wakihitimu chuo ni yupi msoto wake unakuwa wa kutisha
1. Wa kike anashinda ndani kutizama Tv, ila anasimakia shuguli za jikon ambapo chakula kula uhakika
2. Wa kiume huwa tunajifungia chumbani, na watu wakikuchoka watapika watakula bila kukustua ili baadae waseme tulijua ulitoka.
Ila msoto wa baada ya chuo heshima kwake, ukiwaza na kidgree chako cha kukariri notes za community development na huku jamii ilokujaza bichwa ukiwa chuoni kwamba ww ni msomi, ndo unaanza kujitusi,
Ndio maana mabinti wengi wakitoka chuo anachotamani ni apate madanga wampangie chumba au nyumba halafu awe huru hata miaka 5 awe anafanya hata biashara isiyo na faida town ili tu aonekane anaenda town kazini akijiskia asitoke alale tu ndani mradi kupoteza muda kuwa huru. Halafu umri ukienda atokee fala m'moja ampigie goti amuoe aendelee na maisha kawaida.
Balaa kwa mtoto wa kiume, akiwa hajapata ajira na ameshamaliza chuo kitaa watamvumilia mwaka m'moja then baada ya hapo ni mwendo wa kunyanyaswa na kunyanyapaliwa kama vile mtu mweusi kwenye jamii ya wazungu karne ya 18.
Hakuna mtu anakutetea, ukiomba hata buku ya vocha lisala utakayopewa hadi utajiuliza huyu mtu nilishawahi kuwa na hela nikamnyima msaada nini? [emoji23]
Ndugu wanakutenga kauli zao zinakuwa tata wakiongea na wewe mradi tu wakuonyeshe kuwa wewe ni outcast na misfit kwa sasa. Yaani unakuwa unaishi kwa huzuni na msongo mkubwa wa mawazo aisee.
Sasa subiri utoboe ghafla hapo hautaamini wale wale ndugu wanavyogeuka na kuwa upande wako wanajua sasa kuna kitu watapata kutoka kwako. Kimsingi jamii ya sasa inamkandamiza sana mtoto wa kiume kwa makusudi bila huruma na haijali afya yake ya akili wala ustawi wake ila wanataka mgao wa mafanikio yake ikitokea kafanikiwa.
Boychild, jikaze popote ulipo, ukitoboa kula na wale waliokushika mkono tu, hata kama sio ndugu zako wa damu. Kama ndugu zako wa damu walikuletea umafia na wewe waletee umafia somo liwafikie. Hakikisha wanajua kuwa walikukosea. Familia yako ulipozaliwa inatakiwa ikutetee nyakati za shida na unapojitafuta wakupe bega la kuegemea hata uanguke mara ngapi, sapoti ya shida ndogo ndogo kama vocha, pesa ya kula mavazi haitakiwi kuleta maneno kama familia yako wanajimudu wao wanatakiwa kukulinda huku wakikuhamasisha na kukuencourage kujipanga upya na maisha.