Sasa kama unajua maisha ni ya kustruggle why unasumbua kichwa chako kuamini mwanaume unayetakiwa kuolewa nae anatakiwa kuwa na mafanikio ambayo baba yako miaka yote amekulea hadi sasa ana miaka 60 hajawahi kuyafikia? [emoji848]
Wanaume wapo tayari kubeba majuku ila sio majukumu yankushtukizwa, kupangiwa, kupelekeshwa, kuforce, na kadhalika. Majority wanaume wanashindwa kuishi na wanawake sababu wanawake wanaokutana nao wana mambo mengi sana na wapo speed na tamaa za maisha. Hawana utulivu wa akili na upole wa nafsi ili mwanaume aweze tulia kufanya yake.
Unakuta mwanaume anataka kufocus afanye biashara fulani halafu ikue ili afungue nyingine kwa faida ile ya kwanza wewe mwanamke kazi yako ni kuharibu huo mpango na kuharibu focus yake. Ukiona tu mnabadilisha chakula ushabeba ujauzito bila hata kumshirikisha, ukiuliza unasema kwan yeye hajui kuwa tunafanya mapenzi tupate watoto, wewe hujui siku zako uzicontrol ili mkubaliane lini mtapata watoto?
Mara ulete shida zako binafsi kwenye biashara mara umpe shida za familia yako wakati yeye binafsi unakuta amewalia buyu hata familia yake.
Kwann upiganie kuolewa? [emoji848] Ndoa au kuolewa sio kitu cha kupigania, ukiona unapigania then jua haupo tayari kama mwanamke. Ndoa huwa inakuja yenyewe na mwanaume atakufuata na kukushika mkono akitaka umfuate. Wanaume huwa na ufahari sana akimpata mwanamke aliyemvutia na akamkubali kwa wakati sio kuleta usumbufu na mapozi as if kuna mwanaume anapenda kuchezewa akili na mwanamke m'moja na wakati kuna wanawake zaidi ya milioni.
Nikuulize na wewe usipoolewa ni guarantee ya kupata kila unachokosa ukiwa umeolewa? [emoji848] Ukiishi maisha kwa formula ya kutaka kila unachotaka then utajikuta unafocus kufuta 20% ya hasara huku ukiacha kukinga mikono kupokea 80% ya faida. Take a second think about that.
Unaolewaje halafu uwe single mother, hivi umeelewa hata ulichosema. Ni sawa na useme mtu ambaye hakuwahi kusoma darasani akalia chuo kumtengenezea cheti feki useme ni msomi, alisomea nini na hakukaa darasani? Sasa mtu single mother aliolewaje, au haujui matumizi ya neno Single kwenye mahusiano?
Tufanye kuolewa ni Bahati. Bahati ni matokeo ya maandalizi yanapokutana na fursa. Wewe kama mtoto wa kike na hizi mentality za kuona ndoa ni bora liende umejiandaa fursa ikikutokea mwenzi huu au ndio hadi uanze kublock watu huko WhatsApp, ufunge status kwa baadhi ya watu wasione post zako na mtu mpya, mara uweke yale ma WhatsApp ya hovyo sijui WhatsApp FM , GB.
So wanawake miaka ya nyuma hawakuwa na ajira kama wasasa, waliishi na kula kwa namna gani? [emoji848] Nadhani hapa unamiss the point kuwa maisha ya sasa yanawatoa wanawake kwenye uhalisia wao taratibu bila wao kujijua. Wanawake wachache sana wanaplay role yakuwa mwanamke kwenye jamii ila wengi sana wanaplay roles za kiume of which inawagharimu sana.