Mangi Moshi
Member
- Jun 21, 2011
- 22
- 11
Hivi majuzi kati nilikutana na binti mmoja club fulani hapa jijini. Tukachati hapa na pale, then tukapeana contacts za simu. Nikakaa siku kama tatu hivi, nikam-text, badala ya kujibu akaanza kunibip. Nikampigia simu, tukazungumza kidogo ikiwa ni pamoja na kuweka mihadi ya kukutana jioni ya siku hiyo. Wakati tunafikia mwisho wa mazungumzo msichana akaniambia naomba unitumie vocha ya 10,000/=. Nikamwambia sawa, kimsingi sikumtumia, akaanza kubip, akabip kama mara 3 hivi, baada ya kama saa moja hivi akatuma sms kwamba bado anaisubiria hiyo vocha. Sasa cha kujiuliza hapa ni kwamba hivi hawa wasichana wanaotanguliza njaa hata kabla ya kufahamiana vizuri ni sahihi kweli? Je hiyo si kumfukuza mpendwa mtarajiwa? Hawaoni kwamba hiyo inaonyesha hali ya ngono ya biashara tangu mwanzo ambayo kwa mtu mstaarabu haitamvutia?Nawasilisha.