Wewe siku zote nilijua ni kiazi kweli. Kama una MD kama unavyodai hapa, nadhani uliipata kwa mizengwe sana.
Nesi na vipimo vya maabara wapi na wapi; na hata wewe hapo utaanza kujidai miaka mitano ilikupa uwezo wa kujua kazi ya maabara, si ujinga huo?
Kila mtu anayo kazi yake katika fani hizo, hakuna mwenye ujuaji zaidi ya mwenzie katika fani isiyomhusu.
Ngoja nikufundishe kidogo layman wangu upate uelewa angalao kidogo wa haya masayansi na matekinolojia:
Vipimo vingi vya maabara sasa hivi viko simplified and automated. Vingi hata mgonjwa au wewe unaweza kujipima ukielekezwa kidogo tu. Nitakupa mifano:
- Blood sugar: Nunua GlucoPlus meter na glucose test strips kwenye duka la dawa. Gharama yake ni ndogo tu na utaweza kupima mwenyewe sukari yako ya mwili ili mradi tu uwe una uwezo wa kusoma na kuandika. Wagonjwa wa kisukari hu monitor blood sugar ya kila siku kwa bei isiyozidi Sh 200 kila kipimo. Hauhitaji mmaabara wala muuguzi kukupima sukari yako.
- Kipimo cha malaria cha MRDT (Malaria Rapid Diagnostic) Kit: Hichi hata wewe layman unaweza kujipima mwenyewe ukiwa nyumbani kwako. Unaweka tone moja dogo la damu na matone matatu ya assay fluid na baada ya dakika chache unapata majibu. Hauhitaji muuguzi wala mmaabara. Kipimo hiki ndicho walikuwa wakibishana kwenye hiyo video clip kati ya muuguzi na mmaabara. Wote wanaweza kukifanya na hata mgonjwa akioneshwa anaweza kukifanya.
- HIV blood test kit: Kipimo hiki unaweza na unashauriwa kukifanya mwenyewe nyumbani au guest ukiwa na mpenzi wako. Kinafanyika kama kile cha MRDT, unapata majibu yako na ya mpenzi wako baada ya dakika kumi. Kipimo kimoja hata Sh 200 hazifiki.
- HIV saliva test kit: Hiki kinatumia mate badala ya damu. Yaani kabla ya huo mchezo wa wawili kila mmoja anaweka mate kidogo kwenye kit, mnasubiri dakika 20 mnayaona majibu na kuamua mchezo utachezwa kwa namna gani. Kits hizi zinapatikana kwenye maduka ya dawa kwa bei ya chee. Tatizo wizara ya afya haijazikazania. Zilipaswa kumwagwa kwa wingi hadi machinga wazisambaze kwani ndiyo mwarobaini wa kudhibiti janga hili la UKIMWI. Kondomu wengi hawazitumii kwa sababu mbali mbali zikiwamo zenye mashiko na zisizo na mashiko.
- Kipimo cha mkojo: Hiki nacho ni rahisi sana na unaweza kujipima mwenyewe. Kinapatikana kwenye maduka ya dawa kwa bei chee. Kinatumia urinary strips. Unachukua mkojo wa katikati (mid urinary stream), unachovya hiyo strip kwenye mkojo huo. Itakupa majibu kama una UTI, kisukari, protein, albumin, bilirubin, red blood cells na kadhalika.
Cha muhimu sana ni kwamba tumia mkojo wa katikati. Ule wa mwanzo na wa mwisho huwa ni mchafu kwa kawaida. Hasa kwa wanawake, mkojo wa kwanza kwenye stream huweza kuchanganyika na uchafu wa ukeni ikiwamo seminal fluid, blood cells kwa walio kwenye hedhi na kadhalika. Tatizo la wanamaabara wengi huwa hawawaelekezi wagonjwa mkojo wa kuchukuliwa ie mid stream urine. Hiki ndicho chanzo cha wagonjwa wengi kuonekana wana tatizo la UTI wakati hawana bali walipima mkojo wa kwanza au mwisho ya stream.
- Pregnancy test strips: Kujua kama umeshanasa mimba ni rahisi tu. Unanunua pregnancy test strip moja kwa bei ya jero. Unachovya strip hiyo kwenye mkojo wako wa asubuhi. Yaani hata mimba ya wiki moja kipimo hiki itakiona. Huhitaji usubiri hadi ukose hedhi ya mwezi ujao au hadi uanze kutapika tapika ovyo. Yaani ndani ya siku 3 hadi 7 tu utajua kama mimba imeingia na hivyo utajua ni ya mwanaume yupi aliyesababisha hilo. Hauhangaiki kwenda maabara au kwa daktari.
- Kipimo cha pressure ya damu: Unahitaji kununua tu digital blood pressure machine. Unajifunga mwenyewe, unabonyeza kitufe na baada ya muda mfupi unapata unapata pressure yako na pulse rate yako.
- Huko kwenye maabara vipimo karibu vyote hufanywa na automated machines. Kazi ya mmaabara ni kutumbikiza tu hizo samples kwenye machines. Yaani ni kama kutumbukiza nguo kwenye mashine ya kufua nguo na kuwasha. Ujuzi wake aliosoma chuoni hautumiki kwani muuguzi au hata layman wa medicine yo yote anaweza kutumbukiza hizo samples na kuwasha mashine. Yaani kwa sasa laboratory technicians hawahitajiki sana kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Ujuzi wao unahitajika kwenye viwanda vya kutengeneza vitendanishi, kwenye taasisi za utafiti, vyuo vya kufudisha taaluma. Ni kama ilivyo kwa sasa kwa wafamasia. Ujuzi wao ni wa kutengeneza dawa na utafiti wa dawa. Hapo zamani kazi yao hospitalini ilikuwa ni kutengeneza au ku compound dawa mbali mbali. Sasa hivi dawa zote zinakuja hospit ziko fully compounded toka viwandani. Hivyo kazi ya pharmacist hospitalini imebaki ku dispense tu dawa kwa wagonjwa na kutunza store ya dawa, kazi ambayo haihitaji kisomo cha miaka 4 chuo kikuu au zaidi kwa wale walio na master degrees or PhD in pharmacy ambao kwa sasa tunao wengi tu wakidispense dawa mbili mara mbili wakiwa na PhD in pharmacy!
Kwa kifupi tunawa under utilize sana hawa watalaamu wetu wa maabara na wana famasia. Ndiyo maana huyo mmaabara wa kwenye hiyo video clip kwanza hakuwa amevaa laboratory coat yake na hakuwa kwenye chumba chake cha maabara. Alikuwa kamfuata huyo muuguzi mrembo kwenye kituo chake cha kazi kupiga soga. Muuguzi alikuwa bize na kazi yake huku hilo linjemba la maabara likimsumbua kwa soga zake zisizo na mashiko.