Mabishano kati ya medical professionals yanayolenga interests za mgonjwa ni jambo la kawaida na ni ethical

Nikisema wewe ni kiazi, sitanii. Ninakwambia ukweli mtupu, wewe ni kiazi.
Na kama huna kumbukumbu, nilishakwambia hivyo mara kadhaa humu humu JF kwamba hiyo MD yako ni ya magumashi.
Huna chochote ulichonifundisha hapo, na wala huna uwezo wa kunifundisha kitu.
Yote uliyoandika hapa ni upuuzi, kama huelewi kwamba huyo nesi anakazania kutumia kipimo kilichokwisha muda wake, hata kama ni automated, na wewe bado hujui maana yake ni nini?
Hizo "automated machines" zinazofanya vipimo hazihitaji ujuzi kuziendesha?

Hata hiyo 'interpretation' ya majibu yenyewe, nesi hajui maana yake ni nini.

Kuonyesha ulivyo mweupe kichwani, hata hujui kazi sahihi zinazofanywa na wataalam kama wafamasia, wewe unaona tu kutoa dawa, basi, hujui kwamba wanajua hiyo dawa wanayotoa zaidi ya hata huyo anayeiandika! Hili hulijui.
Kwa hiyo kwa vile mazingira ya kazi zao hayawapi fursa ya kutumia ujuzi wao kikamilifu, wewe unadhani hivyo ndivyo inavyopaswa iwe.

Ndiyo, teknologia sasa hivi itaruhusu 'self-diagnosis' and treatment' kwa magonjwa mengi, lakini hilo halitakuwa na maana kwamba watu kama wewe hamtakuwepo huko makazini, pamoja na kwamba mtakuwa 'redundant.'
 
Sasa hapo tusi ni lipi masta.. ukienda jeshini si naacha kabisa narud na nyumban.. hahaha
Hapo ulipo unaweza kujua kama nimeenda jeshini au laa? Unafahamu ethics za kiutumishi lakini? Mpaka Mhe Waziri mkuu juzi kawaagiza wakurugenzi kuhakikisha kwamba watumishi kama huyo nesi hawaachwi kuichafua sekta ya afya.
 
Hapo ulipo unaweza kujua kama nimeenda jeshini au laa? Unafahamu ethics za kiutumishi lakini? Mpaka Mhe Waziri mkuu juzi kawaagiza wakurugenzi kuhakikisha kwamba watumishi kama huyo nesi hawaachwi kuichafua sekta ya afya.
Tulia unywe maji ndugu yangu mtumishi
 
Juzi Manesi wamemchoma mtoto wangu sindano zaidi ya 15 et wanatafuta mshipa

Wakataka wamnyoe wamchome ya kichwa, mama ake akakataa wakaanza kumtukana eti anawafundisha kazi.

Akabeba mtoto kwenda private

Manesi wa serikali wa halmashauri na hospital ndogo ndogo sio wa kuwaamini kabisa, post za kupangwa tuu zinabeba na makokoro mengi
 
Najua unafurahia kimoyo moyo hiyo elimu ya bure niliyokupatia. Najua sasa utakapokuwa unahisi umedungwa mimba utakuwa unanunua hiyo pregnancy test strip ya jero na kuichovya kwenye mkojo wako wa asubuhi. Hutahitaji kusubiri hadi ukose hedhi yako ya mwezi ujao au hadi uanze kutapika tapika ovyo. Ndani ya siku 3 hadi 7 baada ya huo mchezo utakuwa unajua kama umenasa! Hapa Jf elimu inatolewa bure.
 
Nasubiri tu kukutoa kazini, kwa sababu wewe kama 'General Practitioner' hutakuwa na kazi tena. Utakuwa 'redundant' na hicho ki-'MD' chako, unachojigamba nacho hapa. Heri ya kumwona 'clinical Officer' kuliko kukutana na boya kama wewe.
Bure kabisa.
 
Nasubiri tu kukutoa kazini, kwa sababu wewe kama 'General Practitioner' hutakuwa na kazi tena. Utakuwa 'redundant' na hicho ki-'MD' chako, unachojigamba nacho hapa. Heri ya kumwona 'clinical Officer' kuliko kukutana na boya kama wewe.
Bure kabisa.
Hujui unaongea na nani. Ndiyo uzuri wa Jf. Kama una akili be careful unapotumia mitandao hii. Unaweza kuwa unambeza boss wako au baba yako au aliye juu zaidi ya hao etc etc. Be very careful my child. You might end up into trouble. Halafu siyo mila na utamaduni wetu. Uhuni siyo deal hata kidogo.
 
Wewe ni bwege mmoja tu, kutokana na hadhi ya michango yako humu JF.

Kwa hiyo usijifanye unahadhi zaidiya thamani ya unayochangia hapa.

Ungekuwa unazo akili za kutosha ungetambua unajibishana na mtu wa namna gani hapa; lakini kwa vile huna fikra nzuri unajiandikia tu na kuropoka hovyo hovyo, kama ulivyofanya hapa.
 
Umeloloma ya maana, lakini hukuainisha unamueleza nani!
 
Yale sio mabishano, ni matukanano!

Ati "pita hivi, mwanaume gani wewe, unajifanya unajua taaluma kuliko wengine"?

Very indisciplined!! AFUTWE KAZI akatafute biashara ya saizi yake ya kusutana!
Hilo mtoa mada hakuliona, yeye kayaita ni mabishano ya kitaaluma!

Ile "nyo nyo nyo" na kebehi zingine kwake ni mabishano na haelewi kuwa hizo ni kauli zenye kuudhi mahala pa kazi.

Nilichobaki mpaka leo najiuliza, kiwango hicho cha matusi ya mazoea, kutukanwa na staff mwenzako namna hiyo ambaye hamjawahi kukorofishana kabla ama kimahusiano, linawezekanaje jambo hilo?

Hakuna njama na fitina za kimahusiano kweli hapo?

Hilo tusi najaribu kulipachika kwa walengwa mbali mbali, mfano: mtu yeyote asiyehusiana naye kimapenzi, junior wake kikazi, senior wake kikazi, linakataa.

Hawa wawili walikuwa na personal conflict, maana si kwa dharau hizo, ndiyo maana imepelekea wakawekeana mitego ya makamera.

Niliona maelezo ya boss wao pale akijieleza kutetea hoja ya kutumia vipimo hivyo expired.

Kumbe sasa suala la matumizi ya vipimo hivyo expired lilikuwa na baraka na wote hao walilijua, ila mmaabara akatega kinasa sauti na kujifanya haelewi ili kumnasisha hasidi wake.

Kafanikiwa lakini kwa mtindo wa upigaji mabomu ya sumu, kweli litaangamiza mlengwa, lakini pia na yeye mfyatuaji hubaki na athari za sumu zitakazomuua pole pole.
 
Ivi mkuu umesikiliza kwa makini hizo video za watukanaji, ukaja ukasikiliza video ya Ummi na mganga mkuu wa hospitali ya watukanaji, ukasikiliza video ya Waziri mkuu kuhusu sakata hilo pamoja na andishi la huyu anayejiita Dr humu unayebishana naye?

Weka conclusion yako kama umeangalia video zote hizo nilizozitaja.
 
Wachache tu watakuelewa ..na kama ukifuatilia yale mabishano sioni kama nesi anakosa
 
Inawezekana hivyo vifaa vya kupima vikatumika na watu ndio ila nadhani bado hatujafika huko kama wenzetu ambapo tayari wameshafika..wao wamewekeza sana kwenye elimu yao na hata akipewa hiko kifaa anaenda kusoma manual yake vizuri anajipima.lakini kwetu tuseme ukweli kufuata maelekezo ya mdomo ni rahisi zaidi kuliko kufuata manual especially kwa mtu ambaye hafahamu vizuri kuhusu kipimo husika.Anayekuuzia kifaa amesomea famasia na akikupa maelekezo hataki kukupa maelekezo ya kutosha either kwa sababu hajui sana kwa kuwa sio profession yake na pia ili isionekane kujipima ni ngumu sana bali atakupa maelekezo ya juujuu ili uone ni rahisi na ili pia asikuchanganye usije ukahairisha kununua biashara zenyewe ngumu wenyeww mnajua😂😂 .manual nyingi zinakuwa zimeandikwa kiingereza na kuna maelekezo yanakua ya nyongeza mfano namna ya uwekaji wa hayo matone ya maji kwenye kipimo cha malaria au cha ukimwi namna ya kuinua kichupa cha matone na kudondoshea matone.

-Utunzaji mbovu wa kifaa cha kupimia unaweza ukaathiri majibu ya kipimo husika so mazingira ya nyumbani sio salama sana kutunza vifaa hivyo..

-Kuna kitu kinaitwa quality control..hii bi lazima uhakikishe kifaa kinatoa jibu sahihi kabla ya kuanza kupima wagonjwa na kutoa majibu..mazingira ya nyumbani unapata wapi control positive ya ukimwi na negative kujihakikishia kifaa chako kinatoa majibu sahihi???haiwezekani..
-Hata kipimo cha kupima sukari kuna maelekezo ambayo usipofuata majibu yake hayatoki sawa..Na chenyewe pia kina solution yake ambayo unapaswa kuitumia kama control ili kujua kama majibu yake yanatoka sawa na strips zake zinafanya kazi sawa.

-Kipimo cha HIV oralquick..cha kutumia mate kinapima maambukizi ambayo tayari mtu ameshaumwa kwa muda kidogo sio cha kujua maambukizi ndani ya muda mfupi baada ya kuyapata so sio kizuri kutumia kujipimia ukiwa unaenda kufanya dhambi huko duniani..utarudi hapa unalia..Blood tests nikiwa na maana. ya vipimo vya damu ndivyo vyenye uhakika zaidi ukilinganisha na kipimo cha mate.sio mimi..hizo ni tafiti huko duniani wanapotengezeza hivyo vifaa vyote ambavyo sisi ndio tunavitumia.

Hata kujipima presha unayosema wewe kuna maelekezo yake ambayo mtu asipofuata vilevile majibu yake hayaji sahihi kama yanavyotakiwa. so uwepo wa machine sio kisingizo cha kujipima nyumbani.

Vifaa vya lab kuwa automated sio kisingizio cha kufanya kazi ikaonekana rahisi kuliko ilivyo. Hata sampuli zikifika maabara zinakaguliwa kama zinaubora na zinapitishwa hatua zingine kabla ya kupimwa ndipo zipimwe. Sio rahisi kama unavyochukulia.
Hao unaosema layman wangepelekwa huko maabara wakapime na wakasaidie kupunguza tatizo la ajira kama ingekuwa kazi yao ni rahisi kama unavyodhani.
 
Reactions: Cyb
Wachache tu watakuelewa ..na kama ukifuatilia yale mabishano sioni kama nesi anakosa
Kosa kitaaluma lipo, ingawa hili anaweza kujivua na pia kapata utetezi kwa mganga mkuu kwamba walikubaliana kwenye briefing kuwa zitumike hizo zilizofikia expiry date ili "kuziokoa" ili usije kufika muda halisi unaokubalika kuteketezwa kabla hazijatumika.

Kosa halisi linalomkaba koo ni yale matusi yake ya nguoni kwa huyo staff mwenzake.

Huyu binti nilidhani "Musoma line" ama "nshomire", nikaja kusikia jina la kichaga!
Ama ni mambo ya "vyeti"!
 
Dah!

Sijasikiliza 'video' yoyote mkuu 'Sakawaka Mao', na wala sina haja ya kusikiliza video yoyote kuelewa majukumu ya kila fani kati ya watu hao wawili, nesi na mMaabara, kama ilivyowasilishwa kwenye mada.

Kuna kanuni za kiutendaji zisizohitaji siasa wala kuonyeshana ubabe kati ya watendaji wa maeneo husika. Hizo kanuni zinapokiukwa, haijalishi nani anaongea nini na anacho cheo gani.

Huo ndio msingi wa hoja zangu hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…