Sasa kama ukumbi hautoshi,mnataka watu waruhusiwe kuingia ili wakakae wapi?
Public hearing hii inafanyika kwa siku 3 mfululizo,sio lazima kila mtu aingia leo...waweke utaratibu wa wale waliojiandikisha kutoa maoni yao juu ya muswada ndio waingie ndani kwa zamu kulingana na uwezo wa ukumbi kubeba watu. Wakimaliza watoke na kuwapisha wengine wenye maoni yao. Wengi wa waliojazana pale ni mashabiki na washangiliaji-wale hawana haja ya kuwemo ndani,wanaweza kufuatilia proceedings hizo kwa kutumia PA system nje ya ukumbi na kwenye vyombo vya habari-radio ONE wanarusha live.
Kwa wale walioamua kuendesha public hearing yao nje,ni counter-productive kwasababu maoni yao hayatafika yanapotakiwa kufikishwa...sana sana wanapoteza muda wao.
By the way,mjadala wa leo ni kuhusu Muswada wa kuanzisha tume ya Katiba, na sio kujadili Katiba yenyewe...hivyo inputs/ideas/critique inatakiwa ku focus kwenye vifungu vilivyo ndani ya Muswada wenyewe.
Baada ya kusema haya mimi nina wazo moja japo kwa mchakato unaoendelea sasa linaweza kuwa limepitwa na wakati. Kwa nini zisiwepo mechanism nyinginezo za kukusanya maoni juu ya muswada husika kama vile wananchi kuruhusiwa kutoa maoni yao kwa njia ya barua, e-mail,social network platforms etc
Kwa kuruhusu hizo njia nyingine,hata watu wasioweza kufika Dar,Dodoma au Zanzibar physically wataweza kutumia haki yao ya kutoa maoni pasipo kulazimika kuwepo kwenye maeneo yanapofanyika shughuli hiyo