Sio kweli Muhosin, Ukumbi hautoshi wangekaa wapi? na bunge ni sehemu ya kuheshimiwa wao wana mabango wanawaza vurugu tu, katika hili natetea kwasababu nashuhudia, ukumbi ni mdogo, kosa labda ni kuchagua ukumbi that all.
Remmy nakubaliana na wewe kwamba ukumbi ni mdogo. Mimi niliposikia kwamba itafanyika Msekwa nilishangaa kama walipanga wanajua nguvu ya umma inayoshiriki katika huu mswada. Pale Mkuruma serikali iliambiwa kwamba public hearing ya mara moja na inayofanyika dodoma siyo haki, kama kawaida yao wakapuuzia.
Tatizo langu Remmy ni nia na uwezo wa serikali. Hakuna jambo moja ambalo mimi nalifahamu ambalo serikali ilipanga vizuri bila kudhulumu haki za raia, kudharau mawazo ya wananchi, na kuwakandamiza kwa kutumia mabavu. Serikali haikutakiwa kuendesha mchakato huu kwa ad-hoc planning. ilitakiwa kusikiliza wadau wanasema nini na itekeleze
Serikali haikutakiwa kuwanyanyasa wananchi waliofika dodoma kwa namna yoyote ile. Haikuwalipia gharama yoyote! Siyo kosa la mwananchi aliyetoka Tanga kwamba ukumbi hautoshi wakati ameshajiandaa point zake anazotaka kuzisema na ametumia gharama.
Baada ya serikali kuchemsha kuhusu kushindwa kuwapatia wananchi fursa ya kuingia ukumbini, ilitakiwa iwabembeleze na kuwatuliza kwa busara siyo mabavu na mabomu na kauli za amri. Serikali ilitakiwa kwa haraka sana ikodi ukumbi mwingine na kuwapeleka hao wanaharakati na kuandaa utaratibu wa kuwasikiliza. Kwa bahati mbaya serikali inafikiri kutumia polisi kila inaposhindwa kuhudumia wananchi
Remmy naomba pia ufute fikra kwamba walio nje ya ukumbi wa bunge ni wanafunzi wanaofanya fujo na vurugu. Pattern yako ya kufikiri hasa ndivyo ya serikali na ccm, kwamba yeyote anayejieleza kinyume na utawala unavyotaka anafanya fujo. Nje ya viwanja vya bunge pia kuna watu wazima na heshima zao, wengine ni wakurugenzi wa mashirika yasiyo ya kiserikali na wengine ni viongozi wa dini. Wote wamezuiliwa kuingia na wamechanganyikana na wanafunzi kwa sababu ni swala la haki siyo "heshima na amani"
Kama serikali haikutaka wananchi wafanye fujo, kwa nini hawakutekeleza maoni mazuri kabisa yaliyotolewa Nkuruma na ambayo yameendelea kutolewa kupitia vyombo vya habari hadi leo? Serikali ingekuwa sikivu na inayojali amani, baada ya mjadala wa Nkuruma tu ilitakiwa irejeshe huo mswada kuandikwa upya badala ya kuendelea kukejeli na kudhihaki wananchi eti inakusanya maoni ya mswada mfu!
Mwisho naomba nitofautiane na wewe kwamba bungeni ni mahali pa kuheshimiwa kwamba mabango eti yanavunja hiyo heshima. Hizi ni fikra za kale sana, nasikitika kusema hivyo. Bungeni ni mahali pa uhuru wa kujieleza usiotakiwa kuzuiliwa kwa namna yoyote ile. Kubeba mabango kunavunja vipi amani? Hata kufanya maandamano ndani ya viwanja vya bunge kunavunga vipi amani?