Mabondia wawili wa Tanzania Yusuf Changarawe na Kassim Mbundwike wameingia robo fainali za mchezo ya Jumuiya ya Madola

Mabondia wawili wa Tanzania Yusuf Changarawe na Kassim Mbundwike wameingia robo fainali za mchezo ya Jumuiya ya Madola

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mabondia wawili wa Tanzania Yusuf Changarawe na Kassim Mbundwike wameingia robo fainali za mchezo ya Jumuiya ya Madola inayoanza rasmi leo jijini Birmingham, Uingereza.

Bondia wa tatu wa Tanzania, Alex Isinde sio tu ataanzia mzunguko wa kwanza bali pia atakuwa ndiye Mtanzania wa kwanza kutupa kete kwenye mashindano haya ya 48 ya nchi zilizopata kutawaliwa na Uingereza kesho Julai 29, 2022.

Isinde atapambana na bondia kutoka Antigua & Barbuda aitwaye Alston Ryan.

Endapo Isinde atashinda ataungana na wenzie katika robo fainali ambapo mshindi anabeba medali ya shaba.

Endapo wakishinda robo fainali wataingia nusu fainali ambako watawania kunyakua angalau medali za fedha.

Michezo ya Jumuiya ya Madola 2022 inazinduliwa rasmi leo saa mbili usiku kwa saa za huku (Tanzania iko mbele kwa saa mbili).

Tanzania itatupa tena kete zingine siku ya Jumamosi Julai 30, 2022 wakati wanariadha wanne wa mbio ndefu (Marathon) wanawake na wanaume wataingia kuchuana.

Wanariadha hao wa marathon ni Alphonce Simbu, Hamisi Misai, Jakline Sakilu na Failuna Matanga.

Kwenye michezo hiyo Tanzania inawakilishwa na wanariadha tisa, mabondia watatu, wacheza judo wawili, waogeleaji wawili na mnyanyua vitu vizito kwa walemavu (Para-Powerlifting) mmoja.
 
Huyo Changarawe jina si geni! Hivi si ndiye baba yake alikuwa mwanajeshi kocha wa masumbwi (Mzee Changarawe) kule Mwanza?

Kama ni kweli, naendelea kuamini, kutoboa TZ ni connection
 
Huyo Changarawe jina si geni! Hivi si ndiye baba yake alikuwa mwanajeshi kocha wa masumbwi (Mzee Changarawe) kule Mwanza?

Kama ni kweli, naendelea kuamini, kutoboa TZ ni connection
Changarawe ni Mwananjeshi huyuu
Wa Kiabakari
 
Naona Tz tumepata silver Kwenye marathon kutoka kwa Felix Simbu.
 
Back
Top Bottom