Crimea
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 25,874
- 36,030
Lisu hana kura za kushindaNi kweli, ndio maana ameshinda lakini hawakutaka kumpa nchi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lisu hana kura za kushindaNi kweli, ndio maana ameshinda lakini hawakutaka kumpa nchi.
Lisu hana kura za kushinda
Ndio ukweli huo na sio tamaaKwa mujibu wa matamanio yako.
Mihemko ya kisiasa inakuzidi tu! TISS haipo kisiasa bali kwa usalama wa taifa. Ingaliona kuwa Magufuli hafai asingeshinda.Sio kazi ya Tiss kuiwezesha ccm kushinda, labda useme Tiss ni idara ndani ya ccm. Sasa kama Tiss ndio wanapanga mipango ya ushindi wa ccm, hiyo ccm itakuwa ni chama cha siasa tena, si itakuwa ni kikundi cha dola kulichojivika koti la chama cha siasa?
Siyo kwamba Tundu Lissu alikuwa haungwi mkono, Bali kwa mfumo tulio nao, Jiwe alilazimisha kila aina ya chombo cha dola, kimpe "support" yeye pekee!Najiuliza kama hadi TISS waakikuwa hawamuungi mkono Lisu alitegemea atashinda vipi sasa?
Yani huungwi mkono na chombo cha usalama hata kimoja utashindaje sasa?
Lisu akikuwa debe tupu. Hajui siasa
Mihemko ya kisiasa inakuzidi tu! TISS haipo kisiasa bali kwa usalama wa taifa. Ingaliona kuwa Magufuli hafai asingeshinda.
Hivi kweli na akili yako, mtu kama Tundu Lissu ana Afya ya akili ya kuongoza taifa? Pengine afadhali mbowe kuliko Tundu Lissu.
Kiusalama unawezaje kumkabidhi nchi mwenye green card kama Nyarandu au uraia wa nchi nyingine.
MmNimejaribu kuichunguza karatasi ya kupigia kura ya Urais wa JMT katika uchaguzi huu uliopita, na nina machache ya kuchangia.
Nianze kwanza kwa kusema karatasi ya kupigia kura inabidi kuichukulia kama ni nyaraka muhimu sana. Uzito wa kipekee unahitajika katika kuibuni, kuichapisha, kuisambaza na kuihifadhi. Kwa nilichokiona katika uchaguzi huu wa 2020, sidhani kama lolote kati ya hayo yalizingatiwa. Najua nayasema haya katika nyakati na mazingira ambayo inaonyesha kama wenye mamlaka wameamua waitupe mkono mfumo wa demokrasia na siasa safi, lakini matumaini bado yapo kuwa siku yaja ambayo tutarudi nyuma na kujirekebisha.
Ngoja sasa niorodheshe baadhi ya vitu nilivyoona katika karatasi hii:
View attachment 1631358
- Picha ya mgombea wa Urais inatakiwa ndiyo ianze kushoto na ya mgombea mwenza ifuate, kinyume na walivyofanya.
- Pia nitazungumzia 'inconsistencies' katika karatasi hii. Hapa namaanaisha jambo moja kufanyika kwa mgombea mmoja lakini halikufanyika kwa mgombea mwingine. Nitatoa mifano michache:
- Mgombea mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan ametajwa kwanza kwa jina la kwanza. Ukiangalia Mgombea mwenza wa CHADEMA, ametajwa kwanza kwa jina lake la Mwisho. Sijajua kwa wagombea wengine kwa sababu siwafahamu vizuri.
- Mgombea wa CCM, John Magufuli ametajwa kwanza kama Dkt. wakati mgombea wa CUF, title yake ya Prof. haikuwekwa.
- Kwenye majina ya vyama, font size hazifanani na zingine kama ziko bold wakati zingine haziko bold, mfano za ACT, CHADEMA, CHAUMMA, etc. ni ndogo zaidi ya nyingine.
- Hakuna haja wala umuhimu wa kurudia title ya 'CHAMA', 'MGOMBEA UMAKAMU WA RAIS', 'MGOMBEA URAIS' wala 'ALAMA' kwa kila mgombea. Hizi titles zingewekwa tu juu pale zikiwa bold na maandishi makubwa zinatosha.
- Kuna hili suala lingine ambalo limeongelewa sawa la utaratibu gani ulitumika katika kuamua orodha hii ya wagombea iwekwe vipi. Ninavyokumbuka, NEC walisema ilitokana na jinsi wagombea walivyorudisha fomu zao. Hili sitaliongelea kwa sababu wote tunajua hizo zilikuwa ni geresha tu. Itoshe kusema huo siyo utaratibu wala majibu ya kisomi kwa watu walioelimika. Nadhani utaratibu sahihi ni kufuata alphabetical order ya majina ya chama au majina ya mwisho ya wagombea. Na hili liwekwe wazi katika kanuni za uchaguzi ili kuepuka 'surprises'.
- Mfano wa karatasi hii utolewe mapema zaidi, ili mapungufu yaweze kurekebishwa na maboresho kufanywa. Kama nilivyosema hapo awali, muundo wa karatasi hii utajwe wazi katika sheria kuu za uchaguzi na kusiwe na room ya kirahisi rahisi ya kuzibadilisha kama inavyofanyika sasa.
- Jukumu la kuelimisha njia sahihi za kuitumia karatasi hii libebwe na NEC wenyewe. Kuna wagombea walitoa matamko ambayo kisheria walitakiwa waadhibiwe. Kuna mmoja alinukuliwa akisema 'wewe angalia mtu wa kwanza tu hapo juu, weka tiki, wengine huko chini siyo wagombea halali'
- Karatasi ya kupigia kura iorodheshwe kama ni nyaraka muhimu sana katika nchi, Sheria itungwe ambayo itasema kuwa atakayekutwa na karatasi hii zaidi ya copy moja nje ya kituo cha kupigia kura, adhabu kali ichukuliwe dhidi yake.
Nimalizie tu kwa kusema, ukiacha mapungufu haya niliyotaja hapo juu ambayo nadhani mengine yalifanywa kama maamuzi ya makusudi, sidhani kama hii ikaratasi imekuwa designed na professional designing na printing company inayojitambua. Inaonyesha ni kama karatasi ambayo imetengenezwa katika kaduka ka stationery na dada mmoja ambaye pia anauza vocha za tigo. Maandishi ya majina hayana uwiano, baadhi yako juu zaidi, mengine katikati, mengine kushoto zaidi. Halafu unaniambia kuna mabilioni yametumika hapa kwa kazi hii?
Tanzania ni urithi wetu sote, hakuna atakayeweza kulibadilisha hilo.
Uchambuzi huu[emoji848][emoji848]Nimejaribu kuichunguza karatasi ya kupigia kura ya Urais wa JMT katika uchaguzi huu uliopita, na nina machache ya kuchangia.

Chombo cha usalama huwezi kukilazimisha.Siyo kwamba Tundu Lissu alikuwa haungwi mkono, Bali kwa mfumo tulio nao, Jiwe alilazimisha kila aina ya chombo cha dola, kimpe "support" yeye pekee!
Kumbe kwako wadada ndio hufanya mambo ya ovyo ovyo siyo? Huu mfumo dume na ubaguzi wa kijinsia inabidi upigwe vita kwa nguvu zote.Inaonyesha ni kama karatasi ambayo imetengenezwa katika kaduka ka stationery na dada mmoja ambaye pia anauza vocha za tigo.
Ulichokisema ni kweli. Hii ni sawa na kuwa na karatasi ya mtihani wa taifa nje ya chumba cha mtihani lakini Bunge gani litapitisha hiyo sheria? Gwajima anaweza kuipigia kura sheria hiyo kweli ikapita? Tuombe tu vikwazo vifanye kazi. Kama vikishindwa, na watu hawataki kumwaga damu, we are stuck with CCM to the end!
Bado sijaelewa kama kuna mtu alikutwa na begi la karatasi za kupigia kura halafu bado anadunda wakati ni mbaya kulipo gaidi na jambazi.
Watu wanachoma moto kibaka na sio pesa aliyoiba cha ajabu kwa Mara ya kwanza kibaka anaachwa kuchomwa moto badala yake Mali aliyoiba ndiyo inayochomwa moto.
Hili zoezi la kupata viongozi limekwisha waliochukua madaraka wamechukua tusubiri watakapoamua kufanya uchaguzi siku zijazo.
Hii ilifanyika maksudi kabisa sio bahati mbaya
Na KIBAYA zaidi huu uchaguzi umeharibiwa na tume yenyewe Mkurugenzi wa Uchaguzi alijivika joho la uwakili wa CHAMA TAWALA na ALIANZA kutoa maelekezo ya kwa waratibu wa mikoa juu ya kuhakikisha CCM inashinda kwa USHINDI mkubwa na kwa mara ya Kwanza DSO'S ndio walikua wanauratibu huu uchaguzi uliopita na wanafanya yote hayo si kwa sababu wao Ni wazalendo wa nchi Bali wakereketwa wa CCM na wafaidika namba moja wa mfumo wenyewe! Wanajipendekeza kutetea vitumbua vyao
Kundi la pili wakurugenzi wote nchini Ni wanafiki na njia ya mnafiki Ni Moto wa jehannamu na laana za muumba ziwe juu yao! Maulana atawalipa sawa na matendo yao! Mtu km sintoo wa hai Ni mtoto wa askofu mola amrehemu babaake ALIKUA muungwana Sana yule mzee wa ITAJA huko SINGIDA na alikua mwema Sana kijana yule hana hata hofu ya mungu halafu JUMAPILI anaingia kanisani kuabudu na kusifu it's better wangekua watu wa kawaida km sisi kazi ya kutoa haki Ni majukumu ya mola muumba ila sisi wanadamu tunafanya kwa niaba na KIBAYA zaidi tunafanya kwa kuzifurahisha nafsi zetu tunasahau Kama kesho. Kuna hesabu ya matendo yetu niishie hapa
Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
Kama ulivyozema, ni jambo baya tunapotambua kuwa vyombo husika havijali hisia, matamanio na mitazamo ya wananchi kiasi cha kufikia kuvuruga waziwazi zoezi zima muhimu kama la uchaguzi.
Kwa kilichotokea, hatuwezi kusingizia eti 'hakuna nchi iliyowahi kufanya 'perfect election', kama Kabudi alivyodai jana. Kama wengi wanavyosema, lile zoezi halistahili hata kuitwa uchaguzi.