Maboresho ya bandari yanavyovutia wateja wapya

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
MAMLAKA ya Bandari Tanzania (TPA), imeendelea kufanya maboresho makubwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Maboresho hayo yamechangia kuongeza ufanisi ikiwa ni pamoja na ongezeko la meli, shehena na kuvutia wateja wapya zikiwemo nchi jirani.

Akizungumza, Mkurugenzi wa Bandari Mrisho Mrisho, amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia uboreshaii wa miundombinu bandarini hapo, ambapo sh. bilioni 70 alizotoa kuboresha mfumo wa kupakua makasha zimeleta tija.

Alieleza kutokana na maboresho yaliyofanyika kumekuwa na ongezeko la idadi ya meli katika bandari hiyo, ikilinganishwa na hali ilivyokuwa katika mwaka wa fedha 2020/2021.

"Shehena iliongezeka kwa wastani wa asilimia 13.4 kutoka tani milioni 16.190 mwaka 2020/2021 hadi tani 18.354 mwaka 2020/22" alisema huku akisema miongoni mwa nchi zilizoanza kuitumia kwa wingi bandari hiyo ni Zimbabwe.

Alibainisha shehena ya nchi jirani iliongezeka kwa asilimia 39.8 kutoka tani milioni 5.579 mwaka 2020/2021 hadi milioni 7.801 mwaka 2021/2022. Kwa upande wa shehena ya makasha, iliongezeka kutoka 713,681 mwaka 2020/2021 hadi 808,245 mwaka 2021/2022 ambayo ni ongezeko la asilimia 13.3.

Alisema shehena ya magari katika bandari hiyo iliongezeka kutoka magari 147,566 mwaka 2020/2021 hadi magari 203932 mwaka 2021/2022 ambayo ni asilimia 38.2. Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa PMCL, Amina Aziz, alisema lengo la ziara hiyo ni kujionea utendaji katika bandari hiyo kusaidia kufikisha mafanikio hayo kwa wananchi.
 
Mbona Bado tuko mule mule? Tukuze uchumi Wetu wa ndani Ili Bandari xifikie walau shehema zaidi ya mil.30.
 
tujitahidi kuongeza uzarishaji kwa kuifanya idadi kubwa ya watu wetu kuwa productive.
Hakuna tunachofanya kama tunahangaika na mastructure haya huku watu wetu kwa kiasi kikubwa ni non-productive.
 
Back
Top Bottom