Napenda kuweka wazi juu ya huu mpango wa maboresho ya Elimu, huu mradi ulianza enzi ya utawala wa Mkapa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia (World Bank) mradi huu ni matokeo ya mpango wa serikali kusamehewa madeni chini ya HIPC na unaenda hatua kwa hatua kulingana na mahitaji ya wakati na ufanisi wa utekelezaji wa mradi.
Mradi huu ulianza na MEMKWA, uliolenga kuboresha elimu ya msingi. Kazi kubwa ilifanyika ikiwemo kutoa mafunzo kwa walimu na kuongeza udahili kwa watoto wa darasa la kwanza
Badae wakati wa utawala wa Kikwete ulikuja mradi wa MESS huu ulilenga kuboresha elimu ya sekondari ndio mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari kila kata ulianzishwa na kuongeza udahili wa watoto wa sekondari, pia idadi kubwa ya walimu waliajiriwa na vitabu kusambazwa mashuleni
Hii phase ya tatu ilihusu uboreshaji wa elimu ya juu ikiwemo vyuo vya ufundi, mradi ulilenga kuwezesha angalau kila wilaya inakuwa na chuo cha ufundi kwa maana ya VETA, pia mradi umelenga kuboresha elimu ya vyuo vikuu na vyuo vishiriki kwa kuboresha mitaala na kuongeza mafunzo kwa wahadhiri na watumishi wa kada mbalimbali, kuongeza usimamizi wa shughuli za elimu ikiwemo utoaji wa nyenzo za kazi kwa maofisa ukaguzi wa elimu katika kada mbalimbali
Mradi huu ulikuwa ufadhiliwe na bank ya dunia kwa zaidi ya trilioni moja fedha za kitanzania, lakini mradi huu umesimama kwa muda kutokana na pingamizi lililowekwa na Mh Zitto aliloliwasilisha Word Bank kwa madai kuwa mradi huo utaijenga CCM kisiasa kwani umekuja wakati wa uchaguzi hivyo mradi umesimama kwa muda kupisha uchaguzi.
Mzozo mwingine uliochelewesha mradi ni madai ya Zitto watoto wanaonyonyesha waruhusiwe kuendelea na masomo jambo ambalo serikali haikuwa tayari kukubaliana nalo hivyo JPM alichukua jukumu la kumwita Mkurugenzi wa World Bank Ikulu wakazungumza na kufikia mwafaka hivyo baada ya uchaguzi mradi utatekelezwa, mradi upo palepale na pesa ipo tayari
Lissu anaposema ataboresha elimu ni uongo huu mpango upo mezania tayari ni uhuni wao ndio umezuia utekelezaji wa huu mradi na ni fedha ya mkopo kutoka WB. huu ni mpango wa CCM na fedha zimetafutwa na CCM na upembuzi yakinifu umefanywa na serikali za CCM, Lissu hajui chochote juu ya huu mradi ndio maana anadandia kusema atafumua Elimu ni uongo, mpango ni kuboresha Elimu na ni mpango wa siku nyingi unaenda hatua kwa hatua. Kama kweli anajua anacho kinena mwambie awaonyeshe kabrasha la andiko mradi.