Maboresho ya Reli ya TAZARA yaangalie usifanyike udanganyifu kama wa Kenya

Maboresho ya Reli ya TAZARA yaangalie usifanyike udanganyifu kama wa Kenya

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Tumeeelezwa Rais wetu mpendwa pamoja na mwenzake wa Zambia watasaini Makubaliano na Serikali ya China kwa ajili ya Maboresho ya Reli ya TAZARA!

Kuna kaukimya fulani kwa Serikali kuhusu namna reli hii itakavyoboreshwa! Hatujui kama itaboreshwa kwa viwango vya umeme au la? Tofauti na wakati tunaanza kujenga reli ya kati ambapo kila kitu kilikuwa kinawekwa wazi! Kaukimya haka kananifanya kudhani kuwa maboresho haya yatakuwa kama China alivyowadanganya Kenya halafu akawategenezea reli ya treni ya dizeli tena kwa gharama kubwa.

Maombi yangu sasa waafrika tuonyeshe tuna akili znazofanya kazi sawa. Kama mayoress hayatahusisha kuifanya kuwa reli ya mwendokasi inayotumia umeme basi tuyakatae.

Ni maoni yangu kuwa endapo maboresho haya ya reli ya TAZARA hayatahusisha kuiboresha hii reli kuwa ya mwendokasi ya umeme basi hayatakuwa na faida yeyote kwa nchi yetu.

Soma Pia: Ili Kuongeza Ufanisi wa reli ya TAZARA,Tanzania na Zambia Ziiombe China Wajenge reli Mpya ya Makambako-Mtwara & Kasama-Lubumbashi/Likasi
 
Pamoja na kutaka reli ya kisasa ya TAZARA, iboreshwe hata hii iliyopo ili iwe katika viwango vinavyokubalika.

Mara ya mwisho mimi kupanda reli hii ni miaka 45 iliyopita.
 
Kama Zambia anaungana na Mozambique reli hii italipa? Zambia ina kihere here.
Hii reli sio kwa mizigo pekee, Pia kama ita boreshwa kwa kiwango cha SGR itakuwa safi kabisa na kutatua shida ya usafiri Kama ilivyo sasa ktk Ukanda wa TRC dar to dom

Vile vile, usalama uliopo ni Nguzo kwa biashara na nchi jirani kama DRC wanaweza chukulia mizigo Yao dry port huko Zambia 🇿🇲 Mbeya

Fursa ni nyingi zaidi
 
Geografia ya Tanzania ilikua nzuri lakini viongozi walichelewa sana kujenga miundombinu wezeshi kulinda bandari leo tunahaha tu
Huwezi kuzuia wengine kuwa na options au wasifanye biashara

Biashara itafanyika tu, ni namna ya kutengeneza mikakati ya kufanyabiashara japo tuna aminishwa serikali zinatoa huduma na sio kufanya biashara

Hizi bilateral agreements sijui mutual kitugani ndio huwa zina leta mwanga ktk maeneo mtambuka
 
Pia tujenge kwa kujiangalia Sisi kwanza na mahitaji yetu na sio kumfurahisha jirani

Jirani awe ni ziada

Tujenge miundombinu kwa ajili yetu, leo Zambia wanatua JNIA baada ya kipindi kirefu kupita, tulienda kuwaomba waje? Hapana Bali kuna vitu tukiweka sawa mteja mwenyewe anakuja bila shida
 
Tumeeelezwa Rais wetu mpendwa pamoja na mwenzake wa Zambia watasaini Makubaliano na Serikali ya China kwa ajili ya Maboresho ya Reli ya TAZARA!

Kuna kaukimya fulani kwa Serikali kuhusu namna reli hii itakavyoboreshwa! Hatujui kama itaboreshwa kwa viwango vya umeme au la? Tofauti na wakati tunaanza kujenga reli ya kati ambapo kila kitu kilikuwa kinawekwa wazi! Kaukimya haka kananifanya kudhani kuwa maboresho haya yatakuwa kama China alivyowadanganya Kenya halafu akawategenezea reli ya treni ya dizeli tena kwa gharama kubwa.

Maombi yangu sasa waafrika tuonyeshe tuna akili znazofanya kazi sawa. Kama mayoress hayatahusisha kuifanya kuwa reli ya mwendokasi inayotumia umeme basi tuyakatae.

Ni maoni yangu kuwa endapo maboresho haya ya reli ya TAZARA hayatahusisha kuiboresha hii reli kuwa ya mwendokasi ya umeme basi hayatakuwa na faida yeyote kwa nchi yetu.
Ubarikiwe sana kwa alert

But I think Tanzarep was already an sgr

Hatq Kama ni manual, tupate the best in class

And from what I know, serikali Iko very serious on that
 
Ubarikiwe sana kwa alert

But I think Tanzarep was already an sgr

Hatq Kama ni manual, tupate the best in class

And from what I know, serikali Iko very serious on that
vyovyote vile iwe ya mwedokasi inayotumia umeme
 
Beggars can't be choosers
Na hasa kwa reli hii ya TAZARA, baada ya sisi wenyewe na Zambia kushindwa hata kuiendesha tu kwa ufanisi.

Lakini ukweli ni kwamba, hata isipo kuwa ya umeme, waChina hao hao wakipewa kuiendsha patakuwepo na ufanisi mkubwa.
Kwa hiyo badala ya kulilia reli ya umeme (ingawaje ni vizuri zaidi), la msingi ni uendeshaji wa reli hiyo kwa ufanisi

Hiyo ya Kenya anayo izungumzia mleta mada, pamoja na kuwa ya diesel, lakini hadi sasa uendeshaji wake ni mzuri, kwa vile bado mChina anasimamia kazi hiyo.

Reli inaweza kuwa ya umeme, lakini uendeshaji wake ukawa mbovu, hapo faida ipo wapi?
 
TAZARA inaboreshwa mizigo yenyewe iko wapi?
Copper kutoka Zambia na Congo vinatakiwa kupita TAZARA badala ya kuharibu barabara. Mafuta kwenda DRC, Zambia na Malawi yanatakiwa kupita TAZARA. Mizigo ni mingi sana, bado watu.
 
Back
Top Bottom