Maboresho ya Reli ya TAZARA yaangalie usifanyike udanganyifu kama wa Kenya

Maboresho ya Reli ya TAZARA yaangalie usifanyike udanganyifu kama wa Kenya

Tumeeelezwa Rais wetu mpendwa pamoja na mwenzake wa Zambia watasaini Makubaliano na Serikali ya China kwa ajili ya Maboresho ya Reli ya TAZARA!

Kuna kaukimya fulani kwa Serikali kuhusu namna reli hii itakavyoboreshwa! Hatujui kama itaboreshwa kwa viwango vya umeme au la? Tofauti na wakati tunaanza kujenga reli ya kati ambapo kila kitu kilikuwa kinawekwa wazi! Kaukimya haka kananifanya kudhani kuwa maboresho haya yatakuwa kama China alivyowadanganya Kenya halafu akawategenezea reli ya treni ya dizeli tena kwa gharama kubwa.

Maombi yangu sasa waafrika tuonyeshe tuna akili znazofanya kazi sawa. Kama mayoress hayatahusisha kuifanya kuwa reli ya mwendokasi inayotumia umeme basi tuyakatae.

Ni maoni yangu kuwa endapo maboresho haya ya reli ya TAZARA hayatahusisha kuiboresha hii reli kuwa ya mwendokasi ya umeme basi hayatakuwa na faida yeyote kwa nchi yetu.

Soma Pia: Ili Kuongeza Ufanisi wa reli ya TAZARA,Tanzania na Zambia Ziiombe China Wajenge reli Mpya ya Makambako-Mtwara & Kasama-Lubumbashi/Likasi
Hayo maboresho hayapo,ni kama tu wanavyodanganya wanafanya maboresho Uwanja wa Mkapa
 
Mizigo si abiria?
Kuna mizigo mingi Sana inaenda Zambia ,congo na Malawi hii reli Ina umuhimu wake kuboreshwa Barabara ya TAZAM imezidiwa na maroli ni mengi mno plus yanayosomba makaa ya mawe bado product za chuma hazijaanza mchina sio fala akubali kutia gharama zake kuboreshwa hii reli Ina mizigo ya kutosha
 
Ni proposal ya mchina mwenyewe
As global powers vie for control over critical mineral trade routes, China plans to spend US$1 billion to refurbish a key railway line connecting Zambia's copper belt region with the Tanzanian port of Dar es Salaam under its Belt and Road Initiative.9 Feb 2024
View attachment 3086117

China plans to spend US$1 billion to revamp Tanzania-Zambia railway ...

Yaani Tanzania na Zambia wameshindwa kutoa hiyo USD 1 billion mpaka mchina aje tena kusaidia.
 
IMG-20240228-WA0000.jpg
1725424111989.jpg
 
Na hasa kwa reli hii ya TAZARA, baada ya sisi wenyewe na Zambia kushindwa hata kuiendesha tu kwa ufanisi.

Lakini ukweli ni kwamba, hata isipo kuwa ya umeme, waChina hao hao wakipewa kuiendsha patakuwepo na ufanisi mkubwa.
Kwa hiyo badala ya kulilia reli ya umeme (ingawaje ni vizuri zaidi), la msingi ni uendeshaji wa reli hiyo kwa ufanisi

Hiyo ya Kenya anayo izungumzia mleta mada, pamoja na kuwa ya diesel, lakini hadi sasa uendeshaji wake ni mzuri, kwa vile bado mChina anasimamia kazi hiyo.

Reli inaweza kuwa ya umeme, lakini uendeshaji wake ukawa mbovu, hapo faida ipo wapi?

Tuwe wafanisi, tusiwe wafanisi, HATUTAKi kuendeshewa miundombinu na Mchina, au na mja yeyote wa kigeni.

Kujenga huwezi, kubuni huwezi, kuendesha huwezi, utaweza nini, kuchimba na kuendesha miradi ya matundu ya vyoo vya washichana, wewe potato head wa Afrika ????

Kuna sababu kwa nini Julius Nyerere aliamua kui freeze on ice hii miradi kichaa ya kufanyiwa kila kitu na kuliwa kama mazuzu.
 
Wachina wanajua wanachokifanya.
Kwa sasa Zambia ni kama nchi yao.
 
Tuwe wafanisi, tusiwe wafanisi HATUTAKi kuendeshewa miundombinu na Mchina, au na mkandiga yeyote wa kigeni.

Kujenga huwezi, kubuni huwezi, kuendesha huwezi, utaweza nini, kuchimba na kuendesha miradi ya matundu ya vyoo wewe potato head Mwafrika ????

Kuna sababu kwa nini Julius Nyerere aliamua kui freeze on ice hii miradi kichaa ya kufanyiwa na kuliwa kama mazuzu
Kama unanieleza mimi moja kwa moja, nitakwambia kwamba ni sawa kabisa unavyo eleza; na huo ndio msimamo wangu katika maswala haya yote, iwe Reli, Bandari na kwingineko kote inapo wezekana.
 
Cha msingi hizi reli hata ikiwa ya umeme uendeshaji ukiwa mbovu inakufa tu mfano hii TAZARA tumeiendesha miaka mingapi bila faida hadi wanaamua kurudi tena wachina kuisimamia na Hawa wataitendea haki sisi tuliyaamini Sana maroli kuliko TREN lazima waje watubadilishe mawazo
 
Hata ikiwa ya diseli wakiongeza speed kutoka 80 hadi 120 bado itakuwa na ufanisi kuliko ilivyo Sasa masaa yatapungua kuifikia Zambia maana ya sgr Ina speed 160 km/hr 👇👇👇👇👇👇[TOP STORY] Tanzania, China, and Zambia have signed an important agreement to upgrade the Tanzania-Zambia Railway Authority (TAZARA) in Beijing. The ceremony, which took place at the Great Hall of the People, was attended by Presidents Samia Suluhu Hassan of Tanzania, Xi Jinping of China, and Hakainde Hichilema of Zambia. The agreement aims to improve the railway's capacity, efficiency, and reliability, thus strengthening regional transportation infrastructure.

#CNBCAfrica #DSTV410 #ClosingBell #CBEA
1725507604558.jpg
 
Tumeeelezwa Rais wetu mpendwa pamoja na mwenzake wa Zambia watasaini Makubaliano na Serikali ya China kwa ajili ya Maboresho ya Reli ya TAZARA!

Kuna kaukimya fulani kwa Serikali kuhusu namna reli hii itakavyoboreshwa! Hatujui kama itaboreshwa kwa viwango vya umeme au la? Tofauti na wakati tunaanza kujenga reli ya kati ambapo kila kitu kilikuwa kinawekwa wazi! Kaukimya haka kananifanya kudhani kuwa maboresho haya yatakuwa kama China alivyowadanganya Kenya halafu akawategenezea reli ya treni ya dizeli tena kwa gharama kubwa.

Maombi yangu sasa waafrika tuonyeshe tuna akili znazofanya kazi sawa. Kama mayoress hayatahusisha kuifanya kuwa reli ya mwendokasi inayotumia umeme basi tuyakatae.

Ni maoni yangu kuwa endapo maboresho haya ya reli ya TAZARA hayatahusisha kuiboresha hii reli kuwa ya mwendokasi ya umeme basi hayatakuwa na faida yeyote kwa nchi yetu.

Soma Pia: Ili Kuongeza Ufanisi wa reli ya TAZARA,Tanzania na Zambia Ziiombe China Wajenge reli Mpya ya Makambako-Mtwara & Kasama-Lubumbashi/Likasi
Pole ,Tazara itakuwa refurbished China to bring Tanzania-Zambia railway back to full speed with US$1 billion boost
Screenshot_20241004-080756.jpg
 
Back
Top Bottom