SoC02 Maboresho ya Sera za Bima ili kufikia lengo la serikali la kuwafikia wananchi walio wengi zaidi

SoC02 Maboresho ya Sera za Bima ili kufikia lengo la serikali la kuwafikia wananchi walio wengi zaidi

Stories of Change - 2022 Competition

Paul Faraj

New Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Bima ni nini?
Bima ni njia ya ulinzi wa kiuchumi dhidi ya hasara ya kifedha au hata dhidi ya kifo ambayo watu au kampuni wanafuata kwa kulipa kiasi fulani kwa shirika la bima kadiri ya mkataba maalumu, hivi kwamba shida ikitokea shirika litoe fidia.

Zipo aina mbalimbali za bima kama vile bima ya afya, bima ya maisha, bima ya magari, bima ya nyumba na vitu, bima ya uwekezaji.

Nchini Tanzania suala Zima la bima lipo chini ya mamlaka ya usimamizi wa shughuli za bima (TIRA) ambayo pia husimamiwa na Benki kuu ya Tanzania.

Ili kufikia lengo la serikali la kuwafikia wananchi walio wengi zaidi; Serikali, mamlaka na makampuni yanayojishughulisha na suala Zima la bima yanapaswa kuzingatia yafuatayo:

Uandishi wa mikataba ya bima katika lugha na misamiati yenye kueleweka Kwa Kila mtumiaji/ mteja wa bima husika hasa kabla hajaingia kusaini mkataba husika.

Katika hili makampuni yaliyo mengi yamekuwa yakitumia lugha na misamiati isiyoeleweka Kwa watumiaji (wateja) wa bima zao.

Kitendo hiki kimekuwa kama ni siraha moja wapo inayotumiwa na makampuni ya bima kuwakandamiza wateja wao.

Kwani ukiachana na lugha na misamiati migumu pia mikataba hii imekuwa ni yenye maelezo marefu yenye kumchosha msomaji kitendo kinachowapelekea wateja walio wengi kusaini pasipo kusoma yoote yaliyomo ndani.

kama tunavyo fahamu wateja walio wengi huwa wanapatikana Kwa kupata taarifa Kwa watu ambao tayari wameshapata huduma au bidhaa husika, hivyo kitendo hiki hupelekea kupungua Kwa wateja mara tu mikataba Yao inapoisha, pia kukata mirija ya wateja wapya kutokana taarifa walizopata kutoka kwa wateja wa awali.

Matumizi ya vidakuzi na kuongeeza (cookies na adds) kwenye mitandao ya kijamii pamoja na matangazo yenye ulazima ndani ya vyombo vya habari kama vile redio, magazeti na runinga.

Tumekuwa tukishuhudia matangazo mbalimbali ndani ya vyombo vya habari ambayo yamekuwa yakidhaminiwa na serikali na mashirika mbalimbali ya kimataifa.

Kwa mfano matangazo ya uzazi wa mpango, chanjo ya uviko. Hivyo ni mda sasa serikali kuhimiza vyombo vya habari kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya faida za bima ambapo katika hayo yote Serikali inapaswa kudhamini matangazo hayo au kuweka matangazo hayo kama mojawapo ya vigezo vya usajili wa vyombo vya habari ili kuweza kutangazwa mda wote wa vipindi.

Utunzi na usimamizi wa sera Bora za Serikali juu ya bima ikishirikina na mamlaka zake zinazosimamia masuala ya bima.

Katika hili Serikali inapaswa kusimamia vema kanuni na sera mbalimbali ikiwemo kupitia masharti na vigezo na mikataba inayo tungwa na makampuni mbalimbali ya Bima ili kuwalinda wananchi ambao ni wateja wa makampuni husika dhidi ya masharti kandamizi yanayokuwa yakitungwa na makampuni ya Bima.

Mbali na kusimamia masharti haya pia mamlaka zinazosimamia Bima zinapaswa kuweka kiwango Cha fedha ambacho kitatumiwa kama sehemu ya vigezo vya usajili wa kampuni ambacho kitasimamiwa na serikali Kwa ajili ya kuwalipa wateja wa Bima husika pale kampuni husika inapokuwa imefirisika ili kuwalinda wananchi waliolipa pesa zao.

Utoaji wa kifutajasho (bonasi) au kupunguza malipo Kwa wateja ambao hawakupata majanga kipindi Cha mikataba Yao.

Hii itatumika Kama sehemu ya kuongeza chachu kwa wateja kuendelea kutumia Bima husika hivyo kuwafanya waone kuwa hawajatupa pesa zao, au pesa zao hazijaweza kuwanufaisha ndani ya kipindi chote Cha mkataba.

Hii itakuwa ni njia mojawapo ya kuweza kuwavuta pia makundi mbalimbali kama vile vijana, vikundi vya akina mama, katika makundi haya hasa kundi la akina mama ambao shughuli zao za uzalishaji nyingi ni zenye uhitaji wa Bima.

Lakini kundi hili la akina mama limekuwa likitaja baadhi ya sababu ambazo ndizo kikwazo kikubwa Cha wao kushindwa kutumia Bima, sababu hizo ni kama vile kucheleweshwa Kwa malipo pindi mteja anapopata janga, japo walio wengi hutaja Bima kama chanzo Cha hasara.

Kwani nje ya majanga yaliyoainishwa katika mkataba husika hawawezi kupata chochote ikilinganishwa na kwenye vikundi vyao ambako hupeana motisha, kufarijiana, na kupongezana katika matukio mbalimbali kama vile misiba, sherehe.

Zingatia: Bima haijihusishi na ubashiri wa matukio (matukio ya kupanga) Bali kulinda mteja dhidi ya hasara inayoweza kutokea.

Ulipaji wa bima kulingana na kipato Cha mteja husika.
Katika Bima za maisha makampuni yanapaswa kuzingatia malipo ya Bima hizo Kwa kuzingatia kipato Cha Kila mteja, huku fidia zake pia zikiwa zinaendana na malipo ya mteja, tofauti na sasa ambapo aina hii ya Bima imekuwa ikitumiwa na wateja wenye kipato kikubwa.

Hivyo kuacha kundi lililo kubwa la watanzania Kwa kigezo Cha kukosa kiasi kikubwa Cha fedha.
Kwa bima zenye ulazima kama bima ya Afya.

Serikali inapaswa kutunga Sheria yenye ulazima Kwa Kila mwananchi kuwa na bima hiyo. Serikali inapaswa kulenga maeneo kadhaa ili kuongeza idadi ya wananchi / kuwafikia wananchi walio wengi zaidi kumiliki aina hii ya Bima. Maeneo hayo ni kama vile:

Vyuoni na Mashuleni. Serikali inapaswa kuweka ulazima wa Bima ya afya kama kigezo Cha ulazima ili mwanafunzi aweze kusajiliwa ikiwa ni katika vyuo vyote na mashule yote ya serikali na binafsi na kusimamiwa ipasavyo tofauti na sasa ambapo kigezo hicho hakitiliwi mkazo na kupewa kipaumbele.

Biashara na Sehemu za Kazi. Kwa wale walioko katika biashara, serikali kupitia Kwa msajili wa biashara inapaswa kuweka aina hii ya Bima kama kigezo mojawapo Cha usajili wa biashara.

Na Kwa wale walioko makazini mwajili anapaswa kukata kiasi tajwa na serikali Kwa ajili ya kugharamia Bima ya afya Kwa mfanyakazi mwenyewe na Kwa familia yake (Kwa wale wenye familia) ikiwa ni Kwa wafanyakazi wote wa serikali na sekta binafsi.

Kwa kufanya hivyo serikali itaweza kuwafikia wananchi walio wengi zaidi hasa Kwa Bima zenye ulazima kama Bima ya afya.
 

Attachments

Upvote 0
Karibuni Kwa mjadala juu ya andiko langu na Kwa wenye maswali, pia nikiomba kura zenu wote mtakao wiwa na andiko hilo
 
Back
Top Bottom