Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Kuna jamaa kasema tatizo Gen Z hawako serious, unakuta mtu anamuita Boss - Bro😂😂
=====
Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Intelligent, 1 kati ya mabosi 6 wana wasiwasi kuhusu kuajiri Gen Z tena, na 1 kati ya 7 huenda wakakwepa kabisa kufanya hivyo mwakani. Hizi ndiyo sababu:
Kutokujiongeza
Asilimia 50 ya viongozi walioulizwa wanahisi kuwa wahitimu wapya hawaonyeshi juhudi zinazotarajiwa na waajiri.
Kutokuwa na maadili ya kazi (unprofessionalism)
Hii inajumuisha kutofuata taratibu za sehemu ya kazi kama vile kuheshimu muda, matumizi sahihi ya lugha, na mavazi yanayoendana na mazingira ya kazi.
Kuchelewa mara kwa mara
Kuwasili kazini au kwenye mikutano kwa kuchelewa kumeleta usumbufu kwa mabosi na wafanyakazi wenzao.
Kutokuwa na Mpangilio
Waajiri wana wasiwasi juu ya uwezo wa Gen Z wa kudhibiti majukumu yao na kupanga kazi kwa ufanisi.
Mawasiliano Duni
Viongozi wanataja changamoto katika jinsi waajiriwa wapya wanavyowasilisha taarifa, iwe kwa maandishi au kwa mazungumzo.
Changamoto ya kushindwa kumudu majukumu ya kila siku kazini
Zaidi ya asilimia 20 ya mabosi wanasema wahitimu wapya wanashindwa kumudu mahitaji ya kila siku ya kazi.
Soma: Bosses are firing Gen Z grads just months after hiring them