Mabosi waeleza kwanini wanawafukuza kazi Gen Z miezi michache baada ya kuajiriwa. Gen Z chukua notes

Mabosi waeleza kwanini wanawafukuza kazi Gen Z miezi michache baada ya kuajiriwa. Gen Z chukua notes

Kuna jamaa kasema tatizo Gen Z hawako serious, unakuta mtu anamuita Boss - Bro😂😂

=====


Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Intelligent, 1 kati ya mabosi 6 wana wasiwasi kuhusu kuajiri Gen Z tena, na 1 kati ya 7 huenda wakakwepa kabisa kufanya hivyo mwakani. Hizi ndiyo sababu:

Kutokujiongeza
Asilimia 50 ya viongozi walioulizwa wanahisi kuwa wahitimu wapya hawaonyeshi juhudi zinazotarajiwa na waajiri.

Kutokuwa na maadili ya kazi (unprofessionalism)
Hii inajumuisha kutofuata taratibu za sehemu ya kazi kama vile kuheshimu muda, matumizi sahihi ya lugha, na mavazi yanayoendana na mazingira ya kazi.

Kuchelewa mara kwa mara
Kuwasili kazini au kwenye mikutano kwa kuchelewa kumeleta usumbufu kwa mabosi na wafanyakazi wenzao.

Kutokuwa na Mpangilio
Waajiri wana wasiwasi juu ya uwezo wa Gen Z wa kudhibiti majukumu yao na kupanga kazi kwa ufanisi.

Mawasiliano Duni
Viongozi wanataja changamoto katika jinsi waajiriwa wapya wanavyowasilisha taarifa, iwe kwa maandishi au kwa mazungumzo.

Changamoto ya kushindwa kumudu majukumu ya kila siku kazini
Zaidi ya asilimia 20 ya mabosi wanasema wahitimu wapya wanashindwa kumudu mahitaji ya kila siku ya kazi.
Kuna Dogo alikuja Field...Eti Site akawa anakuja na Jeans kubwaa na mayeboyebo makubwaa kichwani kanyoa kiduku
Nikamwambia Dogo peleka Ujinga huko nisikuone na mavazi hayo.
Hakurudi asee sjui alienda kupatia wapi field.
 
Punguzeni Umwinyi Hizi Si Zama Za Mawe Za Kati Mambo Yamebadilika,,Nyie Ndio Mnabidi Muachie Ofisi Kwa Sasa Tuondoe Fikra Za Kizamani Na Za Kizee Ili Kukimbizana Na Dunia Na Elimu Zenu Za La 7 Zilizojaa Uchawi,Majungu Na Chuki Ndani Yake..###SiWoteBaadhi###Mjifunze Kuishi Kwa Maandilizi Na Kuheshimu Nyakati Hakuna Kinachodumu Milele.
 
Shida imeanzia nyumbani, wazazi hawajafundisha vijana jinsi ya ku behave kazini. Kazini kwetu kuna kadada ilibidi wakatishe mkataba wake, yaani kalikuwa na ma excuse sio ya nchi hii. Kwenye kila wiki ana siku mbili haji kazini. Sio mgonjwa wala nini, vitu hata havieleweki. Dharau kama zote
Kabla ya kukatisha mkataba wake, mlikaa mkaongea naye?? Fresh graduates ni wadogo zetu tuwapende..
 
maboss uchwara hao japo ni kweli kabisa

mimi nikienda hospitali nikute daktari ni gen-z basi nachomoka haraka kwenda pharmacy
 
Hawa watoto wa 2000 a.k.a Generation Z au Nzi whatever. Vitoto vina mambo ya hovyo sana hivi.

Ila kitu ambacho nimewaona kuwa wanacho sana ni kukosa communication skills.

Hawa watoto hawajui namna nzuri ya kuwasiliana au kuengage na watu wengi na wanajamii. Ila kwenye mambo ya kipumbavu wapo very active.

Kwa mfano, mchukue mtoto wa ndugu yako,mdogo wako,shemeji yako, au dogo yoyote ambaye ambaye amezaliwa ndani ya kizazi cha generation Z. Kaa nae kwako halafu tazama mwenendo wake.

Utagundua kwanza wanatabia mbaya sana ya kujitenga. Wakikutana wao kwa wao utadhani mashetani wanaelewana ila ukiwa nae labda wewe mzazi au mlezi wake, utaona vinatabia ya kukimbilia chumbani na kukaa huko hata siku nzima pekee yake au akiwa na takataka mwenzake wa generation Z.

Tabia mbaya sana kujitenga na wanajamii wengine ndio maana havina adabu maana hawana muda wa kujifunza kupitia waliowazidi umri ujuaji ni mwingi kupita kiasi kazi kujitenga. Na wakikosea ukiwasema wanajifanya depression walizaliwa nayo ng'ombe hawa kumbe ni viburi tupu.

Ukikaa nao utasikia "mimi ni introvert",matako yao pumbavu hawa watoto.
Hizo ni stages tu za makuzi. Tuwapende fresh graduates. Tuwalee wadogo zetu wa Generation Z, 2000
 
Kuna Dogo alikuja Field...Eti Site akawa anakuja na Jeans kubwaa na mayeboyebo makubwaa kichwani kanyoa kiduku
Nikamwambia Dogo peleka Ujinga huko nisikuone na mavazi hayo.
Hakurudi asee sjui alienda kupatia wapi field.
Kwanini haukumuita na kumuelekeza kwa lugha ya upendo ewe mungu mtu??
 
Back
Top Bottom