Mabosi waeleza kwanini wanawafukuza kazi Gen Z miezi michache baada ya kuajiriwa. Gen Z chukua notes

Mabosi waeleza kwanini wanawafukuza kazi Gen Z miezi michache baada ya kuajiriwa. Gen Z chukua notes

Kuna Dogo alikuja Field...Eti Site akawa anakuja na Jeans kubwaa na mayeboyebo makubwaa kichwani kanyoa kiduku
Nikamwambia Dogo peleka Ujinga huko nisikuone na mavazi hayo.
Hakurudi asee sjui alienda kupatia wapi field.
Mkuu kumbe weye ni ticha.
 
Haaa haaa above 30 naogopa "kwa nini asiolewe mpaka leo", Gen Z jeuri. Sijui nitakumbilia wapi
Wasiwasi wako tu!
Huyo 30+ chukulia hajaolewa kwasababu Mungu amekuekea wewe.

Gen Z hapa kua makini ukimuonyesha una kazi nzuri, unajiweza basi atakuigizia umuoe kisha anachepuka na mtoto mwenzake. (Japo sio wote)
 
Ila tukumbuke kitu kimoja.

Hawa gen z hawakudondoka kutoka angani, ni watoto wetu na ndugu zetu. Kama wakiboronga kwa chochote sisi ndio tunatakiwa tubebe lawama. Hii ni kwasababu sisi ndio tumewazaa na kuwalea na kuwatengenza kuwa hivyo walivyo! Kama wakifeli ni sisi ndio tumefeli kwenye malezi. Maamuzi mengi ya hovyo tuliyoyafanya huko nyuma ndio yametupelekea kuwa na kizazi cha aina hiyo.
 
Wasiwasi wako tu!
Huyo 30+ chukulia hajaolewa kwasababu Mungu amekuekea wewe.
Hawa angalau, tatizo lao wana haraka kwa kuona wamechelewa. Wanataka ndani ya miezi 6 uwe umemvisha shela. Sasa ukimpa matazamio ya 1 yr umchunguze anakukimbia
 
Kwani hakuna mabosi ambao ni Gen Z Pia ?!!!

Tatizo kubwa tuseme ukweli wahitaji wamekuwa wengi, kuliko uhitaji

1739014970826.png


Pia waajiriwa hawana tena nguvu as vyama vya kazi vilikufa kifo cha kawaida ukifukuzwa hauna pa kukimbilia
 
Gen Z wetu wana taatifa nyiingi sana lakini wana processing capability ndogo mnooo hivyo mwisho wa aiku nibwatu wenye rundo la taarifa lakin maarifa wanakosa, ni finyu mnoo.
Hawana maarifa hawa watoto
 
Siku zote Mwanzo huwa ni mgumu bro. Hata hao maboss walikuwa fresh graduates pia, na wao pia walikosea na kufundishwa. Wadogo zetu tunawapenda sana na tutawafundisha pindi wanapokosea.
Ni kweli kabisa wala sipingani na hayo
Ukiwa graduates ndio maana vijana huwa wanaletwa kwenye makampuni au taasisi kunolewa na kujifunza
Kazi ni kazi inatakiwa wajifunze sana na pia vitu vikuu vya kuzingatia kwanza ni punctuality, kuelewa majukumu yako na pia kuwa muaminifu na utii pamoja na heshima
Vijana wengi nawaona wanasababisha kampuni iwe na jina baya kumbe ni individuals na sio kampuni kama kampuni
Kuna kijana nilimwambia unaendesha lorry chafu namna hii na hela ya ziada unapata ya kuoshea kwanini?
Aidha ni uchafu wako au umekula mpaka za kuoshea
Unaharibu kazi kwa vitu kama hivyo akabaki anajichekesha
Tunawaelemisha na kuwafundisha maana hata sisi tulifundishwa
 
Kuna jamaa kasema tatizo Gen Z hawako serious, unakuta mtu anamuita Boss - Bro😂😂

=====


Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Intelligent, 1 kati ya mabosi 6 wana wasiwasi kuhusu kuajiri Gen Z tena, na 1 kati ya 7 huenda wakakwepa kabisa kufanya hivyo mwakani. Hizi ndiyo sababu:

Kutokujiongeza
Asilimia 50 ya viongozi walioulizwa wanahisi kuwa wahitimu wapya hawaonyeshi juhudi zinazotarajiwa na waajiri.

Kutokuwa na maadili ya kazi (unprofessionalism)
Hii inajumuisha kutofuata taratibu za sehemu ya kazi kama vile kuheshimu muda, matumizi sahihi ya lugha, na mavazi yanayoendana na mazingira ya kazi.

Kuchelewa mara kwa mara
Kuwasili kazini au kwenye mikutano kwa kuchelewa kumeleta usumbufu kwa mabosi na wafanyakazi wenzao.

Kutokuwa na Mpangilio
Waajiri wana wasiwasi juu ya uwezo wa Gen Z wa kudhibiti majukumu yao na kupanga kazi kwa ufanisi.

Mawasiliano Duni
Viongozi wanataja changamoto katika jinsi waajiriwa wapya wanavyowasilisha taarifa, iwe kwa maandishi au kwa mazungumzo.

Changamoto ya kushindwa kumudu majukumu ya kila siku kazini
Zaidi ya asilimia 20 ya mabosi wanasema wahitimu wapya wanashindwa kumudu mahitaji ya kila siku ya kazi.
Utanisamehe Ila kutamka neno boss sijawah kuwapigia magoti Ata wazazi au kuwa omba samahani🤣sembuse mtu baki tu
 
Back
Top Bottom