Mabraza wa Kariakoo na dili zao

Dah hii ni Extra Miles Bruh ... Nimewakumbuka ma bro wa TMK, tembea Tandika yote ile tena shuka mpaka Yombo huko Relini, Mnanda daily Mtaani tena hapo Mateja Kibaoooo

Rip all of em
Chichi Baunsa,Bangua,Nanga Boy Simela,Mudy Gayi,Ogola,Ally Mbumo,Njeche nk

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Iseee! Patel kama ndo wenyewe hao mbona ulichukua pesa ndogo sana. Hapa code inazingatiwa maaana kuna vitu nikiconnect balaa.
Nikapata mchongo unatofautiana kidogo sana na huo basi muhindi akaruka hewani anatafuta mtu wa kusafirisha madini kutoka congo mpk tz hapo kumbuka wajomba zangu kitambo wako kwenye hizo mishe na ndio walioniunganisha na muhindi na wao wako Congo, kiufupi nilienda kwa lori sikupata shida mpk wakati wa kurudi mzigo ninao naambiwa kuwa makini madini huwa yana harufu. Basi nikajibebisha kwa dereva aliekua anarudi bongo ili yangu yaende bwana eee kadri nilivyokua naisogelea bongo shetani ananimbia utajiri huo unao toroka..... Sikua na simu lakini kila mji nilikua na maelekezo yake na kumbe kuna mtu sikuwa najua kama ananifatilia kila steps! Nafika mpkaani nikapanda bus mpka dar ile kufika tu wazee hawa hapa nikatoa mzigo nikapewa changu kwa usalama wangu sikwenda hotel walinitafutia night club asubuhi nikarudi zangu kwangu na maokoto kusubiri madili mengine. Umenikumbusha moja ya harakati zangu...... Siku nikipata muda ntaongeza manjonjo na viuongo kuficha id yangu nielezee vizuri. jf kuna watu wengi
 
Asante sana.. binafsi nitasubiri kwa hamu kusoma toka kwako....
 
Noma sana!
 
Aiseh ni kamaaa!!
 
Hii si yakukosa
 
Kaa pale , dah sisteri mpaka hapo ID yako wafiche wengine ila wewe ni dada angu hizo harakati zako zimekutambulisha vilivyo kwangu nakumanya vyema .

Wale wahindi wako walishanichezea mchezo mchafu ila alhamdulilah nilikuja kulala na dada yao .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Mi sio dada ako bwana wwee! Nina uhuru wa kuongea hapa sababu hata mume wangu hajui
Vitu ambavyo nimewahi kufanya na sembuse familia yangu kaka kama wewe..... Sina kaka ujue, braza alizamia kitambo ujerumani mpaka sasa ivi namsubiri labda ipo siku ntamuona!!!.. Mi roho ngumu sina baba wala mama niliyopitia na uanaume wako hujawahi na hutawahi!. Hata humu jf member wawili tu ndo wananijua tena kupitia id tofauti na hii.
 
Natupia dili lilonipatia maokoto kizembe,
Basi 2016 niko zangu shoga angu akanipigia simu wee leo dada uko wapi? Fanya haraka kesho saa kumi uwe umefika kuna ramani huku. Basi nilifika kwa muda muafaka nikakutanishwa na boss.. Huyu bosi yeye ni dalali wa mabosi wenye pesa zao basi nikaelekezwa mchongo uko hivi unapewa pesa unaingia pori kununua mazao na kila mtu anapewa pesa kulingana na uaminifu wake na aliempeleka. Tulikua wengi wengine watu wazima kabisa kama kumi ivi! Basi baada ya mawaiza ya hapa na pale tukaanza kugawiwa pesa Yule shoga alipewa mil 100, mimi 50 wengine mpka mil 200 inategemea uzoefu! Hapo mnakubaliana bei kama gunia la mahindi ni laki moja bei mliyofungia basi ikipungua ni yako hakuna malipo rasmi ni akili yako tu! Mungu alivyomkubwa kama baada ya siku mbili jioni yake tunajiandaa tuanze safari ya pori boss alipigwa mzinga bonge la ajari aligongwa na roli kiufupi alitoka vipande vipande..... Huku wanachama tukaitana inakuaje tukimbie au?! Mtandao mkubwa tutakamatwa twende msibani tukasikilizie, basi mpaka msiba unaisha jamani hakuna alieuliza wala nn!! Wahuni wengine walienda kuchoma ofisi yake kupoteza ushahidi kabisa.
Yule shoga angu akaniambia hapa kila mtu njia yake ikipatikana ramani tutatafutana mie huyooooo mpaka Zanzibar, nikatoa kwanza 10ml ya kunipoza kula bata nikamsuprise shemeji yenu nikamtumia tiketi anifate,. Kufika full misifa babe mpambanaji wewe( kimoyoni laiti ungejua nyau wewewee)
Basi hiyo pesa niilipata bila stress wala kuvuja jasho kwa aina yoyote ile. Pesa iliobaki tulijenga kamjengo mkoani hukoo nikakaa kusubiri simu nyingne.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…