TUNAVUKA MPAKA NA KUINGIA DRC!!!!!
Basi wenyeji wetu wakatuletea ugali na samaki tukala...baada ya hapo tukafunga funga mabegi yetu madogo ya mgongoni!!
Kumbuka tulikua porini nje kabisa ya mji mdogo wa Miduha......pale tulipokua ni kilimani maana ukishuka kidogo tu unaingia DRC kwenye misitu na mapori kati ya mji wa Bukavu na Uvira uelekeo kuelekea mji wa Kitenge,ambapo ndio starting point ya kuanzia tour yetu ya kutazama fursa.
Sasa wale wadau wetu wakatugongea mlango"""Hey bana tanganyika mko kwa fuasi tuondoke bayemba bayemba"""""
Ndagara akawajibu""""Nzala bayemba bayemba tuko kwa fuasi"""""
Wakatupokea mabegi yetu na tukatoka nje ya nyumba na kushuka chini kilimani mpaka chini kabisa..
Daaaah na msimu wa mvua ulikua ndio umeanza maana niliambiwa kule DRC kwenye misitu mvua inanyesha miezi kumi kwa mwaka mzima sasa sijui ni ukweli ila mimi nilikuta mvua kubwa tu kwa siku zoote nilizokaa misituni kati ya Burundi na DRC.
Waongozaji wetu walikua watu watano....watatu walikua na silaha na wawili walibeba mabegi yetu na mizigo yao.
Wote walivalia kiraia kama sisi na ilikua saa tano kasoro asubuhi ila kulikua na ukungu mkubwa kwa sababu ya mvua.
CHANGAMOTO YA KWANZA:
Pale tu tulipofika kule chini kilimani kabla harujatembea umbali mrefu ili kuingia aridhi ya DRC tulikutana na kundi kubwa la asikari wa jeshi la Burundi wakiwa katika doria ya mpaka wao dhidi ya waasi wa kitusi wa kirundi waliojificha kwenye misitu ua DRC hasa kutokea jimbo la Kivu kusini.
Muongoza msafara akatoa ishara tusimame na kulala chini kwenye majani na tutulie tuli......!!!Wao walikua hawatuoni ila sisi tunawachora tu walipokua wanapita kichakani kwa mstari mmoja ulionyoooka huku wengineo vichwani wakiwa wamebeba masufuria na madumu na silaha na kuni wanaongozana kuelekea destination ya doria yao.Sisi pale chini tumelala tuliiii....mpaka wakapita wote na idadi yao ni kama 150 hivi na ushehe.
Walipopita basi sisi hao tukainuka na kuvukia upande wa DRC na kuendelea na safari yetu.
Kumbuka tunapitia pori kwa pori na hakuna barabara zaidi ya kukata majani ya miti na mapanga na kuvuka mabwawa ya maji yaliyosababishwa na mvua zinazonyesha mwanzo huu wa mwaka.
Baaada ya masaa matatu au manne kutokea pale mpakani tukafika sehemu ya kijiji kinaitwa Punge na wakazi wa pale ni wa kabila moja na wale waongozaji wetu...na hapo ni katikati ya Uvira na Bukavu katika uelekeo wa kuelekea mji wa Kitenge.
CHANGAMOTO YA PILI:
Wakati ndio tumefika nje ya nyumba ambayo ndio tunatakiwa tupumzike pale Punge ghafla tukasikia mlio ya miluzi na wenyeji wetu wakatuchukua haraka kutukimbiza kwenye mashimo yaliyokua katikati ya ua wa ile nyumba na kwa juu wameweka mawe makubwa ya kusagia unga wa mihogo.
Ndani ya yale mashimo ni kama mahandaki kumeifadhiwa magunia ya mihogo mikavu kwenye vichanja vilivyojengewa humo humo shimoni kwa utaalamu wa ngazi kwa ngazi......na yale mashimo ni marefu futi sita kwa tisa kama sikosei hivi....kwa juu ndio wameweka vifuniko vya majani na mawe ya kusagia ili kupata unga wa mihogo.
Nilikuja kujua baadae kua wanafanya vile ili kutunza akiba zao za chakula dhidi ya wezi na waasi na wanajeshi wa vikosi vya serikali ya DRC.
Tukaingia mle ndani haraka sisi wote watu saba.
Ila kuna matundu madogo madogo kwa juu unaweza kuchungulia nje....mara nasikia milio ya magari na viatu vya watu vinakimbia kimbia.....nikainuka kuchungulia na kuona pale juu uwanjani zimepaki landcruser za kijeshi kama tano na wanajeshi wameshuka na kuanza kukagua kagua nyumba za pale kijijini na kuzungumza na wanakijiji afu baadae wakaondoka.
Baada ya mda nikasikia mluzi tena na wakaja watu wakatoa lile jiwe kwa juu,afu wakatuwekea ngazi tukatoka taratibu mpaka nje.
Tukapelekwa mpaka kwenye ile nyumba ya mwanzo tukaingia ndani....tukakaa chini tumechoka kweli na hiyo ilikua mida ya saa kumi kasoro.
Hapo tukapumzika kidogo na tukapatiwa uji wa mihogo afu safari ikaendelea mida ya saa moja jioni.....hapo kila mtu na tochi yake mkononi ila haturuhisiwi kuziwasha mpaka kiongozi wa msafara atoe ruksa....sababu kuwasha taa usiku ni hatari sana hasa msituni.
CHANGAMOTO YA TATU:
Tulipotembea umbali mrefu mpaka saa nne za usiku tukaamua tupumzike katika eneo ambalo ni kambi ya waasi wa KIBANGU BANGU waliyokua wameitelekeza baada ya kushindwa na vikosi vya majeshi ya FARDC na kukimbia.
Kambi yenyewe ni vibanda vilivyovunjika na majani yameota kila mahali maana kambi ilikua imetelekezwa mda mrefu.
Tukachagua vibanda vyenye nafuu kidogo tukajiegesha tujipumzishe.
Mda hata hatujatulia kidogo tukaanza kusikia mlio ya risasi kwa mbali......basi fasta fasta wale waongozaji wetu wakatutoa eneo lile na kuingia pembeni kwenye misitu ile na kutupandisha juu ya miti na rochi zote zikazimwa tukabaki tunaisikilizia ile milio ya risasi.
Milio ile ghafla ikakoma afu kujawa kimya sana na tukaanza kusikia vishindo vya watu wanaokuja kwa kukimbia na kumbe ni Wabangu bangu militia,s wamerudi kuchungulia kambi yao waliyoitelekeza.
Na kiasili Wabangu bangu na Makemba Bunene ni maadui wa jadi kwa sababu wote ni wezi wa madini na wanatafuta kumiliki maeneo na kuisumbua serikali ya DRC.
Mara zikaanza risasi kulia kuja ule upande wetu ila zinapita kwa chini....ni usiku unaona cheche na kusikia matawi ya miti mifupi inakatika tu....kwa mda wa dakika tatu afu kukawa kimya kwa mda wa nusu saa......mara ukasikika mluzi tena na vishindo vya watu kuondoka eneo la kambi ile kwa kukimbia na kuimba nyimbo zao....kumbuka sisi tupo pale juu ya miti tunasikilizia.
Baadae wale waongozaji wetu wakatuambia huenda wale wabangu bangu walipata taarifa kua kambi yao imevamiwa tena na wanajeshi wa serikali wa FARDC kutoka Bukavu au Uvira au waasi wa kinyarwanda na....ndio maana wakaja kuwaharibia ila walipofika wakakuta kambi ni tupu ndio maana wakaondoka.....na waliowapa taarifa ni watu wao MBILIKIMO WA MSITUNI ambao walitufananisha na wanajeshi wa FARDC au waasi wa kinyarwanda.
Tulishuka pale juu ya miti taratibu na tukaendelea na safari yetu mpaka usiku wa manane ndio tukafika kijini kilichochangamka kiitwacha Zendi au Zendika sikumbuki vizuri na hapo ni eneo rafiki kwa waongozaji wetu,,,,tukapata nyumba ya nyasi ya kupumzika ambayo ndani yake mlikua ni kama ghala la vifaa ila tukatandika chini matandiko tukalala tumechoka balaa maana tumetembea masaa manne au matano bilia kupumzika afu ni usiku wenye baridi balaa.
Ili asubuhi tukiamka tuendelee kuitafuta KITENGE ambayo ndio starting point yetu ya kutazama fursa.
CHANGAMOTO YA NNE:
Mda wa alfajiri nikashitushwa na Ndagara aliesema dogo vaa vizuri tuondoke maana huku usijiachie kama nyumbani Tz.Fasta nikaweka vitu vyangu sawa na kutoka nje ya ile nyumba tuliyofikia.
Kumbe bhana kijiji kizima wana Zendi ni masoja na hakuna akina mama wala watoto bali wazee wa kazi....na kile kijiji ni kambi yao isiyo rasmi....afu wake na watoto wao wanawaficha porini au kwenye miji mikubwa mikubwa especially kwenye mji wa KITENGE.
Na taarifa zetu zoote walikua nazo kutuelezea sisi ni kama wadau ambao tunaweza kuwatafutia masoko ya uhakika ya kuuzia mawe yao nchini Kenya na Tanzania.
Basi wakaongea kibangu bangu pale na bro Ndagara afu tukapewa makoti ya kuzuia mvua.....tukaanza safari ile alifajiri pori kwa pori....kuutafuta mji wa KITENGE....!!
DRC bhana hakuna barabara za uhakika hasa kipindi cha mvua na hakuna usalama kabisa maeneo ya mashariki...maana ilikua tukitembea mara tusimame tuchunguze uelekeo....mara tujifiche wakija watu karibu yetu.
Kwahiyo mwendo wetu ulikua wa pole pole pori kwa pori afu mvua inanyesha na inakata.
CHANGAMOTO YA TANO:
Humo njiani tukielekea mji wa KITENGE tulifika sehemu ya milimani hivi,kuna uwanda mkubwa wa majani majani.Tulikuta vita kati ya waasi wa vikundi vidogo vidogo vya waasi walikua wamedhulimiana madini.
Ikabidi tutulie huku juu ya kilima huku wale waongozaji wetu wakitafuta njia salama ya kupita chini ya vile vilima.
Tatizo la waasi wanapigana kama watoto....mara wanakimbizana...mara wanasimama na kutukanana...mara wanaimbaimba na kukata mauno....mara wavute bangi....mara wapige risasi hewani......Basi ilikua tafarani......ilibidi tutulie kule juu ya kilima masaa matatu afu ndio tuangalie utaratibu wa kushuka chini ya vile vilima ili tuendelee mbele uelekeo wa mji wa KITENGE.
Hiyo ilikua inaelekea adhuhuri na tulikua hatujapumzika toka asubuhi ila kwa sababu ya mvua hakukua na jua kali mpaka mda huo.
ITAENDELEA.........!!!!!!!