Mabraza wa Kariakoo na dili zao

Mabraza wa Kariakoo na dili zao

Natupia dili lilonipatia maokoto kizembe,
Basi 2016 niko zangu shoga angu akanipigia simu wee leo dada uko wapi? Fanya haraka kesho saa kumi uwe umefika kuna ramani huku. Basi nilifika kwa muda muafaka nikakutanishwa na boss.. Huyu bosi yeye ni dalali wa mabosi wenye pesa zao basi nikaelekezwa mchongo uko hivi unapewa pesa unaingia pori kununua mazao na kila mtu anapewa pesa kulingana na uaminifu wake na aliempeleka. Tulikua wengi wengine watu wazima kabisa kama kumi ivi! Basi baada ya mawaiza ya hapa na pale tukaanza kugawiwa pesa Yule shoga alipewa mil 100, mimi 50 wengine mpka mil 200 inategemea uzoefu! Hapo mnakubaliana bei kama gunia la mahindi ni laki moja bei mliyofungia basi ikipungua ni yako hakuna malipo rasmi ni akili yako tu! Mungu alivyomkubwa kama baada ya siku mbili jioni yake tunajiandaa tuanze safari ya pori boss alipigwa mzinga bonge la ajari aligongwa na roli kiufupi alitoka vipande vipande..... Huku wanachama tukaitana inakuaje tukimbie au?! Mtandao mkubwa tutakamatwa twende msibani tukasikilizie, basi mpaka msiba unaisha jamani hakuna alieuliza wala nn!! Wahuni wengine walienda kuchoma ofisi yake kupoteza ushahidi kabisa.
Yule shoga angu akaniambia hapa kila mtu njia yake ikipatikana ramani tutatafutana mie huyooooo mpaka Zanzibar, nikatoa kwanza 10ml ya kunipoza kula bata nikamsuprise shemeji yenu nikamtumia tiketi anifate,. Kufika full misifa babe mpambanaji wewe( kimoyoni laiti ungejua nyau wewewee)
Basi hiyo pesa niilipata bila stress wala kuvuja jasho kwa aina yoyote ile. Pesa iliobaki tulijenga kamjengo mkoani hukoo nikakaa kusubiri simu nyingne.
Hapo umepambana au umeingia kwenye mtego wa kuzurumu?.
 
SIMULIZI ITAENDELEA NIPO NJIANI NARUDI KIGOMA........!!!!!
UNAJUA WADOGO ZANGU NIWAMBIE KITU KIMOJA.
VIJANA WA KITANZANIA TULIOTOKEA MAISHA YA KAWAIDA TUNAPAMBANA SANA NA HAMUWEZI KUELEWA.
TULIFIWA NA WAZAZI TUKIWA WADOGO..... NA BAADHI YA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WALITUTENGA KIMAKUSUDI AU LABDA WALICHOKA KUTUSAIDIA.....HATUWALAUMU SABABU NA WAO WALIKUA NA MAISHA MAGUMU KAMA MNAVYOJUA MAISHA YA KITANZANIA.
MUNGU NI MWEMA MTAANI MABRAZA HAWAKUTUTENGA HIVYO HIVYO WALITUPA SUPPORT HATUWEZI KUWASAHAU JAPO WALITUFUNDISHA MEMA NA MABAYA.
*USHAURI USIO RASMI NO 1
VIJANA WA KISHUA HAMWEZI KUELEWA.
VIJANA MLIOPATA AJIRA ZA SERIKALINI SEHEMU NYETI HAMUWEZI KUELEWA,WENYEWE MNAJIITA WATU WA KWENYE SYSTEM.
VIJANA MLIOPEWA URITHI NA WAZAZI WENU HAMUWEZI ELEWA JINSI MLIVYO NA BAHATI.
PUNGUZENI KUWAHUKUMU SANA VIJANA AMBAO BADO WANAJITAFUTA
*USHAURI USIO RASMI NO 2
VIJANA AMBAO MLIPATA BAHATI YA KUPATA WATU WA KUWASHIKA MKONO HAMUWEZI KUELEWA.
MSIWASEME VIBAYA VIJANA AMBAO BADO HAWAJAFANIKIWA.
WASAIDIENI PALE MNAPOWEZA HAMUWEZI KUJUA KESHO.
**********************************
VIJANA WA KITANZANIA ACHENI KUWAAMINI SANA MOTIVATION SPEAKER KWENYE MITANDAO....97% WANAONGEA VITU VYA KUFIKIRIKA... . TAFUTENI MABRAZA WA KITAANI WAWAPE MIPANGO HALISIA.
VIJANA WA KITANZANIA WANAHITAJI KUPATA WATU WA KUWASHIKA MKONO NA KUWAONYESHA FURSA....ILA KIZAZI CHA SASA NI CHA WATU WABINAFSI...TOFAUTI NA SISI KIZAZI CHA MIAKA YA NYUMA.
ILA MSIFE MOYO WADOGO ZANGU......CHA MSINGI JIFUNZENI KUISHI NA WATU VIZURI SABABU.......WATU NDIO KILA KITU!!!!
ANGALIZO*
KUNA WATU WAKIWAADITHIA WALIPOTOKEA HAMUWEZI KUAMINI.....!!!
KWAHIYO USIWAHUKUMU
UKIONA WAMEKUA MATEJA
UKIONA WAMEFUNGWA JELA
UKIONA WAMEFIA UGHAIBUNI
UKIONA HAWAJAFANIKIWA.
USIPENDE KUWAHUKUMU VIJANA WA KITANZANIA WANAPITIA MENGI.
VILE VILE USISHOBOKEE SANA HELA ZAO....MAANA WANAJUA WALIPOZITOA.
TANZANIA NGUMU KAMA HAUNA CONNECTION.
TANZANIA NGUMU KAMA HAUNA WATU WA KUKUSAIDIA.....NA NI MUNGU PEKEE ANAYELETA BAHATI NA FURSA KWA VIJANA WA MTAANI.
**JAMII HAITUELEWI
JAMII HAITUELEWI SABABU HATUELEWEKI KUTOKANA NA HISTORIA YA NYUMA....!!!
KUSEMA KWELI TUSHAKUAGA VIBAKA.
TUSHAKUAGA WAHUNI WASIO NA AKILI.
TUSHATAPELI.
TUSHADANGANYA SANA.
TUSHADHULUMU SANA.
TUSHAWAINGIZA MJINI SANA WAZEE WA MIGODINI MPAKA TUNAJISIKIA HATIA NA AIBU KWENYE NAFSI ZETU.
JAMII INAYO HAKI YA KUTOTUELEWA VIJANA WA MTAANI NA WALA HATUILAUMU KWA HILO...TUNAOMBA MSAMAHA JAMII ITUSAMEHE
SABABU TULIANZIA NEGATIVE KWENDA POSITIVE.
MIMI NAHADITHIA HARAKATI ZANGU KUWATIA MOYO WADOGO ZANGU KUA MTAFUTAJI HACHOKI NA AKICHOKA BASI HUYO UJUE AMESHAPATA.
HAKUNA KUKATA TAMAA MUNGU YUPO.
KAMA WAO WAMEPATA UKWASI...BASI HATA SISI TUNAWEZA KUUPATA PIA HUO UKWASI.
MUNGU NI MWEMA.
Kwenye hii season kuna ushauri mzuri sana ila sasa nina wasiwasi na ushauri wako kwa vijana au wadogo zako.

Je, ni lazima wapitie njia yako as kufundishwa na hao unaowaita mabraza, maana katika kila njia uliyopitia nimesoma mabraza wako hawakuwa na njia sahihi ya kupata mkate ni njia hatarishi!.

So kuna haja ya kurekebisha kwa kuwaeleza vijana, wadogo zako kuwa mabraza si lazima wawe wezi, vibaka, wazurumao ni hata mabraza smart wanaokubali kuwashika mikono wadogo zao.

Mfamo hata wewe kwa sasa, baada ya mafanikio labda ya madini (najua kwa sasa DM yako ipo busy madogo na vijana wakitaka uwape connection) hapo ina maana hawatapitia kule mwanzo ulipopitia kwenye ukabaji na utapeli ila utawashika mkono kupitia mafanikio ya sasa.

Aluta ...
 
Kwenye hii season kuna ushauri mzuri sana ila sasa nina wasiwasi na ushauri wako kwa vijana au wadogo zako.

Je, ni lazima wapitie njia yako as kufundishwa na hao unaowaita mabraza, maana katika kila njia uliyopitia nimesoma mabraza wako hawakuwa na njia sahihi ya kupata mkate ni njia hatarishi!.

So kuna haja ya kurekebisha kwa kuwaeleza vijana, wadogo zako kuwa mabraza si lazima wawe wezi, vibaka, wazurumao ni hata mabraza smart wanaokubali kuwashika mikono wadogo zao.

Mfamo hata wewe kwa sasa, baada ya mafanikio labda ya madini (najua kwa sasa DM yako ipo busy madogo na vijana wakitaka uwape connection) hapo ina maana hawatapitia kule mwanzo ulipopitia kwenye ukabaji na utapeli ila utawashika mkono kupitia mafanikio ya sasa.

Aluta ...
Umeongea kwa usahii kabisa....na nakubaliana na ww!!!
 
Bro I appreciate this kaka unatoa funzo kubwa sana kwa sisi wadogo zako..Mimi nimetoka Duce graduate wa 2016 lakini kutokana na tatizo la ajira nilikua kusaidiwa na braza mla ngada na vilevi vyote mpaka sasa Nina familia na watoto wawili..Ukikaa na baharia yeyote wanajua sana kutoa ramani za maisha
Mungu ni mwema.......mshukuru Mungu
 
Back
Top Bottom