Mabroo wa miaka 40+ tupeni ushauri namna ya kuukimbia umaskini,vijana mnaojitafuta pitienj huku!

Joined
Sep 6, 2021
Posts
49
Reaction score
26
Vijana wanaojitafuta katika mazingira ya kiafrika wamekua wakikumbana na changamoto nyingi zinazopelekea kubaki katika dimbwi la umaskini. Hata hivyo,kuna watu wamefanikiwa kujikwamua kiuchumi katika mazingira hayohayo,tunahitaji kupata maelekezo kidogo kutoka kwa wakubwa zetu waliofanikiwa kujipata,waliwezaje,walizingatia nini wakati wa hustle zao angalau na sisi tufikie walau robo ya walichochacho.
NAWASILISHA!!!
 
Kijana chunga sana. Dunia imeharibika hii. Hakuna Msaada wa bure
 
Ukimbie umasikini kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa ubunifu

Epuka kubeti, madawa ya kulevya na kamari za aina zote.

Ikiwa utavuta bangi, basi vuta ule muda wa kulala tu kwaajili ya kuponya afya yako ya mwili na akili... Ukiizoea inakupoteza lakini ukifuata hii ratiba utaziona hazina za gizani
 
Vijana wanaojitafuta katika mazingira ya kiafrika wamekua wakikumbana na changamoto nyingi zinazopelekea kubaki katika dimbwi la umaskini. Hata hivyo,kuna watu wamefanikiwa kujikwamua kiuchumi katika mazingira hayohayo,tunahitaji kupata maelekezo kidogo kutoka kwa wakubwa zetu waliofanikiwa kujipata,waliwezaje,walizingatia nini wakati wa hustle zao angalau na sisi tufikie walau robo ya walichochacho.
NAWASILISHA!!!
Punguzeni ku fake maisha tu.
 
hakuna mtu atakayekuambia siri ya mafanikio yake,,, zaidi sana atakuambia kaza, kumbe mshenzi ana mbinu zake hataki mtu azijue ! #walimwengu
 
Nyumba ndiyo baraka ya kwanza kwa mwanadamu, hela zikikutembelea hakikisha una nyumba yako.
 
Mche Mungu wako, Jiamini katika kila unachofanya. Kuwa na maono na nidhamu ya pesa na uishi na watu vizuri.
 
Pambana usikubali kubaki kwenye umasikini , Billgate aliwahi kusema Siyo kosa kuzaliwa masikini bali nikosa kufa masikini. U have to fight until the end of ur life .
 
Mtangulize Mungu sana kwenye hussle zako ,

Amka mapema sana asb na chelewa pia kulala ukipambania ndoto zako usichague kazi, tengeneza mifereji yako mingi mingi ya kukuingizia hela .

kaa na watui wenye fikra+ usipoteze muda kwa watu wanafki wanao kuwazia mabaya muda wote, watu wengi sana ni wanafki especially ndugu usimuamini kabisa mtu anaitwa ndugu wala kumuonesha ndoto zako za upambanaji
weka mbali kabisa na watoto. ukiishi maisha yako ukimtegemea Mungu unatoboa kikubwa sala na kazi kwa bidii.
 
Back
Top Bottom