Mimi napendelea hata zile nyama za kwenye makopo!!! Chumvi kwa wingi, standardized kokote pale duniani. Na ukizijulia kuzifungua, mtu weweeee.... usiku, jioni, asubuhi, adhuhuri, mchana, twende tu!! Hamna anayekuhoji wala kukukodolea macho. Kwenye mikate, kwenye chapati na kwa kuziunga kidogo, poa tu!! Yanini kwenda kusimama kwenye mibucha na kutoka huko na shombo na miinzi ikiwa inakufata nziiiiiiii nyuma nyuma, eti tu umejibebea nyama fresh!! mweee!!!Najua wengine mnazipenda lakini mnaziogopa kwa kutojua kuzifungua... maana kukatwa vidole na tule tubati, ni noo -- nooouma!!! lol 😉