KERO Mabwepande hatuna daladala, tunateseka kwa nauli za Bajaj. Tupate daladala angalau hadi Tegeta

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mabwepande kuelekea Bunju B ni Shilingi 1,500 kwa Bajaj kitu ambacho ni gharama kubwa kwa wananchi wa hali ya chini, ushauri wangu zipatikane daladala zitoke Mabwepande ziende Tegeta Nyuki, ambapo kila mtu anaweza kuafodi nauli hata wanafunzi wa shule itawarahisishia sana.

Zipatikane daladala zitoke Mabwepande zije mjini vyovyote vile lakini kule ziwepo daladala tu ili kusudi wasioweza nauli ya Bajaji wapande daladala na isitoshe kule kuna Hospitali ya Wilaya sasa bajaji zimepanda nauli kwa sababu ya mafuta wako right lakini ikiwepo daladala watapanda watu wengi hata bei iwe Sh 1,000 kama ruti zingine.
 
LATRA ni kama kijiwe cha masela hata zikiwepo daladala hazijafika Mabwepande na kama zitafika labda asubuhi sana na jioni saa kumi hadi kumi na mbili au saa moja baada ya hapo mateso yatabaki pale pale kwa sababu ya usimamizi duni na kulindana lakini pia ile njia inasababisha daladala zisifike kwa sababu ya ubovu hasa kipindi cha mvua hivyo Serikali iweke lami kutokea Magufuli hadi bunju halafu ziwepo daladala za Magufuli to Bunju sokoni kupitia Mpiji Magoe Mabwepande
 
Mabwepande kuelekea Bunju B ni Shilingi 1,500 kwa Bajaj kitu ambacho ni gharama kubwa kwa wananchi wa hali ya chini, ushauri wangu zipatikane daladala zitoke Mabwepande ziende Tegeta Nyuki, ambapo kila mtu anaweza kuafodi nauli hata wanafunzi wa shule itawarahisishia sana.

Zipatikane daladala zitoke Mabwepande zije mjini vyovyote vile lakini kule ziwepo daladala tu ili kusudi wasioweza nauli ya Bajaji wapande daladala na isitoshe kule kuna Hospitali ya Wilaya sasa bajaji zimepanda nauli kwa sababu ya mafuta wako right lakini ikiwepo daladala watapanda watu wengi hata bei iwe Sh 1,000 kama ruti zingine.
Sawa kabisa kabisa
Tena kuna ofisi za kata kule, mashauri ya kila aina yanafanyika.
Hili swala na ombi ni muhimu kuliko.
 
Back
Top Bottom