kuna watu hapa naona wamesimama hoja mtu aishi apendavyo kijamii haipo hivyo kabisa mtu anapotoka nje ya mstari anapaswa kurudishwa kwenye mstari, unakumbuka kesi ya Songea jamaa alikuwa anaishi na mama yake mzazi mpaka akamgeuza kuwa mke wake akawa anamlala mama yake mzazi watu hili hawalioni kama laweza tokea, mtu akiishi muda mrefu na wazazi wake zaidi 30+ hata akili huwa zinapotea hana maarifa ya kujitegemea kila kitu anapewa na wazazi watu hawa pindi wazazi wao Mungu anapo wachukua hugeuka kero mitaani mara umepigwa ngeta n.k
Akili yako inagota mapema sana. Tena una taahira ya uelewa sio bure. Naona umeamua kutuwekea na picha ambayo bila shaka haiendani na kitu kinachozungumzwa hapa.
Juzi hapa wanafunzi wa IFM wameingiliwa na mateja, je tukio hilo moja ndio kigezo kwamba kukaa hostel ni vibaya? Tumia akili yako wewe.
Nachoweza kukueleza ni kuwa, umbea ndio unaokufanya unashindwa kutanua akili yako na kutafuta sifa kumekupofusha ukafikiri wewe ndio uko sahihi saaana. Hebu tumchukulie huyo mume wenu TID kama mfano: (Nimesema mume wenu kwa kuwa wenyewe mmeamua kufuatilia maisha yake binafsi as if mnataka awaoe):
Mtu kuishi na mama yake na mtu kumtegemea mama yake ni mambo mawili tofauti. Kama TID anamtegemea mama yake kwa mahitaji, kiukweli si jambo jema. Hata hivyo, kwa kuwa siijui hali yake na nini kitakuwa kimepelekea hilo, basi si vyema kwangu kuanza shutuma dhidi yake.
Kwa upande mwingine, TID anaweza akawa anakaa na mama, lkn ni yeye mwenye kuwasapoti hapo nyumbani kwa mahitaji muhimu. Lets say nakaa nyumbani na nina ajira ya uhakika. Nikaona ni vyema kuendelea kuwepo hapo wakati najenga nyumba yangu. Uwepo wangu pale nyumbani na uwezo wangu wa kiuchumi unanifanya mm niwe nategemewa na familia kuwapatia mahitaji (baadhi) labda ndio nalipa umeme, maji na nanunua chakula.
Sasa katika hali ya kushangaza, wanaume (mnaojiita wanaume) tayari mmekurupuka na kukonkludi kuwa TID analelewa. Je huwa mnakuwepo kwao asubuhi wanapopanga bajeti za matumizi yao au ndio mnawashwa?
Na hizi tabia zenu ni matokeo ya kukulia kwenye nyumba za kupanga, tena uswahilini. Huko ndio mmejifunza umbea kwa mama zenu kiasi sasa maisha ya watu wengine ndio mada zenu.
Naanza kupata picha za maisha yenu kwa maneno yenu kwani mwenzako amesema ni mbaya kupishana na mama koridoni na taulo. Hapo napata picha ya nyumba ya kupanga ile ya kushea choo nje sasa mnadhani watu wote wanaishi hivyo. Wenzenu tuna nyumba zenye vyoo ndani kwa hauna nafasi ya mimi kukutana na mama na taulo wakati nina choo ndani kwangu. Halafu inaonesha ndio dizain zile za kutoka na taulo uwanjani kupiga mswaki na mitongotongo yako huku unasubiri foleni yako ya kuoga...poor you!
Acheni umbea wanaume