Tetesi: Machache aliyonieleza mfanyakazi wa TPA yana ukweli?

Tetesi: Machache aliyonieleza mfanyakazi wa TPA yana ukweli?

Mpaka siku akitokea Rais atakae nyonga watu kwenye hzo taasisi nyeti ndo tutaona ufanisi

Bila shaka hatuwez kumpata rais wa namna hyo maana kila rais anaeingia lazima alipe fadhila za waliomuweka kwahyo unakuta taasisi nyeti kama hzo kumejaa watoto wa waliomsaidia kukalia hicho kiti

Kwahyo suruhisho rahisi ni katiba mpya tu
Pole mkuu, umeongea kwa uchungu sana
 
Nchi hii ina IGA ngapi zilizo kazini muda huu?. Umezifahamu zote zilivyo kifungu kwa kifungu?. Kuna IGA nyingine mbili zinakuja hapo hapo bandarini mwezi ujao, unazifahaamu zipo vipi?.

Narudia kukwambia mwezi wa kumi tarehe za mwishoni hapo TPA panaanza kazi mpya kabisa ya uendeshaji, kama jamaa zako wanakula kwa kutegemea mifumo ya wizi na upigaji biashara yao ndio imekwisha rasmi.

Rais kusema anakaa kimya ni busara za kiuongozi alizoamua kutumia.
mkuu nimesikia tetesi kuwa kampuni ya Wahindi ya Adani ipo pale au ndio mmoja ya wawekezaji watakokua wanashindana na DPW
 
Je tukisema tuendelee kumuomba Mungu itakuwa ni idea ya uhaini?

Mungu pekee ndo anaweza kutuvusha kwenye hili
Hiki ndicho kinachofanyika..

Hawa kenge hawaelewi kitu. Wameteka bunge na mahakama. Unadhani next step ni wapi?

Obvious, ni ku - appeal mbele ya baba yetu aliye mbinguni na ndivyo ambavyo inafanyika..

Na tayari, hatua za kimbingu zimekwisha anza kuchukuliwa na kutekelezwa...
 
Wameanza kugeukana.
Wameanza kula nyama zao wenyewe
 
Binafsi nafanya kazi za bandali, nikijionea micontenar inayotoka na kuingia kila siku nasikitika kwanini inchi yetu haisongi mbele. Kunasiku supervisor mmoja alinambia kua, mzunguko wa siku hiyo ilikua contener Mia nane, akisema kua hiyo ni takwimu yakawaida, wakati mwingine zinafika hadi miatsa au elfu moja, na hiyo ni kwaupande mmoja tu ule aliokua amekodishiwa ticts.

Kumbuka pia na TPA Wana upande wao ambao pia mzunguko wake unazidiwa kma 40%. Na kumbuka kila contenar huacha pesa si chini ya milioni moja.
Bandari tunaiweza kuindesha ,tatizo nii viongozi wa Tanzania tu
 
Yuko sahihi kabisa ingawa hilo la bajeti kukata na kushindwa kuendelea kujiendesha sio kweli, serikali ina mifuko ya kifedha ya dharura kwenye changamoto hizo au kwa taasis zake.
Kuhusu ufanisi ni kweli, ziko taasisi za kizalendo na hapa ieleweke sio lazima haya makampuni yawe ya ndani ila umiliki ni wa watanzania, haya yanaweza kuleta tofauti ya kiundeshaji na kimapato.
Changamoto iliyopo tanzania ni kwamba kila mradi lazima kuna watu wanahitaji kufaidika nayo hata hao waarabu pamoja na ubora wao na ambao wanao na haki ya kupata hii tenda bado zimetumika njia haramu kuanzia utangazaji wa tenda mpka mchakato wa kupatikana mzabuni, hiyo sababu ni kupata chochote kitu kwa matumbo yao.
Mh Raisi ana mamlaka, pamoja na Bunge letu kukataa haya na bado naamini wana uwezo huo. La muhimu ni kukubali makosa na kurekebisha ki utu na sio kushupaza, naandika haya sababu hii changamoto ya leo na zilizopita zinatengeneza kizazi cha baadae kitakachokua na maamuzi ya ajabu iwe kwa maendeleo ama kuharibu maendeleo.
 
JPM hakufanikiwa lolote huko bandari, ufisadi haukuwahi kuisha TPA na ufanisi Bado ulikua chini sana.

Sijui why mnamuona JPM alikua perfect, hivi si ndio NIDA alitumbua weee mbona bado vitambulisho havitoki?

Wote Yale Yale tu
Naenda U tube andika aliyekuwa mfanyakazi WA Bandari afunguka mazito
 
Nikuulize, wewe umeijuaje familia yangu hadi ulizungumzie hapa.
Hili tu linakufanya uonekane kuwa mpuuzi.

Angalia ujuha wako: Eti "ni serikali yenyewe ndiyo inajua hasarra na faida inayopatikana bandarini"; wewe umezuiwa kujua kama hiyo bandari inafanya kazi kwa ufanisi au la?
Hapo ulipo hujui kwamba matatizo yaliyopo hapo hapo bandarini yanatokana na ubovu wa utendaji unaoanzia serikalini; hata hili hulijui?
Mimi najua serikali imeweka ruzuku kwenye mbolea ili mimi nimudu kuinunua kwa bei himilivu,mimi mkulima hapa ndiyo nimeguswa.Mimi najua serikali imetoa ajira nyingi za afya na elimu.Wadogo zangu na ndugu zangu wamepata ajira na kumeniondolea utegemewa niliokuwa nao kwa hawa wanandugu,hapa serikali imeyagusa maisha yangu.Haya ni baadhi tu kati ya mambo mengi ambayo serikali imefanya na inaendelea kufanya yanayo wagusa rai moja kwa moja.
Suala la Bandari ni suala la serikali moja kwa moja.Mimi rai nilishaunda hiyo serikali kupitia uchaguzi na wote waliopita katika uchaguzi ndiyo wawakirishi wangu katika masuala ya vitegauchumi vya serikali na mambo yote ya kiserikali.
Aisee!Mimi nina mambo mengi ya kushughulikia kuisaidia serikali katika kukuza uchumi.Mimi kuwa kwangu mkulima,mfanya biashara na muajiriwa,ni msaada tosha kwa serikali.
 
Mkuu 'KING KIGODA', umejitahidi sana kuigiza, na kwa sababu ya jitihada hiyo uliyofanya sitakujibu kwa dharau, ingawaje unastahili dharau kubwa katika haya uliyoandika hapa.

Ingekuwa kama siyo kuigiza, na ningeamini kuwa hayo baadhi ya uliyoyasema hapa ndio uelewa wako unaokuwezesha kuyajua, ningekuhurumia tu kwa kuendelea kuwa ndani ya ujinga.
Lakini najua siyo hivyo, wewe ni muigizaji.
Na ujinga mkubwa sana unaoshabihiana na upumbavu ni kuhusu haya uliyoandika hapa chini:
Suala la Bandari ni suala la serikali moja kwa moja.Mimi rai nilishaunda hiyo serikali kupitia uchaguzi na wote waliopita katika uchaguzi ndiyo wawakirishi wangu katika masuala ya vitegauchumi vya serikali na mambo yote ya kiserikali.
Aisee!Mimi nina mambo mengi ya kushughulikia kuisaidia serikali katika kukuza uchumi.Mimi kuwa kwangu mkulima,mfanya biashara na muajiriwa,ni msaada tosha kwa serikali.
Sina la ziada nawe, ila nashukuru kukufahamu wewe, na njia zako hizi za kipuuzi za kutetea uovu ndani ya nchi yetu.
 
Siyo kweli kwamba Watanzania hawana uwezo wa kuendesha bandari bali ufanisi hauonekani kwa sababu watawala wamekinga mirija yao bandarini.

Kama kipindi cha Maguful, Yule mama Mbunge mke wa Mkwere alitaka kuoitisha kontena kwa nguvu zikapigwa ban

Hali sasa hivi itakuaje??

Hizo pesa za wizi wanapeleka Asia maana Ulaya ya America watazikata kodi nusu yake

ASIA =AFRICA tofauti rangi ya ngozi tu
 
Naeleza kwa ufupi. Wenye kuelewa haraka hongereni.
  1. Bajeti ya Bandari inakata Sept 2023 ambapo kwa mujibu wake anasema kuanzia Oktoba TPA itakuwa ktk wakati mgumu kwenye kujiendesha
  2. DPW walipaswa kuanza shuguli bandarini mnamo Oktoba 2023. Lakini mpaka sasa seems deal halijafikia muafaka.
  3. Siyo kweli kwamba Watanzania hawana uwezo wa kuendesha bandari bali ufanisi hauonekani kwa sababu watawala wamekinga mirija yao bandarini.
  4. Endapo serikali ingeunda mamlaka inayojiendesha kibiashara kusimamia bandari na kuwepo nanusimamizi wa kizalendo, bandari zetu zingeweza kuleta tija mara kumi zaidi ya kinachotarajiwa kuletwa na DPW
Najua humu JF wapo wenye kuyaelewa haya mambo yanavyokwenda, je hizi taarifa zimekaaje?
Suala la kusema bajeti ya TPA inakata ctober ili sikubaliani nalo ata kidogo
 
Suala la kusema bajeti ya TPA inakata ctober ili sikubaliani nalo ata kidogo
Hiyo ni mkakati WA mafisudi Ku lazimisha mambo kwamba hakuna hela na meli zipo hapo , hivyo ilikuwa lazima DP weldi aingie au yeyote wanayemtaka wahusika
 
Utasubiri wazalendo miaka 100 ijayo na hautawapata
Nchi imejaa wapigaji na wapigaji ni sisi wenyewe
Ufanisi utoke wapi wakati mtu anaomba kazi sehemu sio kwamba akaongeza uchumi wetu bali anawaza kuiba na kama ni kiongozi anahakikisha mwanae anaingia sehemu za wala rushwa sana

Bandari hakuna anaeiweza maana kuna ulaji na inapitisha bidhaa nyingi sana
Hizo meli kila siku zinaleta vitu na hivyo vitu ni wafanyabiashara na taasisi kama hizi ambazo kwa ukiherehere wanavimba na kusema usiguse hizo zina msamaha wa Kodi na hapo ndio madudu yote yanapitishwa na hao so called wazalendo

Siku ukiona unapita na kuwapa masikini barabarani hela au unaona mtu binafsi hata awe na cheo kwenye dini anapeleka mikate yeye kama yeye hospitali na kuwapa wagonjwa

Basi siku hiyo ujue neema inaingia nchini bila hivyo sahau kuna majizi tu
 
Back
Top Bottom