Ninawaelewa sana wenye mawazo kama haya uliyowasilisha hapa, ila huwa nashindwa kabisa huwa hamuendi mbele zaidi na kutaja tatizo la haya yote hasa ni nini?
Hivi serikali zetu hizi na viongozi wao, wao hufanya kazi zao vizuri sana kiasi kwamba huko hatuwezi kuhimiza wawepo wawekezaji ili tupate ufanisi mkubwa huko pia?
Ninavyojua mimi, matatizo yote ya akina TPA, TRA na wengineo chimbuko lake ni huko huko serikalini, kama ulivyogusia mwenyewe.
Mimi nashindwa kabisa kuelewa, inakuwaje mwekezaji afanye kwa ufanisi, kwa msukumo wa kupata faida; lakini mtu wetu mwenyewe, mzalendo wa nchi hii yeye awe ni mtu wa kuharibu tu?
Kwa kweli somo hili hapa huwa silielewi kabisa.
Labda siku moja italazimu nitafute msaada wa 'brain transplant" toka kwa magwiji kama nyinyi, ili nami nipate kulielewa hili jambo vizuri zaidi.
Kwa mwendo huu mnaotupeleka sasa ni kwamba hakuna jambo hata moja tunaloweza kufanya kwa ufanisi sisi wenyewe, bila ya kuwategemea wawekezaji, na hasa hao toka nje!
Ni ajabu sana.