Tetesi: Machache aliyonieleza mfanyakazi wa TPA yana ukweli?

Tetesi: Machache aliyonieleza mfanyakazi wa TPA yana ukweli?

Mpaka sasa nyie watz mmeshashindwa mnataka mshindwe mara ngapi ndo mkubali hamuwezi? TPA inaendesha bandari zote tz Kwa mwezi analeta bilioni 700 na ajiendesha Kwa bilioni 600 so obviously Kwa mwezi anatengeneza faida ya bilioni Mia tu, sasa linganisha na tict kakodishwa gati moja tu lkn kila mwezi analeta faida ya bilioni Mia tatu, njoo Kwa DP world world anakuhakikishia kuwa bandari pekee ya dar atakuwa analeta faida tilioni 26 Kwa mwaka sasa unapingaje dili tamu hili ukiwa na akili timamu kisa wimbo wa uzalendo? Haya nyie wamutumbi mnaojisifu mnaweza kuendesha miradi yenu wenyewe hebu nambie kamradi kadogo tu kamwendokasi kanawatoa jasho kila siku mnasondeka watu na kuku, soko la abiria ni la uhakika kuongeza tu mabasi mmeshindwa kila siku abiria wanapiziana sababu ya mbanano.
Rais Samia aliwaomba mabalozi wakaulize nchi walioendelea walitumia uchawi gani...

Anauliza hilo wakati ripoti ya CAG kaifungia kabatini
 
Tukisema bandar akabiziwe DPW watu wanaona sisi sio wazalendo ngoja tuone octbr sio mbali
Mkuu punguza mawenge.
Bandari ni yetu. Tutaingia ubia na siyo kuitoa kwa hao jamaa wanaotaka kujimilikisha
 
Mimi naona huelewi ninachoeleza hapa.
Ubovu wa viongozi serikalini hauwezi kuwa ndiyo iwe sababu na kisingizio cha nchi kutoweza kufanya chochote na kusimamia maendeleo yake.
Kwa nini hutaki kuondoa ubovu huo ndani ya serikali?
Kwani serikali zinaundwa ili ziwe na viongozi wabovu, wala rushwa na wasiojali maendeleo ya nchi zao?

Mnazungumzia kibandari hicho hapo kana kwamba ni muujiza kabisa kuondoa takataka zote zilizopo hapo, kwa nini?
Kwa vile hao hao waliomo serikalini ndio wanaolea hali hiyo?
Kama ni hivyo, kwa nini hiyo serikali isibinafsishwe basi, si kubinafsisha ndilo suluhisho?
Hizi ni blah blah tupu. hiyo IGA ya DPW inaongelea juu ya kupandisha uwezo wa wafanyakazi wa sekta nzima ya usafiri wa majini, maana yake ni kwamba nguvu kazi yetu ya bandari bado ina uwezo mdogo na hili ni tatizo la afrika nzima.

Tunakuwa na ufundi mwingi wa kuongea lakini ile output yetu inakuwa ni sifuri kabisa.
 
Sababu ambayo huwa siikubali Hata kidogo.

Mtu anaibia, ni mwizi, na sheria za nchi zinazuia wizi na adhabu za ukigundulika umeiba zipo, bado unasema ukiharibu unahamishwa?

Tatizo ni usimamizi wa sheria 100% Hamtaki kufuata sheria, mnataka sheria zifuatwe na wananchi tu lakini "wananchi sana" wao wapete wasiguswe na sheria!! Hili tatizo mnalijua. Na halikubaliki!
Ni utamaduni wa serikali yetu kulinda wezi kwa kuwapa more chances kwa kuwahamisha hamisha
 
Hiyo ni IGA ambayo ni kifupisho cha mradi mzima kwa ufupi utakuwa vipi, project contracts zinazoandikwa muda huu ndio pana zenye kuhusisha kila kitu. IGA ina kurasa 32 lakini hizo consession na lease plan zinakuwa na kurasa mpaka 200.
Soma article 2 ya huu mkataba
Objective is to set legally set of framework to
1: develop
2: Improve
3: Manage
Ports in ocean and Lakes
Chawa mkibanwa kufafanua hii objective mnakimbilia oooh IGA mbona hili kusudi hamlisemi
 
Naeleza kwa ufupi. Wenye kuelewa haraka hongereni.
  1. Bajeti ya Bandari inakata Sept 2023 ambapo kwa mujibu wake anasema kuanzia Oktoba TPA itakuwa ktk wakati mgumu kwenye kujiendesha
  2. DPW walipaswa kuanza shuguli bandarini mnamo Oktoba 2023. Lakini mpaka sasa seems deal halijafikia muafaka.
  3. Siyo kweli kwamba Watanzania hawana uwezo wa kuendesha bandari bali ufanisi hauonekani kwa sababu watawala wamekinga mirija yao bandarini.
  4. Endapo serikali ingeunda mamlaka inayojiendesha kibiashara kusimamia bandari na kuwepo nanusimamizi wa kizalendo, bandari zetu zingeweza kuleta tija mara kumi zaidi ya kinachotarajiwa kuletwa na DPW
Najua humu JF wapo wenye kuyaelewa haya mambo yanavyokwenda, je hizi taarifa zimekaaje?
Kinachoniuma ni kwa nini tunaangalia kampuni za nje. Kuna matajiri watanzania wanaweza wakapewa tenda na wakasimamia vizuri. Hii ishu ya bandari ilibidi wapewe watanzania. Unampa mkataba mwarabu yeye mchango wake ni kukupa faida. Lakini ukimpa mtanzania atakupa faida na pesa ataiwekeza hapa nyumbani. Vilevile Mtanzania akiharibu ni rahisi kumkamata maana yupo hapa hapa nyumbani. Serikali yetu ina ulimbukeni unampa mchongo mhindi au mwarabu, anajua hapa sio nyumbani. Akipata hela anapeleka kwao, mwisho wa siku tunapungukiwa dola. Nimefanya biashara na wahindi na waarabu wao wanaishi kwa kujibana sana ili wawwekeze kwao.
 
Bajeti inakata vipi wakati wanauwezo wa kukusanya fedha za kutosha. Naona mnapima upepo humu. Shubamit [emoji3]
 
Hizi ni blah blah tupu. hiyo IGA ya DPW inaongelea juu ya kupandisha uwezo wa wafanyakazi wa sekta nzima ya usafiri wa majini, maana yake ni kwamba nguvu kazi yetu ya bandari bado ina uwezo mdogo na hili ni tatizo la afrika nzima.

Tunakuwa na ufundi mwingi wa kuongea lakini ile output yetu inakuwa ni sifuri kabisa.
Hiko kipengele siyo kibaya.

Eneo tata ni muda wa mkataba, status ya eneo la uwekezaji, fao la kujitoa na mkataba unasoma Tanzania lakini utekelezaji ni upande mmoja wa Muungano
 
Neno lako la chawa ulilotumia linaonyesha ni shabiki tu mwenye upande wake ambaye pia hana adabu kwenye maongezi.

Magati namba nane mpaka kumi na moja yatakuwa chini ya DPW, usitishwe na hayo yaliyoandikwa kwenye IGA atamiliki asilimia nane tu ya eneo zima la TPA.

Sisi watanganyika ni wazee wa blah blah nyingi lakini matendo yetu ni sifuri siku zote. Tunapopata kazi tunachokiweza ni kutengeneza michoro ya utapeli na wizi pamoja na kuanzisha makundi ya majungu yale ya kupigana vita.
Hacha kupotosha, ni sehemu ipo ya mkataba onaonesha hivyo
 
HHil

Hili suala siyo la kumuachia Mungu kwani lipo NDANI ya uwezo wetu
Tunafanyaje mkuu.

Kwa sasa tunakosoa huku tumeficha majina yetu. Tumeona kilichowapata waliotumia majukwaa kukosoa.

Wale wanaounga mkono huu uzwazwa wanaweka mabandiko huku wameambatanisha namba zao za simu🤣
 
Hii ndio point ya msingi watu tunazungumzia vipengele vyenye utata wajinga wamekazana kutuletea faida za huo mkataba sasa kama mkataba hauna ukomo hizo faida tutazipataje tutampimaje muwekezaji
Huu utata umekuwa ukifafanuliwa zaidi ya mara elfu moja. Tumepotoshwa kwa kulishwa kwa kina suala la mwarabu kutaka kututawala tena miaka hii ya 2020!, na wasomi wetu wamedanganyika na kuuingia huo mkenge.
 
Back
Top Bottom