Tetesi: Machache aliyonieleza mfanyakazi wa TPA yana ukweli?

Tetesi: Machache aliyonieleza mfanyakazi wa TPA yana ukweli?

Naeleza kwa ufupi. Wenye kuelewa haraka hongereni.
  1. Bajeti ya Bandari inakata Sept 2023 ambapo kwa mujibu wake anasema kuanzia Oktoba TPA itakuwa ktk wakati mgumu kwenye kujiendesha
  2. DPW walipaswa kuanza shuguli bandarini mnamo Oktoba 2023. Lakini mpaka sasa seems deal halijafikia muafaka.
  3. Siyo kweli kwamba Watanzania hawana uwezo wa kuendesha bandari bali ufanisi hauonekani kwa sababu watawala wamekinga mirija yao bandarini.
  4. Endapo serikali ingeunda mamlaka inayojiendesha kibiashara kusimamia bandari na kuwepo nanusimamizi wa kizalendo, bandari zetu zingeweza kuleta tija mara kumi zaidi ya kinachotarajiwa kuletwa na DPW
Najua humu JF wapo wenye kuyaelewa haya mambo yanavyokwenda, je hizi taarifa zimekaaje?
Ni kweli wamekinga mirija pale watawala. Hata Mimi siamini kwamba sisi hatuna uwezo wa kuendesha bandari. Ni ujinga na uzandiki unaendelezwa wa kuaminisha na kujianika kwamba sisi ni vilaza. No we can yes we can tatizo kubwa hatuna Rais mwenye high IQ.
 
Vyovyote iwavyo lakini siyo kigezo cha kuwapa wajomba kuendesha Bandari
Hapo hujatumia akili kabisa.Yaani kuna kikundi kinavuruga uendeshaji wa bandari halafu kwa dhana mbaya tu unataka mtu mwengine asiingie kuja kurekebisha kasoro hizo.Afadhali huyo mjomba angekwishaingia akaharibu ndipo ukasema maneno hayo ya hasira.
 
Tatizo ni mama Mwenyewe Wala SIO watanzania.

Hii nchi kamwe haiataacha kutafunwa kama tutakua na watu wabinafsi na wanaosimamia Mila na itikadi zao Badala za Katiba.

Yani akiingia mmanyema anaangalia Mila za kimanyema, akiingia Mzaramo anaangalia Mila za kizaramo Badala ya Katiba. Akiingia Mzanzibari au mtanganyika akataka ajikite kwenye ukanda wake Badala ya Katiba ya nchi. Mbaya zaidí CCM Imekua ikicheza mchezo mbaya zaudi Wa Udini Kila Wanapoona Wizi wao unaanza kuwachosha Wananchi.

Mfano karata anayetaka kuitumia Kikwete ni kuwachanginisha Wakristo kupitia madhahebu anayojua miaka yote hawalipendi kanisa la Roma ,Mfano Wasabato,na makanisa ya Mabepari na wakaloni Mambo Leo ya kimarekani yanayoendeshwa kifamilia na kukusanya Sadaka Kwa ajili ya kujilimbikizia Mali bila kutoa Mchango Wowote au huduma yoyote kwenye jamii.

Magufuli alikua na akili kubwa na Maono.
Chuki kubwa ya watu wachache sana ndiyo inayoliumiza taifa hili.

Kuelekea 2025 wapinzani walikua na nafasi kubwa sana ya kuchukua nchi Kwa asilimia kubwa sana.
Tatizo litakalowasumbua ni Kuwa na Vyama visivyo na Mrengo Wa kisiasa.
CCM ni Chama Cha kijamaa na katiba Yetu na Mila zetu na utamaduni WETU ni utamadunia unayoendana sana na ujamaa na kujitegemea .
Mwalimu alitumia nguvu kubwa sana kulinda Mila zetu ,umoja WETU na utamaduni WETU na hulka Yetu ya Ujamaa.
Tatizo wamejitokeza watawala wanaoendekeza ama Udini au biashara Zao na uroho Wa Mali . Yani kuanzia kipindi Fulani walijitokeza watawala wakaanza kuwagawa wanafunzi mashuleni kulingana na Dini zao Kwa kuvaa mavazi Tofauti. Mara zikaanza Taasisi za kudhaminiwa na Matajiri Wenye Dini Fulani kuanzisha benki zisizo na Riba Kwa watu Wa Dini Fulani,mara wakaanza kufadhili Taasisi za kuficha watoto misituni na kuwafundisha mambo ya kupigana na kupigania Dini. Mabiloni ya pesa yakaelekezwa mifukoni mwa watu. Baadae wakajitokeza watu wakapiga Kelele Kuwa hatuelekei kuzuri. Watawala wakakaa kimya na chama tawala. Watu wakaanza kumwagiwa Tindikali kule Zanzibar watawala wakakaa kimya . Zanzibar ni kaeneo kadogo watu wanajuana lakini hakuna aliyekamatwa. Kwa kuchoma makanisa moto Wala kumwagia mapadri Tindikali.
Kikwete akemee Dini zinazokaa kimya wakati watawala wanapokiuka Sheria na kuwaonea wanyonge kwenye utajiri aliouumba Mwenyezi MUNGU.

Nchi ni ya MUNGU,rasilimali ameziumba Mungu sio chama Cha Mapinduzi Wala Watawala na tamaa Zao. MUNGU ananungunikiwa na wanyonge kwenye nchi aliyoiumba na kuiwekea rasilimali nyingi Kwa sababu ya Wanasiasa waovu halafu eti viongozi Wa Dini wakae kimya.!!

Lakini walipoanza kusema CCM isichaguliwe kule Zanzibar ndipo walipokamatwa mashekhe na kupewa kesi ya ugaidi. Waliona CCM ikiondoka madarakani maslahi ya wale wanaotumika kupokea Mapesa machafu kupitia mipango Yao ya hovyo yatapotea.

Hii nchi Kuna watu wachache wanajilimbikizia Mali kutokana na harakati chafu sana na Kwa sababu wamejificha ndani ya Chama Cha Mapinduzi hawaguswi.

Haiwezekani bandari kubwa kama ya Dar es Salaam wapewe Waarabu kuja kuiendesha Chini ya Serikali ya wezi waliojawa na Udini ,uchama na ubinafsi mkubwa halafu ifanye Vizuri . Ni ndoto ya alinacha . Kinachofanyika ni Wezi waliochota pesa za umma kuungana na DPW kujiuzia bandari Kwa mgongo Wa Nyuma.

Hivi kama Mwarabu Chini ya mkataba huo mbovu na utawala mbovu Chini ya Chama kibovu na TRA yenye utendaji mbovu na TPA mbovu akishindwa kuleta tija atafanywaje.?
Yaani Waarabu wanaotuibia wanyama na kufanya njama kumiliki nchi ya Loliondo ndani ya Tanganyika Leo wamegeuka na Kuwa na Huruma ya kutukuaanyia pesa za bandari yetu Kisha watupe tupate maendeleo tusomeshe watoto WETU wapate utaalamu mkubwa na tuwe na jeshi kubwa na imara ,na teknolojia kubwa na maendeleo makubwa ,tuchimbe mafuta Yetu na gesi yetu na urenium Yetu Kisha tuchukue bandari Yetu tuimiliki na wao warudi Dubai Jangwani . Ni kichaa pekee aliyechanganyikiwa na kubaki kama Nabii Tito anaxeweza kuamini Kuwa DPW watatuletea maendeleo.
Kwanza hawatamuogopa MTU yeyote Kwa sababu Hana Cha kuwafanya na Hana mamlaka ya kuwafanya Chochote.
Magufuli aliogopwa mana alikua anaweza kumfanya MTU Chochote.

Hawa Hata Wakiiba hakuna MTU atawakamata Wala Kufunga Akaunti zao Wala kuwafungulia kesi za uhujumu uchumi Wala kuwanyanganya Mali zao Wala kutengua uteuzi wao.
Kifupi Kwa Serikali ya chama Cha Mapinduzi ni Bora tuendelee kuendesha bandari Yetu mana angalau akijakutokea Magufuli Mwingine basi atawatumbua Wezi na kuwaweka gerezani au Hata kutaigisha Mali za wale wasiotaka kubadilika . Angalau watu watakua waoga pale bandarini. Watanzania ni waoga lakini wakiona wenzao wanaiba na hawasemeshi Wala kutumbuliwa basi na wao Wanaiba. Na wakiona Kuwa kibali Cha kuiba ni shati la kijani basi wanavaa.

Bandari zetu wapewe watanzania Wenzetu . Wapewe Kwa mikataba inayobana wizi kuliko kupewa waarabu ambao hatutaweza kuwabana Kwa sababu mkataba umewapa heshima kubwa Kama miungu. Mbaya zaidí kuna watu wanawaona kama vile ni wakombozi Wa kidini na kiroho.

Bodi ya bandari iundwe na Majenerali Wa Jeshi la Wananchi Badala ya makada Wa CCM waliotumikia wizi Kwa miaka mingi na wanaendelea kuwaza pesa za Rushwa zipatikane wapate Mgao .

Ukimsikiliza Zito kabwa huwezi kuamini Kuwa Ana Miliki chama Cha kijamaa kifalisafa na kiimani Bali ni Muungano Wa fursa ya kuiba pamoja na CCM.
Pumbas
 
Shida ya Watanzania wengi wanapenda ujanja ujanja, hiyo bandari watunge sheria mpya ya mwaka 2023 za dharura,

ofisi ya CAG iwe na kambi hapo Auditing iwe ni kila siku 😂

Wezi, wabadhilifu adhabu iwe ni kunyongwa, kama mna huruma sana tutaajiri vijana kutoka mashariki ya mbali huko wameshajizira watusaidie zoezi la unyongaji, lazima nidhamu itarudi.

Mambo ya kuoneana aibu na kubebana ndio yanatuleta hapa, wewe nyonga watu tu uone kama kuna mtu atathubutu kuchezea pesa ya serikali.
 
Naeleza kwa ufupi. Wenye kuelewa haraka hongereni.
  1. Bajeti ya Bandari inakata Sept 2023 ambapo kwa mujibu wake anasema kuanzia Oktoba TPA itakuwa ktk wakati mgumu kwenye kujiendesha
  2. DPW walipaswa kuanza shuguli bandarini mnamo Oktoba 2023. Lakini mpaka sasa seems deal halijafikia muafaka.
  3. Siyo kweli kwamba Watanzania hawana uwezo wa kuendesha bandari bali ufanisi hauonekani kwa sababu watawala wamekinga mirija yao bandarini.
  4. Endapo serikali ingeunda mamlaka inayojiendesha kibiashara kusimamia bandari na kuwepo nanusimamizi wa kizalendo, bandari zetu zingeweza kuleta tija mara kumi zaidi ya kinachotarajiwa kuletwa na DPW
Najua humu JF wapo wenye kuyaelewa haya mambo yanavyokwenda, je hizi taarifa zimekaaje?
Nakubaliana kabisa, viongozi wengi wanamirija hapo, mim binafsi nakubaliana na Uwekezaji but not Mkataba wa DP kabisa. Maana kama mifumo haitatoa Uhuru kwa wazawa kujiendesha kibiashara bila kuwaingilia, wangeweza... Ila naamini vimemo haviezi Isha... Bora aje mwekezaji angalia sura ya Mtu yeye kazi na pesa
 
Kama njia ya kuingia barabarani imeshindikana kwanini isitafutwe njia nyengine yenye kuwezekana? Ina maana tutaendelea kukaa tu na kusema watanzania waoga hatuwezi kuingia barabarani?
Njia nyingine ndiyo hiyo mkuu 'Tz mbongo' niliyoielezea hapo kwa ufupi, yaani kupitia kwenye chaguzi hizi zinazokuja 2024 na 2025.
Inajulikana kwamba kuna waTanzania wasiopenda kuchezewa kura zao wakati wa uchaguzi, na ushahidi huo upo wakati ule CHADEMA walipopata wabunge wengi Bungeni nchi nzima. Watu walikataa kabisa hujuma walizojaribu kuzifanya CCM kuwazuia.

Kwa hili tunajua linawezekana; na CCM waking'ang'ania maana yake ni wao watakuwa wanaanzisha vurugu nchini, na siyo CHADEMA.
 
Tusiruhusu akili zetu kuchoka namna hiyo.

Tukubali kwamba kuitoa CCM ni mchakato kama ilivyojichakata kujisimika kwenye veins za serikali.

Tukubali kuwa, siyo kila mabadiliko kwamba ni lazima tuyashuhudie kwa macho yetu bali tukubali kuwa msingi wa mchakato wa kuipumzisha CCM.

Jambo la kufanya ni kusimika uzalendo kwa wenetu. Tuwaeleze ukweli na watuone tunaishi kwenye huo ili wakija kutupokea wajue adui namba moja wa Tanzania ni mfumo mbovu wa CCM

Narudia tena, kuendelea kusimama kwenye mstari wa kura eti unachagua kiongozi ni utani wa mchana kweupe. Ni aidha machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi ili kuondokana na hiki chama kilichoko madarakani kwa shuruti.
 
Je tukisema tuendelee kumuomba Mungu itakuwa ni idea ya uhaini?

Mungu pekee ndo anaweza kutuvusha kwenye hili
Huyo Mungu hayupo.

Matatizo yalitengenezwa na Binadamu mwenyewe, Yata tatuliwa na binadamu huyo huyo.

Haya mambo ndio yana kwamisha waafrika, matatizo mnatengeneza wenyewe, Halafu mnadhani kuna nguvu isiyo kuwepo itakuja kuwatatulia matatizo yenu.

Huko ni kujifariji Fictions.
 
Ninachokiona huku Kilombero kwenye bonde la mpunga,ni kuongezeka kwa viwanda vya kuchakata mpunga na ungezeko la maghala ya kuhifadhia mpunga kila kona.
Utitiri wa majengo mapya kutoka kwa wakulima tena wakiezeka nyumba zao kwa Bati za rangi a.k.a msauz.Yaani ne Bandari halisikiki kabisa zaidi ya kwenye ofisi za umma na mitandaoni.
Kifupi Sa100 na CCM yake hawana wa kutoa madarakani hivi karibuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni mwongo.

Hujaeleza chochote kama hao watu wanaofanya hayo unayodai wanayafanya ni kwa sababu ya Samia.
Umewauliza wakakwambia hawataki wawe na bandari yao ya Dar es Salaam?

Kwa hiyo kwa akili zako finyu, kwa wao kutokuwa na habari juu ya DP World ni sawa na kukubaliana na upumbavu unaofanywa na Samia na genge lake?

Umewauliza wakakwambia wao hawaoni tatizo lolote juu ya mkataba huo?

Hopeless Kabisa!
 
Narudia tena, kuendelea kusimama kwenye mstari wa kura eti unachagua kiongozi ni utani wa mchana kweupe. Ni aidha machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi ili kuondokana na hiki chama kilichoko madarakani kwa shuruti.
Na huo ndio ukweli unfortunately
 
Ninawaelewa sana wenye mawazo kama haya uliyowasilisha hapa, ila huwa nashindwa kabisa huwa hamuendi mbele zaidi na kutaja tatizo la haya yote hasa ni nini?

Hivi serikali zetu hizi na viongozi wao, wao hufanya kazi zao vizuri sana kiasi kwamba huko hatuwezi kuhimiza wawepo wawekezaji ili tupate ufanisi mkubwa huko pia?

Ninavyojua mimi, matatizo yote ya akina TPA, TRA na wengineo chimbuko lake ni huko huko serikalini, kama ulivyogusia mwenyewe.

Mimi nashindwa kabisa kuelewa, inakuwaje mwekezaji afanye kwa ufanisi, kwa msukumo wa kupata faida; lakini mtu wetu mwenyewe, mzalendo wa nchi hii yeye awe ni mtu wa kuharibu tu?
Kwa kweli somo hili hapa huwa silielewi kabisa.
Labda siku moja italazimu nitafute msaada wa 'brain transplant" toka kwa magwiji kama nyinyi, ili nami nipate kulielewa hili jambo vizuri zaidi.

Kwa mwendo huu mnaotupeleka sasa ni kwamba hakuna jambo hata moja tunaloweza kufanya kwa ufanisi sisi wenyewe, bila ya kuwategemea wawekezaji, na hasa hao toka nje!

Ni ajabu sana.
Nenda kasome private enterprise over public enterprises nadhani utaelewa mantiki yake!! Iko hivi ni nature kabisa ya public enterprises kuwa inefficient over private enterprise so hata aje malaika kuongoza hawezi kuondoa inefficient on public enterprises sababu ndo asili ya huo mfumo.
 
Sina muda wa kwenda kusoma nadharia huku uhalisia ukiwa wazi.
Na hata hizo nadharia mnazolazimisha hapa, ni kama hamuelewi kinachozungumziwa humo ndani, badala yake mnaleta kupindisha tu kila kitu.
Nipe mfano mmoja tu wa nchi iliyoendelea kwa kuwategemea tu 'private sector' bila ya uhusika wa 'public sector'.
 
Kitendo cha DP world kuchukua njia zote kuu za kuiuchumi yafuatayo yatatokea:

1. Ukifika wakati wa uchaguzi mkuu watahakikisha Rais lazima atoke upande wanaoutaka wao na mtu anayemtaka yeye.

2. Wakati wa uchaguzi mkuu watamwaga fedha Walizozichukua hapa hapa nchi kuvuruga uchaguzi Ili kumpata wanayemtaka.

3. CCM na DP world watakuwa wameingia ndoa ya kudumu hivyo mapato ya nchi yatakuwa yanamulikiwa na kutumika wanavyo Taka Hawa wawili.

4. DP world ina udini mkubwa kuliko CCM inavyo sema suala la kuepuka udini.

5. DP world itaingiza utawala wa kidini na ukitizama Lile lidude limesainiwa na waislam watupu.

6. Mkataba wa DP world ufutwe na uondolewe Tanganyika.

6. Awamu ya pili mzee mwinyi alitaka kuingiza nchi OIC na kelele zikawa nyingi hilo likafutwa, sasa huyu bibi kaja kwa mbinu ile ile ya mzee mwinyi ila kajia kuuza kila kitu kwa waarabu.
Fear of unknown!
 
Naeleza kwa ufupi. Wenye kuelewa haraka hongereni.
  1. Bajeti ya Bandari inakata Sept 2023 ambapo kwa mujibu wake anasema kuanzia Oktoba TPA itakuwa ktk wakati mgumu kwenye kujiendesha
  2. DPW walipaswa kuanza shuguli bandarini mnamo Oktoba 2023. Lakini mpaka sasa seems deal halijafikia muafaka.
  3. Siyo kweli kwamba Watanzania hawana uwezo wa kuendesha bandari bali ufanisi hauonekani kwa sababu watawala wamekinga mirija yao bandarini.
  4. Endapo serikali ingeunda mamlaka inayojiendesha kibiashara kusimamia bandari na kuwepo nanusimamizi wa kizalendo, bandari zetu zingeweza kuleta tija mara kumi zaidi ya kinachotarajiwa kuletwa na DPW
Najua humu JF wapo wenye kuyaelewa haya mambo yanavyokwenda, je hizi taarifa zimekaaje?
Hiyo point namba 3 ndio adui mkubwa wa taifa hili, haya yote yanayoendelea muda huu chanzo chake ni upigaji wa hapo TPA. Maaskofu wanatumika pengine bila hata ya kujua wanafanya nini maskini ya Mungu.

Na huyu ni mwekezaji mmoja tu kati ya watatu wanaotakiwa kuanza kazi muda wowote kuanzia sasa. Suala lote limeingiziwa siasa za kipuuzi sana lakini wapo wafaidikaji wachache wa haya mambo.
 
Sina muda wa kwenda kusoma nadharia huku uhalisia ukiwa wazi.
Na hata hizo nadharia mnazolazimisha hapa, ni kama hamuelewi kinachozungumziwa humo ndani, badala yake mnaleta kupindisha tu kila kitu.
Nipe mfano mmoja tu wa nchi iliyoendelea kwa kuwategemea tu 'private sector' bila ya uhusika wa 'public sector'.
All developed countries zimefikia hapo Kwa kutoa kipaumbele Kwa private sector kuwa as the machinery for development, watanzania tunadharau theory ndomana tunafeli hata ktk shughuli binafsi za mtu mmoja mmoja, India pia wakati inaanza kubinafsisha mashirika yake ilipata upinzani mkali kutoka vyama siasa na wananchi wa kawaida wale waoga wa mabadiliko lkn mwisho wa siku walifanya na Leo hii wanainjoy maamuzi ya viongozi wao!!
 
Naeleza kwa ufupi. Wenye kuelewa haraka hongereni.
  1. Bajeti ya Bandari inakata Sept 2023 ambapo kwa mujibu wake anasema kuanzia Oktoba TPA itakuwa ktk wakati mgumu kwenye kujiendesha
  2. DPW walipaswa kuanza shuguli bandarini mnamo Oktoba 2023. Lakini mpaka sasa seems deal halijafikia muafaka.
  3. Siyo kweli kwamba Watanzania hawana uwezo wa kuendesha bandari bali ufanisi hauonekani kwa sababu watawala wamekinga mirija yao bandarini.
  4. Endapo serikali ingeunda mamlaka inayojiendesha kibiashara kusimamia bandari na kuwepo nanusimamizi wa kizalendo, bandari zetu zingeweza kuleta tija mara kumi zaidi ya kinachotarajiwa kuletwa na DPW
Najua humu JF wapo wenye kuyaelewa haya mambo yanavyokwenda, je hizi taarifa zimekaaje?
Point namba nne imekaa kisiasa zaidi, inaepuka ukweli kwamba kwenye suala la teknolojia hatupo vizuri hata kidogo.

Kuongelea uzalendo kwenye masuala ya bandari ni kuweka siasa za muda tu, kuna suala la teknolojia kuwa pana na kumilikiwa na wachache duniani, sio masuala mepesi kama yanavyoongelewa na Father Kitima.
 
Back
Top Bottom