Nidhamu ilikuwepo mkuu.
Siku magufuli anatangazwa Kuwa amefariki watu walihamishia matrioni majumbani mwao .
Alipoingia Samia akakuta hazina ni nyeupe wakamdamganya Kuwa JPM hakufanya Kitu.
Yule MTU aliifanya kazi kubwa sana .
Nilitofautiana Naye aliposhindwa kuzuga Hata kumpa pole Tundu Lisu. Na kuvuruga uchaguzi na kuibeba CCM . Kuibeba CCM Ilikua ni Kama kumlaza mtoto mchanga kwenye Chumba chenye Siafu.
Lakini mambo Mengi JPM alikua Yuko Sahihi sana.
Nchi hii haihitaji mjomba kuja kuendeleza zaidi ya kupata Rais mwenye ujasiri na roho ngumu ya kuiua CCM na kuwaacha Wezi wapambane na Hali zao.
Bandari na miundombinu mingi Ilikua inawekwa Vizuri Ili uanze kukusanya pesa Kwa Kasi.
Hivi umewahi kujiuliza pesa zinazokusanywa kwenye mizani Kila MAHALI, masoko, Stendi Kila Halmashauri, vituo vya mafuta, Nyumba Asilimia kubwa katikati ya miji ni za NHC. Pesa karibu asilimia 60 mpaka 70 zinaishia mifukoni Kwa watu . Hivi Soko kama la kariakoo linapataje hasara. Stendi Kama ya Mbezi inapataje hasara? Shirika la Nyumba linapataje hasara, bandari inapataje hasara?
Watu wanajiunganishia bomba la mafuta kuelekea majumbani mwao halafu wanabembelezwa Badala ya kuzsmishwa kwenye kisima cha mafuta na kutiwa kiberiti.
Watanzania watapataje ajira Kwa Mwarabu wakati wametangaziwa Kwa Wazi Kuwa sio waaminifu ,ni Wezi na wasiojituma!! ?
Watu Kama Hao Kwa nini wasinyooshwe kwanza Kwa miaka 20 Ili wabadikike kwanza ndipo waendane na Kasi ya utendaji Wa Dunia unaohitaji watu waadilifu. CCM mpaka Karne hii Bado Wanaweka watu Wa kuchota pesa za kampeni kwenye mashirika ya umma na Kisha Kurudi madarakani kuiba Tena.
Mfano tu Yule Aliyeiba pesa za Benki ya Walimu alipata uteuzi Badala ya kufungwa halafu utegemee banki ile iweze kuwanufaisha walimu?
Pesa za Tasaff ni wizi mtupu lakini ndio bajeti yake inaongezwa baadala ya kunyoosha kwanza wezi na kuwafunga gerezani Ili anayeingia upya awe muoga na Kuwa mwadilifu .
Tabia zinatengwa na jamii kulingana na mazingira . Wizi ukizidi Lazima pawe na hatua Kali na SIO kubembelezana Kama Yule Mkurugenzi Wa maje alivochukizwa na Mafisadi wanaoletea vimemo mezani halafu waziri anawalamba Miguu . Ingekua Mimi ningempiga Chini waziri nimpe yule Dada kazi mana anaonekana kukerwa na Uovu unaorudisha Nyuma maendeleo ya watu.