Tetesi: Machache aliyonieleza mfanyakazi wa TPA yana ukweli?

Tetesi: Machache aliyonieleza mfanyakazi wa TPA yana ukweli?

Mafisadi in terms of rushwa maana unaelewa urasimu uliopo. Hata mizigo huwa inapotea sana mazingira ya kutatanisha.

Kingine ufanisi wao upo chini sana na serikali pia CAG amekiri wameshindwa kazi. Sasa solution ni kufanya outsourcing tu maana hata ukibadili wafanyakazi wanaokuja ni Wezi zaidi.

Cha ajabu watu wanakazania ooh bandari itauzwa wanasahau hata sahivi haijauzwa ila Kuna mafisadi machache yanakula hiko hiko kidogo kinachopatikana
1) Kuhusu rushwa sina hakika na hilo. kwa sababu hakuna mahali unatakiwa kulipa kwa cash.
2) Kuhusu mizigo kupotea, hii iliwa hapo awali, kwa sasa kuna ulinzi wa kutosha na kamera (cctv), zimewekwa bandari nzima
3) Kwa sasa ufanisi umeongezeka sana baada ya JPM kununua vifaa vipya vya kisasa, na matengenezo ya Gati na kina cha bahari. Ndio maana TPA wamepokea tunzo hivi karibuni kwa kuingizia serikali pesa kwa mashirika ya umma.
3) Out sourcing sio jibu sahihi. Bado hatujashindwa. Ndio kwanza matengenezo yanakaribia kukamilika. Tuwape japo miaka miwili tuangalie uelekeo.
4) Kuhusu mafisadi kula hicho hicho kidogo - Watakuwa watu wa Hazina/Serikali.... TPA hawakusanyi mapato.
 
Sio kweli hili, bajeti huandaliwa mapema kulingana na makadirio ya Mapato na huidhinishwa, Sasa kivipi pesa ikosekane? Huwa Wana miradi hewa kibao ndio inakula Hela Wala shida Yao sio vifaa ila wizi tu. Unakumbuka kesi ya flow meter kuzimwa? Au Makinikia kusafirishwa bila kukaguliwa kama kilichokua delcared kwenye karatasi ndio kipo ndani ya container?

TPA are bunch of embezzlers, hiyo bandari mara 10 wapewe hata JWTZ pengine tutaona Mapato yakipaa ila hao TPA Are shit.
Sasa kama bajeti inaandaliwa mapema, kwaninin serikali haitoi pesa kwa ajili ya kununa vifaa? ...
Hata wakipewa JWTZ...... serikali ndio inakusanya mapato kupitia Control namba.
 
JPM alifanya trip kadhaa pale bandarini mara baada tu ya kuingia madarakani. Haikuwa kazi rahisi kuikata ile mirija pale.

Huyu mama ameingia madarakani akaanza kuwachekea hao wezi akidhani JPM alikuwa kichaa kuwanyoosha.

Sasa anadhani DPW watafanya nini? Shida ni yeye, amekuta mifumo imara kaamua kuibomoa kwa ushauri mbovu aliopewa na hao wezi waliotega mirija yao hapo.

As long as anaongoza nchi kwa kulipa fadhila kwa maswahiba asahau kuhusu ufanisi. Kwanini alimwondoa Kakoko pale? Nani alimshauri? Arejee hatua zake nyuma atawajua wabaya wake.
Na hana uwezo wa kurejea huko kwa sababu hana uwezo wa kufanya maamuzi
 
CCM haitegemei kura kukaa madarakani, ni aidha tuingie kwenye machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi
Tusiruhusu akili zetu kuchoka namna hiyo.

Tukubali kwamba kuitoa CCM ni mchakato kama ilivyojichakata kujisimika kwenye veins za serikali.

Tukubali kuwa, siyo kila mabadiliko kwamba ni lazima tuyashuhudie kwa macho yetu bali tukubali kuwa msingi wa mchakato wa kuipumzisha CCM.

Jambo la kufanya ni kusimika uzalendo kwa wenetu. Tuwaeleze ukweli na watuone tunaishi kwenye huo ili wakija kutupokea wajue adui namba moja wa Tanzania ni mfumo mbovu wa CCM
 
Shida kubwa kwa Tanzania ni kuwapata hao wa kwenda barabarani.

Isingekuwa hivyo, nami ningesema tuanze kesho.

Lakini kwa 2024/2025, nasema kama CCM itabaki kuendelea madarakani kwa njia yoyote ile, huo utakuwa ni muujiza wa kipekee sana.
Ninachokiona huku Kilombero kwenye bonde la mpunga,ni kuongezeka kwa viwanda vya kuchakata mpunga na ungezeko la maghala ya kuhifadhia mpunga kila kona.
Utitiri wa majengo mapya kutoka kwa wakulima tena wakiezeka nyumba zao kwa Bati za rangi a.k.a msauz.Yaani ne Bandari halisikiki kabisa zaidi ya kwenye ofisi za umma na mitandaoni.
Kifupi Sa100 na CCM yake hawana wa kutoa madarakani hivi karibuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwangu mimi nilivyosikiliza maelezo ya wataalamu nauona unafaa, lakini sina ufahamu sana wa Biashara ya Bandari wala ujuzi wa sheria za kimataifa, lakini vipo vitu watu naona wanapotosha makusudi kwa wwnaopinga, mfano mtu anasema bandari imeuzwa kivipi?

Haki za ardhi atapewa bure kivipi sababu hata raia wewe leo ukipewa hati ya eneo ni unakodi kwa miaka 99, inshort baada ya miaka hiyo serikali ina haki ya kuja kuwaeleza watoto wako au wajukuu zako hili eneo wanalihitaji sababu hukuuziwa ulikodishwa, lakini jambo jengine ninalofahamu mtu hawezi kutaka kuleta pesa zake na resources zake afu akupe masharti mepesi
Watu wanasema bandari imeuzwa kwasababu kwenye huo mkataba hakuna sehemu panapo onyesho ukomo wa mkataba pia kwenye sehemu ya sahihi hapaonyeshi jina la mtu au cheo chake kuna sahihi tu, sasa huyo mwenye hiyo sahihi ni nani? amabaye serikali yetu imeingia mkataba nae kwanini jina lake halipo kwanini ajifiche kama ni mwakilishi wa DPW ?
 
Naeleza kwa ufupi. Wenye kuelewa haraka hongereni.
  1. Bajeti ya Bandari inakata Sept 2023 ambapo kwa mujibu wake anasema kuanzia Oktoba TPA itakuwa ktk wakati mgumu kwenye kujiendesha
  2. DPW walipaswa kuanza shuguli bandarini mnamo Oktoba 2023. Lakini mpaka sasa seems deal halijafikia muafaka.
  3. Siyo kweli kwamba Watanzania hawana uwezo wa kuendesha bandari bali ufanisi hauonekani kwa sababu watawala wamekinga mirija yao bandarini.
  4. Endapo serikali ingeunda mamlaka inayojiendesha kibiashara kusimamia bandari na kuwepo nanusimamizi wa kizalendo, bandari zetu zingeweza kuleta tija mara kumi zaidi ya kinachotarajiwa kuletwa na DPW
Najua humu JF wapo wenye kuyaelewa haya mambo yanavyokwenda, je hizi taarifa zimekaaje?
Mfumo wa ccm tayari umekuwa kama ukoo wa mafisi, kambale au sangara!
Wanakula kila kitu hadi wao wenyewe!!
Cannibalism is real within ccm.
 
HAPANA, 2025 mbali ,watakuwa wameuza Kila ki2,

Tuungane na Nabii Mwabukusi kupeleka mashtaka mahakama ya umma iliyo juu ya zote, mabarabarani na Viwanjani Ili waovu watokomee!!
Tulia mkuu 2025 hatufiki," Nikungojapo chini shetani kaburini naenda" litapigwa Song
 
Hata mimi niliwatembelea kwenye banda lao pale sabasaba wanasema TPA haina shida ya ufanisi kwenye kupakua meli, ni janja janja tu ya wachache kutaka kufanya madili. Nchi hii kila kiongozi anayekuja akitaka kufanya dili kwenye rasilimali za nchi vizazi vinavyokuja vitakuta kitu kweli? maana watajikuta wanakaa kwenye ardhi ambayo ilishapigwa mnada kitambo.​
 
Back
Top Bottom