Watanzania tunajifanya wajuaji sana hata katika tusivyovijua, huu uzalendo tunaoutaka ushawahi kuua kiwanda cha Nyama cha Tanganyika Packers, tulimnyang’anya Mzungu aliyekuwa anaendesha kiwanda tukakiweka chini ya serikali ili tunufaike kikafeli baada ya Nyama za Tanzania kushindwa kununuliwa kwenye soko la dunia, Kumbe tuliyemtimua ndo aliyekuwa ameshika soko la Nyama huko Duniani.
Dunia ya Sasa ni ya Ubepari na ubepari upo kuanzia maisha yetu ya kila siku, unaajiri mfanyakazi anazalisha milioni nyingi ila unampa kiduchu ya anacho zalisha, Mindset zetu zinatakiwa kukomaa na kuondoa uoga wa jinsi ya ku survive kwenye dunia ya ubepari