Bexb
JF-Expert Member
- Oct 24, 2016
- 715
- 1,619
1. Budget zote za uendeshaji, manunuzi na nyinginezo katika taasisi za serikali hipangwa na kupitishwa katika bunge la bajeti. Amekadiriaje kuwa kuanzia wakati huo pesa haitakuwepo na ukizingatia shirika halihitaji ruzuku kujiendesha kwamba bandari inafungwa?Naeleza kwa ufupi. Wenye kuelewa haraka hongereni.
Najua humu JF wapo wenye kuyaelewa haya mambo yanavyokwenda, je hizi taarifa zimekaaje?
- Bajeti ya Bandari inakata Sept 2023 ambapo kwa mujibu wake anasema kuanzia Oktoba TPA itakuwa ktk wakati mgumu kwenye kujiendesha
- DPW walipaswa kuanza shuguli bandarini mnamo Oktoba 2023. Lakini mpaka sasa seems deal halijafikia muafaka.
- Siyo kweli kwamba Watanzania hawana uwezo wa kuendesha bandari bali ufanisi hauonekani kwa sababu watawala wamekinga mirija yao bandarini.
- Endapo serikali ingeunda mamlaka inayojiendesha kibiashara kusimamia bandari na kuwepo nanusimamizi wa kizalendo, bandari zetu zingeweza kuleta tija mara kumi zaidi ya kinachotarajiwa kuletwa na DPW
2. Ni ngumu sana kwa DPE kuwa ingeanza shughuli mwaka huu hata kama kila kitu kingekua smooth. Handling and passing over activities za bandari sio kama kuuziana dalaala kuwa ukiuziana leo basi kesho utaanzakuamsha asbuhi kubeba abiria. Atupe timeframe iliyosema DPW angeanza kazi October.
3. Hili fuatilia mwenyewe utaujua ukweli. Kama wafanyakazi wa bandari ni mafisadi na wezi ama hao unaoita viongozi ndio mafisadi wa bandari utapata jibu.
4. Mkuu kuwa na bandari pekee sio kigezo cha mtu kupitishia mizigo katika bandari yako na ndio maana kuna masuala mengi ya kibiashara yanayoamua watu wapitie kwako. Hii ni debate tena kubwa tu na sio kwa tuhuma ndogo ama slight accusations kama hizi.
Mkuu kila mtu amekua akiongea lake kuhusu bandari na kama ilivyo kawaida ya majungu kila anayelipata analifanya ku'amplify hivyo kupoteza uhalisia wa mpika majungu wa mwanzo na wa mwisho.
Katika hili suala watu tunapaswa kusoma sanaaaa na kuchimba sana maandiko ya wataalamu katika PORT BUSINESS ili tuuelewe ukweli lakini kama kawaida yetu sisi watanzania ni wavivu kusoma na tunapenda kusimuliwa zaidi kuliko kusoma na siwezi kushangaa kukuta mtu anapondea ile IGA lakini ukimuuliza kama umesoma mkataba husika kwa niliokutana nao ni 80% hawakuusoma waliishia kupata clips na kusimuliwa.
Tunapaswa kutumia akili yetu kwanza kabla hatujatoka nje kutafuta msaada lakini tutafute uhalisia kwa neutral party tunaweza kuokota lolote