Machache yaliyoonekana Simba ikishinda dakika za jioni dhidi ya CS Sfaxien

Machache yaliyoonekana Simba ikishinda dakika za jioni dhidi ya CS Sfaxien

kalisheshe

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2020
Posts
2,064
Reaction score
4,056
1. Nafasi ya kiungo mshambuliaji no. 10 imeendelea kuwa ni tatizo kwa Simba, ni aibu timu kama Azam ina Feitoto halafu Simba haina mtu wa maana nafasi ile.

2. Simba inatakiwa ifanyie kazi eneo la pumzi kwa wachezaji , mara nyingi inataka kuanzia dk ya 60 nakuendelea.

3. Yusuph Kagoma ni kiungo mkabaji sahihi kwa timu ya Simba
Kama angeanza naamini angekua man of the match.

3. Inawezekana kocha hajajua stability na weakness za wachezaji wake, refer wanavyorudia kufanya makosa yaleyale, na substitution zake.

4. Che fondor Malone apunguze kujiamini kupitiliza, makosa madogo madogo yanaweza kusababisha kelele za mashabiki zimuondoe mchezoni.

5. Iangaliwe namna Valente Nouma acheze kama winga, kwani amewazidi vingi mawinga waliopo simba.

6. Kinachoigharimu Na kitakachoendelea kuigharimu Simba ni eneo la kiungo no. 10 pamoja na winga zote mbili 7 na 11 kwani hakuna wachezaji wa maana wa kucheza nafasi hizo. Kama ndio mfumo wa kocha basi umefeli ajaribu mwingine.

Soma Pia: Full Time: Simba SC 2-1 CS Sfaxien | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa National Stadium | Disemba 15,2024

Kiujumla Simba haijacheza vizuri kimfumo ila ni juhudi binafsi za wachezaji kulazimisha matokeo dakika za mwisho.
 
IMG-20241215-WA0037.jpg
 
Hakunaga cha dkk za jioni wala nn, Ishu n ushindi tuu.
Kwan team ikishinda hizo dkk za jion wanapewa point ngapi na wakishinda dkk za mwanzoni wanapewa point ngap
Kinachoangaliwa na team kucheza vizuri na kumaliza biashara mapema

Imagine pressure wanayokuwa nayo mashabiki team inapokua haijashinda na mchezo unaelekea kuisha.
 
Kinachoangaliwa na team kucheza vizuri na kumaliza biashara mapema

Imagine pressure wanayokuwa nayo mashabiki team inapokua haijashinda na mchezo unaelekea kuisha.
Kwahy kupata ushindi wa jion sio kucheza vzr?
 
Michuano kama hii hatuangali kucheza vzur af ukose points, cheza tupate matokeo kama al hilal anavyowanyosha lile kundi hvyo ndivyo tunavyocheza club bingwa sio unacheza vzur af unaishia kukosa matokeo hi sio league, ushaur mzur tutaufanyia kazi kule NBC premeir
 
🤣🤣🤣🤣
Mkuu mbona lakini kama vile uwanjani walikuwepo wanaume na sio wanawake?
Hao ni wanaume wenye tabia za kike
Huoni makelele wakati mashindano yenyewe ya shirikisho
 
Back
Top Bottom