Machache yaliyoonekana Simba ikishinda dakika za jioni dhidi ya CS Sfaxien

Machache yaliyoonekana Simba ikishinda dakika za jioni dhidi ya CS Sfaxien

1. Nafasi ya kiungo mshambuliaji no. 10 imeendelea kuwa ni tatizo kwa Simba, ni aibu timu kama Azam ina Feitoto halafu Simba haina mtu wa maana nafasi ile.

2. Simba inatakiwa ifanyie kazi eneo la pumzi kwa wachezaji , mara nyingi inataka kuanzia dk ya 60 nakuendelea.

3. Yusuph Kagoma ni kiungo mkabaji sahihi kwa timu ya Simba
Kama angeanza naamini angekua man of the match.

3. Inawezekana kocha hajajua stability na weakness za wachezaji wake, refer wanavyorudia kufanya makosa yaleyale, na substitution zake.

4. Che fondor Malone apunguze kujiamini kupitiliza, makosa madogo madogo yanaweza kusababisha kelele za mashabiki zimuondoe mchezoni.

5. Iangaliwe namna Valente Nouma acheze kama winga, kwani amewazidi vingi mawinga waliopo simba.

6. Kinachoigharimu Na kitakachoendelea kuigharimu Simba ni eneo la kiungo no. 10 pamoja na winga zote mbili 7 na 11 kwani hakuna wachezaji wa maana wa kucheza nafasi hizo. Kama ndio mfumo wa kocha basi umefeli ajaribu mwingine.

Soma Pia: Full Time: Simba SC 2-1 CS Sfaxien | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa National Stadium | Disemba 15,2024

Kiujumla Simba haijacheza vizuri kimfumo ila ni juhudi binafsi za wachezaji kulazimisha matokeo dakika za mwisho.
Sahihi..ila kwenye hizi mechi kikubwa alama tatu na si kucheza vizuri.
 
Ondoa Mutale lete namba10 makini, Ondoa Ayubu weka Mpanzu,Ondoa KAZI au Duchu Lete beki wa Kati mzawa
 
Simba wanazingua sana sijajua kuna shida gani sio kwa wachezaji tu mpaka benchi la ufundi nalo linahitaji maombi.
1. Mohamed Huseini akaangalie marudio ya hiyo mechi hasa pale Nouma alipoingia. Atapata somo kubwa sana. Nouma amepiga krosi nyingi tena za hatari sana wakati amecheza muda mfupi kuliko muda alioutumia Mohamed Husein uwanjani. Huyo Mohamed Husein aache upuuzi wake wa kufika kwenye kibendera halafu anarudisha mpira nyuma wakati wakina Ateba wameshaingia kwenye boksi. Sawa yeye ni beki lakini pia timu ikishambulia anageuka kuwa winga anatakiwa alijue hilo..
2. Nimesoma mahali kuna mwandishi mmoja kamuita Mutale kuwa tapeli. Kweli huyo jamaa ni tapeli kabisa. Kwenye pre season na hata mechi ya Simba Day nilivyomuona Mutale nikajua hapo Simba kalamba dume kumbe alikuwa anaonyesha utapeli wake tu. Zaidi ya ile mechi ya Simba day kiukweli kabisa sijamuona Mutale tena akicheza vizuri hata mechi moja. Huyo Mutale wamuuze haraka au wamtoe kwa mkopo hastahili kuwepo Simba baada ya dirisha dogo kuisha Januari maana anafanya kazi kuubwa ili mwishoni sasa kituko. Na huo mpira wake wa anao anao na mbiombio sio aina ya mpira wa Simba. Pacha wake wa anao anao na mbiombio Kibu walau jana kapiga goli mbili kwa hiyo kidogo katoa gundu. Chasambi ni bora mara mia kuliko huyo Mutale. Magori na timu yako ya usajili muuzeni huyo Mutale haraka ili benchi la ufundi lisimuone maana linaonekana linampenda sana Mutale kuliko mchezaji mwingine yoyote.
3. Mkwala naye auzwe au atolewe kwa mkopo. Ana uwezo mdogo sana na hana utulivu mbele ya goli. Anajaza tu nafasi ya mchezaji wa kigeni pale Simba.
4. Che Malone anapita njia ile ile ya Inonga. Alianza vizuri sana msimu huu lakini ghafla kageuka faza. Anapenda sana kukaa na mipira bila hata sababu za msingi wakati yeye ni mtu wa mwisho. Mafowadi wa timu pinzani wameshamsoma kuwa akipigwa "ambush" anatoa mpira kirahisi sana.
5. Mavambo nafikiri kuna kitu hakipo sawa. Kazi kwenu uongozi na benchi la ufundi inabidi mkae naye chini mjue shida ni nini mkataba au maslahi. Au labda tusubiri tuone kwakua Kagoma karudi labda naye atarudi vizuri. Huyu Mavambo kwangu mimi nampa nafasi nyingine kwani mpira ana uweza ila sijui upepo mbaya umetokea wapi ukambeba
6. Benchi la ufundi nalo liache kupaniki. Hivi kweli unamtoa Ateba kwa kukosa tu magoli ya wazi halafu unamuingiza Mukwala. Hapo ndio mechi ilipozidi kuwa ngumu kwa Simba. Ateba aliyechoka ni bora zaidi kuliko Mukwala aliye fiti. Benchi la ufundi lijifunze namna ya kuwatuliza washambuliaji wakati mchezo unaendelea na kuwahamasisha wachezaji waongeze kasi. Waarabu waliupooza mchezo toka mwanzo badala ya Simba kuuchangamsha wapate goli za kutosha haraka haraka matokeo yake Simba wakaingia kwenye mchezo wa Waarabu na wao nao wakaanza kucheza taratibu huku muda unaenda. Mwishoni Simba wanakuja shtuka muda umeenda na hapo mechi ishakuwa ngumu kwani Waarabu walikuwa wanataka sare tu. Iwapo Simba wangelazimisha mpira uchezewe kwenye goli la waarabu tu ndani ya dakika 20 za mwanzo mchezo ungeishia pale pale lakini wao Simba wakaamua wacheze "square pass" kwenye goli lao. Hili kiufundi lilikuwa ni kosa kubwa sana na sijui kwanini benchi la ufundi halikuona hili tatizo.

Ni mtizamo tu
 
2. Simba inatakiwa ifanyie kazi eneo la pumzi kwa wachezaji , mara nyingi inakata kuanzia dk ya 60 nakuendelea.


Kiujumla Simba haijacheza vizuri kimfumo ila ni juhudi binafsi za wachezaji kulazimisha matokeo dakika za mwisho.
Kauli zinapingana
 
Back
Top Bottom