Machaguo ya Wanafunzi wanaojiunga Form 5 yapangwe mapema, mamlaka zinawaumiza Wazazi na walezi

Machaguo ya Wanafunzi wanaojiunga Form 5 yapangwe mapema, mamlaka zinawaumiza Wazazi na walezi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Naomba mamlaka zinazohusika kuchagua Wanafunzi kwenda kidato cha tano zote zitoe nafasi ya waliochaguliwa mapema ili kuwawezesha wazazi na walezi kufanya maandalizi ya kuwapelekea Watoto shule kwa utaratibu.

Machaguo yanapotoka mapema inampa fursa hata mzazi au mtoto kujipanga mapema kwa kujua shule husika, kama ni Serikali au mhusika ajipange kwenda Binafsi.

Mfano hawa wa safari hii wamemaliza form four Mwaka jana (2022) mwishoni, majibu yakatoka mwanzoni mwa mwaka 2023 kisha wanakuja kupata majibu ya walipochaguliwa Juni 2023 na kutakiwa kuanza kusoma Julai au Agosti 2023.

Ukiangalia hapo kati kuna nafasi ya kutosha ambayo kwanza naona si sawa kukaa muda wote huo mtaani lakini lwa kweli muda unaotolewa kwa sasa ni mfupi na ni kama adhabu kwa wazazi na Watoto kwa kuwa pia presha ya kumuandaa mwanafunzi wakati mwingine inakuwa kubwa hasa kama shule anayoenda kusoma ipo mbali na makazi ya wanaomsomesha.

Ujumbe huu uwafikie NECTA na TAMISEMI na Serikali kwa jumla.
 
Sisi TAMISEMI tushaanza kuwasikiliza,

unapendekeza hayo majina yawe yanatolewa lini?
 
Back
Top Bottom