Uchaguzi 2020 Machifu wa Makabila na kampeni

Uchaguzi 2020 Machifu wa Makabila na kampeni

Msulibasi

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
5,947
Reaction score
7,939
Nguvu ya machifu wa makabila mbalimbali imekuwa kubwa kipindi hiki cha kampeni. Kila mgombea anatamani abarikiwe na hawa Jamaa.

Nisichoelewa ni kama uchifu bado unatambulika kwa kiwango gani cha kisiasa kiserekali na kijamii.

Je, hawa jamaa wanaoonekana majukwaa ya kampeni ni machifu kweli wa makabila au ni wasanii.

Je, kabila linaweza kuamua au kuamuliwa na chifu liwe chama Fulani? Je Nyerere angalifurahi kuona uchifu ukienziwa kipindi Kama hiki cha uchaguzi.
 
Hawa machifu ni matapeli tu wa kisiasa.Nani asikilize ushauri wa kijinga wa kuchagua watu wanaotunyanyasa muda wote kupata haki zetu
 
Hawa machifu ni matapeli tu wa kisiasa.Nani asikilize ushauri wa kijinga wa kuchagua watu wanaotunyanyasa muda wote kupata haki zetu
Nimeona mgombea uraisi mmoja amewekeza Sana kwenye uchifu jambo ambalo mwalimu alitahadharisha.
 
Nyerere ni nabii, aliwafuta machifu kitambo

Angewaachia power machifu sasa hivi ingekuwa kilabukitaka kura za kabila fulani ni lazima ukubaliane na chief wao kwanza

Nyerere aliona mbali sana kama hawa watu watatusumbuwa baadaye akawaondolea nguvu na sasa hata wewe ukiamuwa unaweza kujiita chief tu kama Chief kiumbe.

Kule Nigeria uchifu unanuliwa, ukipiga pesa ndefu unakwenda kwa Igwe kununuwa tittle unapewa red cap na kuanzia hapo unakuwa na tittle ya kuitwa Chifu.

Hizi ni siku za mwisho hata Masheikh na maaskofu waangalie kwa makini wamebaki wachache mno wanaontumikia Mungu wa kweli.

Si unajuwa hata Q Chila ni Chifu pia?
 
😏😏😶😶😶😶😶😶🤨😑😗
 
[emoji57][emoji57][emoji55][emoji55][emoji55][emoji55][emoji55][emoji55][emoji2955][emoji58][emoji10]
Ukivaa kama mganga unakuwa chifu.

Anyway hotuba za mgombea mmoja zinaanza na salute za kabila. Anaamini Sana kwenye tamaduni.

Utasikia wagogo...... Wanyakyusa...... Wandali.......... Ila akifika usukumani hataji kabila ila anaswitch
 
Ana Switch External Language
😁😂😅😄😃
Huyu Baba, Mungu Anamuona!!!
 
Hawa machifu ni matapeli tu wa kisiasa.Nani asikilize ushauri wa kijinga wa kuchagua watu wanaotunyanyasa muda wote kupata haki zetu
Hakuna chama kinacho nyanyasa wanachama wake kama Chadema. Chama kimekuwa cha mtu mmoja na genge lake, tu hao ndo wenye kauli za mwisho. Mwenyekiti mpaka anavunja mguu, kisa vitu maalum.
 
Back
Top Bottom