Machimbo ya kupata mikopo rahisi kwa njia ya simu

Machimbo ya kupata mikopo rahisi kwa njia ya simu

cadnopoints

Member
Joined
Sep 14, 2019
Posts
65
Reaction score
59
Habari za Jumapili wakuu!

Napenda tujuzane mahali pa kupata mikopo kwa njia ya simu.

Binafsi nimekuwa mnufaika mzuri wa mifumo hii ya ukopeshaji kwa njia ya simu.

Nimekuwa mteja wa makampuni haya kwa muda sasa na kiukweli yanasaidia sana hasa unapokuwa na emergency.

Miongoni mwa makampuni/mashirika ninayoyatumia ni Branch International, L-pesa microfinance na TALA (hii haipo nchini kwa sasa).

Pia kuna huduma za mikopo kwenye mitandao ya simu kama vile M-Pawa, Songesha (Vodacom), Tigo Nivushe (Tigo)n.k

Huduma hizi ni nzuri na uhakika kikubwa ni uaminifu tu kwani mimi nimeweza kukopa na kufikia viwango vya juu.

Kama kuna anayejua chimbo lingine tujuzane.

Ahsanteni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom