Capt Tamar
JF-Expert Member
- Dec 15, 2011
- 12,340
- 16,383
Hahahaaa mimi niliwadaka hapa nanenane arusha kipindi hicho wale wachina ndio wanazipigia promo,ilikuwa sh 6000 kutolewa uchafu,walimrubuni mama yangu ambaye alinishawishi na mimi niende,nilikaa kwa muda kwanza nikiangalia wengine wakihudumiwa,machale yakanicheza,ila nikaona ngoja nihakikishe,nikalipa na kuwekewa maji kwanye karai,wakaweka na kile kiboya humo,nikaambiwa nikae kwa dk 25 hadi 30,wakaniacha hapo,sasa mimi nikaamua kuwloweka tu miguu yangu kwa sekunde kama mbili tu yani niliweka na kutoa,nikaacha kile kiboya kikiendelea kuchemka chenyewe na maji yakiendelea kuwa na rangi nzito nyekundu,mwisho nikaloweka tena kwa sekunde na kuitoa nikamwita mbongo aliyekuwa nao ili aniondolee,alipokuja nilimwuliza hiyo rangi nyekundu imetoka wapi akanijibu kuwa ndiyo uchafu uliovutwa kutoka mwilini mwangu!!nikamwuliza tena kama damu yangu haijapungua kutokana na hiyo iliyotoka na uchafu huo,akanijibu kuwa itakuwa imepungua kidogo sana!!! Nikajua hapo tutaliwa wengi mno.




