Machine za kutoa sumu mwilini

Machine za kutoa sumu mwilini

Hahahaaa mimi niliwadaka hapa nanenane arusha kipindi hicho wale wachina ndio wanazipigia promo,ilikuwa sh 6000 kutolewa uchafu,walimrubuni mama yangu ambaye alinishawishi na mimi niende,nilikaa kwa muda kwanza nikiangalia wengine wakihudumiwa,machale yakanicheza,ila nikaona ngoja nihakikishe,nikalipa na kuwekewa maji kwanye karai,wakaweka na kile kiboya humo,nikaambiwa nikae kwa dk 25 hadi 30,wakaniacha hapo,sasa mimi nikaamua kuwloweka tu miguu yangu kwa sekunde kama mbili tu yani niliweka na kutoa,nikaacha kile kiboya kikiendelea kuchemka chenyewe na maji yakiendelea kuwa na rangi nzito nyekundu,mwisho nikaloweka tena kwa sekunde na kuitoa nikamwita mbongo aliyekuwa nao ili aniondolee,alipokuja nilimwuliza hiyo rangi nyekundu imetoka wapi akanijibu kuwa ndiyo uchafu uliovutwa kutoka mwilini mwangu!!nikamwuliza tena kama damu yangu haijapungua kutokana na hiyo iliyotoka na uchafu huo,akanijibu kuwa itakuwa imepungua kidogo sana!!! Nikajua hapo tutaliwa wengi mno.
 
Kwanini hizi mashine hazipatikani kwenye hospitali kubwa?
 
This device is not recommended for persons with a pacemaker or any other battery-operated electrical device, organ treatment recipients, sufferers of epileptic seizures, pregnant women, nursing mothers, or children under 8 years old. Hypoglycemic persons or persons with low blood pressure should take appropriate medications prior to treatment sessions. Should you have any heart conditions, please consult doctors for advice.
 
Juzi kati wamekuja wataalam fulani mitaa yetu ambao wanatumia computer kujua magonjwa yako
nilishawishka kupima baada ya vipimo niliambiwa ni sumu kwenye, cholestroo na mzunguko wa damu haupo vizuri
walishauri kutoa sumu mashine wanipe dozi inayogharimu TZS 150,000.00
nilikubali kutoa sumu kwa machine ila sikuwa na hela kwa ajili ya dozi.
baada kufungwa machine yao nakuambiwa niweke miguu yangu kwenye dishi lenye maji.
maji yalikuwa masafi ila baada ya muda yalikuwa meusi nilikuwa 50% 50% kama ni kweli au si kweli kwa sumu iliwezaji kutoka wakati siku chomwa sindano wala kutobolewa sehemu ya mwili wangu yoyote au ni kweli mbona maji niliyashuhudia ni masafi na wahusika wanatambulika na TFDA.

kama ni kweli njia zipi naweza kuzitumia kutoa sumu na cholestroo mwilini? mzunguko wa damu nawezaje kuufanya uwe sawa?


wale wa weka picha
Photo-0047.jpg
maji yakiwa kwenye dishi kabla ya kufungwa machine na kuweka miguu
Photo-0075.jpg
baada ya kufungwa machine na kuweka miguu
Photo-0076.jpgPhoto-0077.jpgPhoto-0077.jpgPhoto-0078.jpg
baada ya kuwekwa miguu eti hii rangi nyeusi ndio sumu
 
....hizo picha umetumia simu ya mchina mbona hazionekani vizuri...
 
kupunguza sumu mwilini fanya yafuatayo:
Acha kutumia vinywaji vyenye sumu
Acha kutumia vyakula vyenye sumu
Acha kutumia tumbaku ya aina yeyote
Acha madawa ya kulevya
kunywa maji mengi kila siku (hii itaweka sawa mzunguko wa damu pia)
fanya mazoezi ya kukimbiakimbia/jogging (hii itaponya cholesterol pia)
 
Pole. Ukiona manyoya..................

Sent from my GT-P7500
 
SHAKE OFF PHYTO FIBER,
- Inaondoa tatizo la kukosa choo kwa haraka zaidi
- ni njia ya haraka iliyo nzuri na nyepesi ya kuondoa msongamano wa uchafu mwilini
- huwa kama sponji kwa kufyonza lehemu na mafuta mwilini na hii husaidia kupunguza uzito kwa kiasi kikubwa...
Inapatikana kwa bei ya sh 5000/= kwa pakiti moja .... Ni PM ( send message for more info)
 
SHAKE OFF PHYTO FIBER,
- Inaondoa tatizo la kukosa choo kwa haraka zaidi
- ni njia ya haraka iliyo nzuri na nyepesi ya kuondoa msongamano wa uchafu mwilini
- huwa kama sponji kwa kufyonza lehemu na mafuta mwilini na hii husaidia kupunguza uzito kwa kiasi kikubwa...
Inapatikana kwa bei ya sh 5000/= kwa pakiti moja .... Ni PM ( send message for more info)

huduma inapatikana wapi
 
Back
Top Bottom