Machinga; Je tunatatua Tatizo ambalo Halipo?

Machinga; Je tunatatua Tatizo ambalo Halipo?

Machinga complex ijengwe mbagala
Ijengwe tegeta
Ijengwe mbezi mwisho
Wakabanane hapo
Angalizo tu frame wapewe wamachinga wa ukweli

Ova
 
Ipo hivi machinga huwezi mjengea soko wala kumpatia eneo. Machinga hafanyi biashara kwa mtindo huo. Huku kujengea machinga vibanda na kuwapa maeneo ni kupotezeana rasilimali na wakati.

Piga marufuku machinga maeneo ya masoko, mjini nk. Machinga afanye kazi yake, azunguke majumbani kuuza vitu vyake.

NB hili bomu limetengenezwa na serikali yenyewe baada ya kuwa na sera mbovu za kilimo
 
Machinga complex ijengwe mbagala
Ijengwe tegeta
Ijengwe mbezi mwisho
Wakabanane hapo
Angalizo tu frame wapewe wamachinga wa ukweli

Ova
Ukifanya hivyo, yale maeneo waliyoondoka wataingia machinga wengine. Huwezi mjengea machinga soko.
 
Ipo hivi machinga huwezi mjengea soko wala kumpatia eneo. Machinga hafanyi biashara kwa mtindo huo. Huku kujengea machinga vibanda na kuwapa maeneo ni kupotezeana rasilimali na wakati.

Piga marufuku machinga maeneo ya masoko, mjini nk. Machinga afanye kazi yake, azunguke majumbani kuuza vitu vyake.

NB hili bomu limetengenezwa na serikali yenyewe baada ya kuwa na sera mbovu za kilimo
Tatizo hao so Called Machinga sio Machinga as we know them...., sijui tuwaitaje, ila ni (wafanyabiashara wasiofuata utaratibu); all in all hawa wadau ambao sasa hivi ni wengi kuwepo kwao ni matumizi mabaya ya Rasilimali Watu kwa Taifa letu lililobarikiwa maliasili
 
Viongozi wa serikali wakae na machinga kuangalia jinsi watakavyo wasaidia. Mitano ya wamachinga imetofautiana si wote wanamudu gharama za pango.

Kule East Street Market na Walthamstow market ni barabara zinafungwa na mchana machinga wanafanya biashara.
 
Machinga complex ijengwe mbagala
Ijengwe tegeta
Ijengwe mbezi mwisho
Wakabanane hapo
Angalizo tu frame wapewe wamachinga wa ukweli

Ova
Na kwa Mikoa mingine Arusha, Mwanza N.k? Pia Machinga wa kweli tunampimaje ? Na Frame wapewe au wakodishwe...

Sio kwamba nasema wazo ni baya ujenzi ni muhimu pale unapohitajika..., ila kabla hatujajenga huko, Mbagala, Tegeta na Mbezi Nadhani tuhakikishe kwanza masoko na Machinga Complex zimejaa na kuna uhaba wa maduka / fremu...

Ila kwa kumbukumbu zangu fupi hawa machinga / wafanyabiashara wa mitaroni kabla hawajapata dhahama na kuingia hasara kwa kuisubiri serikali ni vema kama wanauwezo wakaji-organise na kujibana sehemu ambazo watakuwa na uhakika wakirudi kesho, hawatakuta kibanda chao kimekumbwa na tingatinga jana usiku....
 
Viongozi wa serikali wakae na machinga kuangalia jinsi watakavyo wasaidia. Mitano ya wamachinga imetofautiana si wote wanamudu gharama za pango.
Tatizo kama taifa tumebaki na kazi kama mbili ambazo kijana anakimbilia nazo ni uchuuzi na bodaboda...,

Kila biashara ina kanuni na mahitaji, hao ambao hawamudu pango ndio wengine wanazunguka nyumba kwa nyumba mtu kwa mtu..., ingawa hio ni kazi ngumu sana ambayo kuiepuka huenda kushare pango kukawasaidia ingawa wengine kutembea kwao ndio kipato kinaongezeka..., all in all kama taifa / serikali haifai tujikite kwa kuwasaidia watu waendelee kuzunguka na kuchomwa jua bali ni kuwaondoa katika lindi la umasikini na kuingia katika sekta rasmi zenye uhakika....
Kule East Street Market na Walthamstow market ni barabara zinafungwa na mchana machinga wanafanya biashara.
Naam umeziita market ni uamuzi tu hata huku huwa kuna minada ya huku na kule..., hata tukiamua leo mji wa mwanza wote huwe ni mnada ni uamuzi tu ila bila kuhakikisha hatuendelei kuzalisha wabangaizaji soon or later utakuta kanda ya ziwa yote imekuwa mnada.... na watu wanachuuza na kuchuuzwa.

Binafsi nadhani kutoka kufanya biashara barabarani au kufunga barabara na kuwa na sehemu husika zenye miundombinu ya wateja na wafanyabiashara kiafya na kiusalama ni bora kuliko vinginevyo..., hata kama Cairo, Ujerumani hata Marekani wanafanya hivyo..., sio kwamba na sisi ndio tufanye
 
Ipo hivi machinga huwezi mjengea soko wala kumpatia eneo. Machinga hafanyi biashara kwa mtindo huo. Huku kujengea machinga vibanda na kuwapa maeneo ni kupotezeana rasilimali na wakati.

Piga marufuku machinga maeneo ya masoko, mjini nk. Machinga afanye kazi yake, azunguke majumbani kuuza vitu vyake.

NB hili bomu limetengenezwa na serikali yenyewe baada ya kuwa na sera mbovu za kilimo
Shida maana ya machinga hatujaielew vizur. Hawa jamaa wengine ni wateja wa hawa wanaopata vibanda wanatuletea mitaani huku
 
Back
Top Bottom