Macho yangu yananidanganya?

Macho yangu yananidanganya?

Magu anapendwa sana. Kuna tatizo moja kubwa sana la propaganda chafu ambazo zjnaendeshwa na kambi pinzani hasa kupitia mitandao ya kijamii. Lakini uhalisia kwa wananchi ni tofauti kabisa.

Tangu amefariki kambi pinzani wamefanya hate campaign kwa kasi kubwa zaidi. Na hata kudanganya dunia kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi mkuu. Angalia mtu kama Fatma Karume anachukua picha ya msafara sehemu ambayo hakuna makazi ya watu na kuzirusha eti watu wachache! na kuficha sehemu kubwa ambako kuna umati wa watu!

Yaani wanachuki iliyopitiliza na isiyo na sababu, kisha eti wanasema eti marehemu ndiyo alikuwa na chuki
Hizo media za kimataifa zimejibiwa na wananchi kwa urahisi sana. Kama wana akili wameelewa. Sisi tuendelee kuomboleza tu
 
Baada ya uchaguzi CDM walivyoitisha maandamano, rafiki yangu aliniambia hawa wanawajua waTz vizuri hawa? kama wanataka watu waandamane basi machinga wazuiwe au waondolewe kwenye maeneo wanakofanyia biashara hapo ndipo watu wataandamana, hivi hivi waTz wanatafuta mlo tu mambo yaliyo mengi hawaelewi yanawasaidiaje wao, hapo ndio wanasiasa wa chama dola wanapojizolea mashabiki zao.

Anyways to me, magufuli alikuwa na nia nzuri sana na nchi, his approach kuyafikia hayo mazuri ndio ilikuwa changamoto, plus ana issues in person ndio ikafanya things kuwa worse. hata hivyo amefanya pakubwa, apumzike kwa amani.
👏👏👏👏 Amen Kubwa
 
Mimi nilimpenda sana kwenye kupiga vita UFISADI!
Kwa kipindi chake cha miaka 6 ameweza kubadilisha tabia za wafanyakazi na wanabiashara wengi. Ninakumbuka alipoingia madarakani alianza kwa kupiga vita rushwa, kufanya ziara za kustukiza na kufukuza kazi watu hapo hapo. Lakini baada watu bado walikuwa hawabadiliki. Mfano bandarini alifanya ziara pale na waziri mkuu Lakini baada ya muda unasikia rushwa bado inaendelea. Mpaka nikawa nasema labda sisi Watanzania rushwa hatuwezi kuacha ipo kwenye damu.
lakini angalia sasa hivi watu wamebadilika hasa bandarini na maofisini. Watu wameamini wanaweza kuishi bila kutegemea rushwa. Imepungua sana kwa asilimia kubwa. Hata wapinzani wamekosa cha kuongelea.
Kama angebahatika kumaliza miaka hii mitano angekuwa ameshabadilisha mentality za wafanyakazi na wafanya biashara wengi kuhusu rushwa.
 
Jamaa alikuwa anapendwa tuwe wakweli Tu kama watu wanapita mpka kwenye njia zisizo halali pale taifa ili kumuaga Tu Mheshimiwa basi wanaosema alikuwa anachukiwa Wana lao Jambo japo ninkweli huwezi pendwa na kila mtu
Wangemleta Kimara
 
Ukweli u wazi kabisa Magufuli alikuwa kipenzi cha watu wengi sana na si Tanzania tu mpk nje.

Ukiwa huku kwenye mitandao unaweza kupata picha tofauti kuwa anachukiwa na dunia nzima.

Sasa wale maadui wa Watanzania kila muda wanabadili maneno wanapoona wingi wa Watanzania waliojitokeza, mpk mwingine anasema wanasombwa na malori!!
 
Niseme tu pia kuwa sipendelei mwili wake kuzungushwa zungushwa sehemu tofauti nchini, lakini naelewa.

Ila, if Dar is anything to go by, this guy was loved!

Leo mabodaboda wameongoza msafara wake kwenda uwanja wa Uhuru, tena kwa amani kabisa.

Wala hawakubugudhiwa na Askari.
Twitter wanajifanya hawaoni nyomi la Dar
 
Wakamzije haraka Hayati wetu mpendwa ili tushike fedha

Kuwa tajiri sio dhambi

giphy-3.gif
 
Kwa JPM ni Unafiki ila kwa Lisu ni “upendo wa watu” akili za Ufipa.
wachache wameguswa ila wengi ni ma snitch hata humu wamo hata wewe unaweza ukawa mmoja wao

Kuna watu wameonesha kuguswa kwa mambo yao binafsi ya ki financial kwenye maswala yake ya ulaji ambayo yanaonesha wazi kwamba endapo wangepata uhakika wa kuendelea kuwa favored na huu utawala wasingeweza kuona pengo la JPM

Imagine mtu anakuambia anahuzunika kifo cha jpm kwasababu alikuwa na uhuru kufungua kibanda kando ya ofisi ya takukuru. Mtu huyu anatuonesha kwamba hana utu wala upendo bali anajari maslahi yake ameonesha hana uhakika wa kuendelea kudumu kwenye hicho kibanda kwa utawala wasasa na ndio kitu kinachomfanya aone thamani ya jpm.

Kwa maana kuwa huyu mtu angehakikishiwa kuendelea kubaki kwenye hicho kibanda asingeweza kuumia swala la jpm kufa
 
Kwa kweli 'wanyonge' tulikuwa tunampenda na tutammisi
 
Unapohutubia angalia aina ya makofi unayopigiwa , kuna wanaopiga makofi ili kukupongeza lakini wengine wanakupigia ili umalize hotuba ujiondokee zako na wao wachukue hamsini zao , kule kwetu Kyela kuna mnyama anaitwa Kindingo , huyu alisumbua watu sana kwa kula mifugo yao , sasa siku aliponaswa wilaya nzima ya Kyela ilikusanyika Kajunjumele ,

........Itaendelea ....
 
Ayubu 24:19-20.

“Ukame na joto vinayameza maji ya theluji na hivyo hivyo kaburi kwa wanaotenda dhambi”.

“Tumbo lililomzaa litamsahau; minyoo wa ardhini watamla kwa furaha; hatakumbukwa tena; na uovu utavunjwa kama kijiti.”

Hii ni kwa kila mmoja wetu sisi wadhambi mara mauti inapotukuta bila kujali ukuu wa mtu au wangapi waliomboleza.

No offence meant, no sides taken.
 
Ayubu 24:19-20.

“Ukame na joto vinayameza maji ya theluji na hivyo hivyo kaburi kwa wanaotenda dhambi”.

“Tumbo lililomzaa litamsahau; minyoo wa ardhini watamla kwa furaha; hatakumbukwa tena; na uovu utavunjwa kama kijiti.”

Hii ni kwa kila mmoja wetu sisi wadhambi mara mauti inapotukuta bila kujali ukuu wa mtu au wangapi waliomboleza.

No offence meant, no sides taken.
Na Ili iwe dhambi kunapaswa mtu afanye mambo yepi?
 
Kifo cha Magufuli kilikuwa habari ya dunia.

Kwa mtu aliyekuwa hasafiri sana nje ya nchi, sikujua kama watu wa mataifa mengine walikuwa wanamfuatilia kiasi hicho.

Kifo chake kilikuwa headline news kwenye vyombo vikubwa vya habari vya kimataifa!
Nilishangaa sio CNN, BBC, AFP, REUTERS, DW, XINHUA Wote wanaripoti kifo chake wakati hajawahi kwenda Ulaya ,walikuwa wanamfuatilia Sana.
 
Lissu alimdhihaki Nyerere, lakini kwa vile alijuwa anapendwa wakati wa kampeni alienda mpaka nyumbani kwake na familia yake ikampokea kwa moyo mkunjufu.

Tunajua hamuamini mnachokiona,mlidhani hapendwi na watu eeh! Tunawasubiri 2025,ndiyo mtatujua vizuri Watanzania. Endeleeni na “kuendesha Nchi kupitia twitter” but mkija huku Site kuomba kura mtatukuta.
 
Back
Top Bottom