Kamukhm
JF-Expert Member
- Aug 30, 2015
- 2,801
- 4,212
You areHilo haina faida kwasababu hawezi kufufuka, atazikwa na kisha atasauliwa. Inawezekana Mungu amesikia kilio na manung'uniko ya watu juu ya kauli zake za kejeli, juu ya aina ya uongozi wake wa ubabe asiotaka watu kuwa huru wa kutoa maoni, kushauri na kufungia vyombo vya habari wanaotoa habari asizotaka zitaka yeye kuzisikia masikio mwake, watu ambao familia zao zilikumbwa na kukosa ajira tokea wamalizie vyuo wanaambiwa wajiajili nawakati mitaji hawana.
Wanafunzi wengi wa vyuo wameishia kubaki mitaani na wengine wamekuwa wauzaji wa matunda kariakoo.
Watu waliokumbwa na bomoa bomoa kule kimara bila kulipwa chochote halafu wanasikia kauli kuwa Mwanza hatofanyiwa hivyo kwasababu ni wapiga kula wake. Eeh ndio niwapiga kula wake.
Waajiriwa wa serikalini wamekuwa na kilio tokea anaaingia madarakani hakuna kupandishwa daraja wala mshshara. Waliomba hilo mpaka basi lakini kwenye kilele cha Mei mosi wanaishia kupewa majibu ya kejeli.
Katika awamu ambayo muhimili wa bunge umeonekana hauna kazi basi ni awamu hii. Raisi amekuwa akifanya manunuzi bila ushirikishwaji, amefanya miradi na kuingia mikataba bila ya ushirikishwaji hivyo amekuwa mtu aliyekuwa na usiri mwingi katika mambo yaliyofanyika kama ni upigaji wa kodi ya wananchi basi umepugwa hasa.
Wafanyabiashara wakubwa wamekumbana na ongezeko la Kodi na imepelekea baadhi ya biashara kufungwa na baadhi makampuni yalipunguza idadi ya watu hivyo kuongeza idadi ya wakosa kazi mitaani.
Wakulima wa korosho waliipata vizuri
Miradi ya maendeleo huko vijijini ikawa sio wajibu wa serikali tena bali ikawa ni wajibu wa wananchu, watu wanalazimishwa kuchangia ela ili ijengwe shule, madarasa na mazahanati kamahauna ela unaweka ndani.
Tumeona uchatolization, kapeleka miradi mingi mikubwa mkoani kwake chato tena kwa kipindi kifupi tu.
Ukiachana na wamachinga, boda boda na mama ntilie, makundi mengi yaliyobakia yameisoma namba ipasavyo.
Kama unaona ufahali kuzungushwa ndio kupendwa na wengi, basi hao wachache hata wakiwa kumi tu Tanzania nzima watakuwa ni washindi kwa hilo kwasababu hata wakijaa watu Africa nzima hakuwezi kumfanya arudi. Mungu ni wa wote hakuna anayemzidi nguvu na uwezo na hakika wote kwake tutarejea.
Bitter...
And I don't see how Magufuli and what they do with his body is hurting you!?
What's the connection!?