Ukitoa hivyo virefu vyake Cdma na Gsm ni standard za mitandao ya simu.
Cdma ni standard ya marekani na makampuni yake kina Verizon, Sprint wakati huo bila kumsahau alieitengeneza Qualcomm.
Gsm ni standard ya Ulaya kina Nokia, Ericson na baadhi ya mitandao ya Japan huko.
So wakati huo walikua wanagombania wateja, kila mtu anataka Standard yake itumike dunia nzima, ndio maana hapa kwetu ukakuta Mitandao kama Zantel, TTCL, Sasatel wanatumia Cdma wakati huo na kina Voda, Tigo, Airtel wapo Gsm.
Sema mwisho wa siku Gsm akashinda na kuanzia technology ya 4G kukawa hakuna tena mambo ya Gsm na Cdma dunia nzima tu Katumia standard moja.