Mada fikirishi kuhusu ndoa

Umesema kweli kabisa..
 
Kama mdau alivyosema hapo juu nadhani hatujui au tumesahau majukumu yetu.. Wajibu wa wanaume hautekelezeki na pia wajibu wa wanawake
 
Vijana wakiachana na mawazo ya kupata mwenza wa kusaidiana maisha na ku-stick kutafuta mama walezi wa watoto wao taasisi itarudi ktk ubora wake.

Tafuta leo aliyeoa mama wa nyumbani na aliyeoa mfanyakazi utaelewa nachomaanisha hapa.
Labda tujue sababu inayompelekea kijana kuoa ni nini.. Umri? Familia? Au sababu nyinginezo
 
Ndoa ni mpango mtakatifu tangu mwanzo, ujumbe mwema utokao kwa Mungu, yahitajika hekima kuitunza hadi kifo kiwatenganishe.

Mke sio kidude cha kujaribu miguu yako, Mume si kipaza sauti cha kupigia kelele.

Mpendane, msichokozane Amani ya Mungu iwe ndani yenu.🐒

Christ Saint
 
Mimi toka mwanzo nilikuwa nafikiria kuishi huru kama ndege wa porini,ndoa ni kujinyima uhuru
Mimi experience yangu ya udogoni ilichangia nione kama mahusiano na ndoa ni uzushi nikawa na mtazamo mbaya juu ya ndoa. Lakini jinsi nilivyoendelea kukua nimekuja kuna ndoa sio zote ni mbaya.. Na imenifanya kufikiria kwa na ndoa/familia kwa ujumla.. Natamani sana kuna familia yangu katika malezi ya pande zote
 
Kweli..
 
Tumemkataa Mungu, akatuachia tujikate na kiwembe tunacholilia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…