nilipewa baiskel ambayo haina breki kutoka kwa rafiki yangu kwa lengo la kuibariki kwa kupiga round mbili tatu na mwenyewe hakuniambia kama hakuna breki.
niliendesha kuushuka mteremko,aiseee nilipokuja kugundua chombo haina breki ndivyo na yenyewe ilivyozidi kukimbia zaidi.
kwa wenyeji wa ubungo nilipofika usawa wa kanisa la gwajima kutokea rombo/kibo nilikuta wafanya biashara wametandaza bidhaa zao chini enzi hizoooo za JK kama ilivyo kariakoo.
baada ya kuwakwepa woooote ki JAMES BOND kulaleki niliparamia kwenye banda la muuza miwa nadhani yule mwana hata nisahamu kwa jinsi nilivyo-m-surprise.
kilichotokea baiskeli ilibaki ndani mimi nikatokezea upande wa pili wa banda kutokana na speed kali nikawa nimedondoka pale.
siku hiyo nilijaza watu sitasahau kwa aibu niliyoipata kwani badala ya kuwa baraka ya baiskeli ikawa balaa la baiskel
Sent using
Jamii Forums mobile app