Fikra za hivi ndiyo zinatufanya Wa-Afrika tuwe maskini na kila kizazi kiwe kinaanza maisha na sifuri. familia ni baba, mama na watoto tu. kuwasaidia wazazi au ndugu zako ni kuwadhulumu watoto wako, pia siyo lazima.
Nini kifanyike. mtu anapomleta mtoto Duniani, inatakiwa amlee mpaka afikishe umri wa kujitegemea, wakati huo huo ajipange na maisha yako ya uzeeni, mtoto anapoanza maisha, mzazi anatakiwa kumpa mtoto kianzio cha maisha. Mfano: Fedha, nyumba, mifugo, shamba au Gari. Hivi ndiyo jamii zilizoendelea zinafanya, Mfano wa jamii hizi ni Waarabu, Wahindi na Wazungu.
Watu weusi lazima tubadilike kwenye swala la kuhamisha uchumi kutoka kwa baba kwenda kwa watoto na siyo kutoka kwa mtoto kwenda kwa baba. watoto tunawajibu wa kuwalea wazazi kijamii na siyo kiuchumi. Tukifanya hivi vizazi vijavyo vitaishi vizuri kiuchumi.